Ni wakati sasa kwa Serikali kumuomba radhi Tundu Lissu aliyeshauri mapema kuachana na madai ya Barrick

Ni wakati sasa kwa Serikali kumuomba radhi Tundu Lissu aliyeshauri mapema kuachana na madai ya Barrick

Kuwa kiongozi Jamhuri ya wadaganyika hata kichaa inawezekana tu ,Leo hii wote waimba mapambio sijui wataficha wapi sura zao au na wao watacheza kulingana na mdundo unavyopigwa ?

Cha kutuokoa kama nchi ni katiba mpya tu vinginevyo tutakuwa tunaendelea hatua tatu mbele halafu tunakuja rudi nyuma hatua hamsin
AMEN
 
U
Kwani kuna ubaya upi kutumia vitu hivyo! mbona sisi huku mtaani nilivitumia na akuna Mtu aliyeguswa na coronavirus,na mpaka Sasahivi akuna aliyepigwa chanjo na tunadunda kama kawa.Sio kila kitu anachofanya mzungu kinafaa asilimia zote,ndio Maana kwenye fom zao za chanjo walijiondoa pamoja na serikali ili likitokea jambo wasilaumiwe.
Ndio maana umesema ni wewe , kaa ukifahamu kuna watu walihitaji chanjo pia kwanini wanyimwe haki hiyo na kushurutishwa kunywa michanyato.
 
Ripoti za Mruma na Osoro juu ya Barrick/Acacia kulimbikiza deni hadi kufikia Trln 425 zilizua mjadala mkubwa ambapo aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alizikosoa na kuziita ni “Professorial Rubbish Report”.

Lissu alitoa ushauri wake kuwa kutokana na repoti hizo Barrick hawatalipa hilo deni na wakilazimishwa wakienda MIGA watashinda. Lissu alibezwa alipuuzwa na baada ya siku chache alimiminiwa risasi kuwa ni msaliti anayeshirikiana na mabeberu.

Barrick walitoa fedha za (Good faith) US$ 300M sawa na tsh 700b tu kati ya deni lote.

Jana Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kwa niaba ya serikali amesema serikali imeisamehe Barrick/Acacia deni lote.

Uungwana ni vitendo mnyonge mnyongeni lakini haki zake apewe, Tundu Lissu aombwe radhi.

June 19, 2017
View attachment 2366316
Lissu again has proven them Wrong
 
Aliyesema tutashitakiwa Miga aombwe msamaha kwa lipi au atuombe radhi sisi kwa aliyotuhadaa kwa kutaka kututia uwoga

Na JPM angeliogopa tusingepata 700b yetu

Yeye Lissu atuombe msamaha sisi
MIGA naona wengi wetu wameshikilia kushtakiwa lakini wamesahau tulifikaje huku. Serikali yetu sikivu ilianza kutishia KUTAIFISHA mali za acacia na ndipo lissu akashauri mkienda kichwa kichwa mtapelekwa mahakamani. Kama nia yenu ni hiyo lazima kwanza mjitoe MIGA. JPM akaspin kuwa lissu anasema tukiwachukulia hatua acacia tutashitakiwa. Wengi wakamwamini JPM na kumuona lissu mtu wa ajabu. Serikali hawakutaifisha hivyo issue ya Miga ikawa mfu.
 
MIGA naona wengi wetu wameshikilia kushtakiwa lakini wamesahau tulifikaje huku. Serikali yetu sikivu ilianza kutishia KUTAIFISHA mali za acacia na ndipo lissu akashauri mkienda kichwa kichwa mtapelekwa mahakamani. Kama nia yenu ni hiyo lazima kwanza mjitoe MIGA. JPM akaspin kuwa lissu anasema tukiwachukulia hatua acacia tutashitakiwa. Wengi wakamwamini JPM na kumuona lissu mtu wa ajabu. Serikali hawakutaifisha hivyo issue ya Miga ikawa mfu.
Mwigulu amethibisha jana kuwa serikali imenyosha mikono.

Lissu ni genius hakurupuki na hajawahi kukurupuka.
 
Negotiation skills ya high level,
Hamuwez kuelewa ule mchezo ulichezwaje, ila its was a perfectly executes negotiations, kuanzia kwenye madini mpaka kwenye mawasiliano.
 
Kila kitu kilifanywa kwa usiri mkubwa, halafu Magufuli akawa anawahadaa wetu kwa kuwaita viongozi wa dini , sijui makundi mbalimbali kwenye hizo hafla za utapeli wake. Cha kushangaza watu walikuwaje wajinga kiasi kile cha kuamini maigizo yale.

Halafu bunge lilikuwa halishirikishwi kabisa kwenye mambo yale, kisa Magufuli alikuwa hataki yajadiliwe bungeni maana wabunge wa upinzani wataweka wazi mambo hayo. Mambo haya ndio yalipelekea Magufuli anajisi chaguzi za nchi hii na kujaza wanaccm aliowataka yeye ili kusitokee yoyote wa kuhoji. Jambo hili ndio lilipelekea Lisu kupigwa risasi.
Lissu ni foreseer
 
Hivi ni halali kuiita ripoti za Professor Osoro na Mruma kuwa Professorial Rubish kabla kufanya utafiti mwingine wa kisayansi ili kupata matokeo sahihi.Kwa sasa mtazamo wangu katika taaluma ya Research mpaka sasa Ripoti za Professor Osoro na Mruma ni sahihi mpaka pale itakapofanywa study nyingine.Kwaiyo katika jicho la kitafiti yeye Lissu hoja zake ndiyo Rubish!
Kwa wale ambao tupo au tumewahi kufanya kazi za Research and Consultancy nadhani mmenielewa
 
Pia unaweza kukokotoa namna hii.

300 000 000 ÷ 191 000 000 000 =

(3 ÷ 1910 ) × 100 = 0.157 %

Barrick wamelipa 0.16% ya deni lote.

Makisio ya haraka ni sawa na mtu akuibie sh 1000 halafu wewe ukubali akulipe senti 16.
Wangelipa hata asilimia 20% ya deni lote japo kwa awamu, kulipa tsh. 0.7tril kati ya tsh. 400+trilion ni dharau au walitulisha propaganda hawa inzi wa kijani. Pumbafu.
 
Back
Top Bottom