Kila mwenye akili timamu alijua kuwa madai yale ulikuwa uwongo mkubwa. Ni sawa uambiwe kuwa mwenye duka la mtaji wa 2m anadaiwa kodi ya sh 2 bilioni. Lazima uwe punguani kiasi kuweza kuliamini hilo.
Total gold resource ya migodi yote ya Barrick kwa Tanzania ni 0.75MOz Tulawaka + 4MOz Buzwagi + 7MOZ North Mara + 12MOZ Bulyanhulu = 23.75MOz. Mineable resource haiwezi kuzidi 60% = 14.25MOz. Dhahabu iliyokwishachimbwa, japo sina uhakika, haiwezi kuzidi 50%.= 7.1MOz. Thamani ya hii dhahabu iloyochimbwa, kwa bei ya juu kabisa, ya U$2,000 kwa oz = $14 billion (14 billion ×2,300 = TZS 32 trillion)
Hata ungesema hiyo hela yote iwe kodi, halafu wasiwe wametoa kodi hata shilingi moja, bado haifikii hata 10% ya trilioni 360 ambayo waliotuona wajinga walikuwa wakituaminisha.
Hata kama walitaka kuwadanganya wananchi, wangeweka huo uwongo wao uwe unakaribia na ukweli. Lakini wahusika kwa vile walijua wanaongoza nchi ya wasio na kitu vichwani, walijua wapo wenye vichwa vitupu kabisa, ambao ni wengi, watashangilia na kuwaona ni mashujaa. Uwongo ule ni miongoni mwa mambo yaliyotufanya waafrika tuendelee kuonekana kuwa siyo binadamu timilifu.
Kwa namna ambavyo baadhi ya watu wakati ule walivyokuwa wameshibishwa ujinga, hata wangeambiwa kuna mpango wa Serikali wa kumnunulia kila mwananchi ndege aina ya Boeing 737-800, wangeshangilia na kusema tumepata mkombozi. Ujinga ni laana kubwa, hasa ujinga ule unaoelekea kwenye upumbavu.