Ni wakati sasa kwa Serikali kumuomba radhi Tundu Lissu aliyeshauri mapema kuachana na madai ya Barrick

Mayala, sijui nitumie neno gani, maana nisijekutafsiriwa vibaya, ilihali heshima yangu kwako haijawahi kukosekana.

Kwa ufupi kabisa, niseme tu kuwa, utumie akili na maarifa yako vizuri. Kujifanya mjinga wakati una akili ni kudhihaki kazi ya muumba wetu aliyetujalia ufahamu.

Hakukuwa na deni la trilioni 360, hivyo hakukuwepo na msamaha. Hakuna tulichosamehe, bali tuliomba tupewe chochote, tukakubaliwa kupewa $300m ndani ya kipindi cha miaka 7, na hizo pesa zitakuwa zinatoka kwenye mauzo ya makinikia. Installment ya kwanza itakuwa baada ya kuruhusu makinikia yaliyozuliwa, yasafirishwe. Tukatii amri. Halafu tukasaini makubaliano kuwa, kwa vyovyote iwavyo, siku za mbeleni, hata kukiwa na mgogoro, kamwe hatutazuia usafirishaji wa dhahabu wala makinikia, tutaenda kwenye meza ya mazungumzo. Suluhisho lazima liwe limepatikana ndani ya siku 30. Ikishindikana, mahakama ya biashara ya Singapore itaingilia kati na kutoa maamuzi, na maamuzi yake hayatakatiwa rufaa mahali popote na upande wowote.

Hatukuwa na madai, hatukutoa msamaha kwa sababu hakukuwa na chochote tunachokidai, tulipewa pesa ya msaada, kama tunavyosaidiwa na mataifa wahisani.
 
Soma matamshi ya waziri wa Sasa wa fedha kumbeza TAL kwenye hilo gazeti la wakati ule ufahamu kwa nini wamuombe radhi
Pia kuna suala la jaribio la kumuua ambapo kuna hisia kuwa linahusiana na msimamo wake was hiyo professiol rubbish
 

Cha ajabu uongo ule wa wazi ulikuwa unashabikiwa hata na the so called wasomi!
 
Soma matamshi ya waziri wa Sasa wa fedha kumbeza TAL kwenye hilo gazeti la wakati ule ufahamu kwa nini wamuombe radhi
Pia kuna suala la jaribio la kumuua ambapo kuna hisia kuwa linahusiana na msimamo wake was hiyo professiol rubbish
Kwaiyo tumeshitakiwa MIGA kama madai ya Lissu alivyokuwa akituogepesha kuwa watatunyoa kwa vipande vya chupa pasipo kutumia maji?kweli ujinga hautaisha nchi hii.
 
Tundu Lisu huyu huyu wa Ufipa st?

Serikali ilimsomesha bure huyo TAL ujue!
Kwani kusomeshwa bure ndio kigezo cha kutoikosoa serikali?

Maana ya kwenda shule ni kufuta ujinga sasa kama umekwenda shule halafu bado unaona mafyongo ndio ukae kimya kisa ulisomeshwa bure?

Wasomi wangapi wamesomeshwa bure na wameishia kuchemka tu hebu acha lame excuses mnazofundishwa Lumumba huko kuwa fikra za mwenyekiti lazima zidumu.
 
Sasa aombwe msamaha wa nini?
 
Naona kama kawaida Chadema wamevamia hii issue, hawajui purpose ya kuibuka kwake! Hawajachunguza facts za hili jambo, tayari wamebeba mwenge! Haya mambo yamejaa sarakasi ambazo ukikurupuka utatumika kama daraja huku ukibakia pale pale [emoji17]

Tutakumbushana ...
 

Nimecheka, baadhi ya wasomi mliokabidhi akili zenu wakati ule wa zama za giza! Unakosoa kistaarabu uongo?! Kwa taarifa yako huyo Lisu aliyekosoa kwa lugha kali utapeli ule, alieleweka kuliko nyie mlikuwa mnajidai kukosoa kistaarabu. Viongozi wetu wa kiafrika huwa hawajirekebishi wakikosolewa kistaarabu.
 
Kuna muda nakuona huna akili timamu.
Je una uhakika alisomeshwa bure?
Hivi unajua hata ile mikopo sio bure bali ni deni ambalo mnufaika analipa akimaliza masomo.
Kuwa na akili kidogo basi, punguza ujinga.
Yes tulisoma naye Ilboru ilikuwa ni bure hadi nauli iliyokuleta unawasilisha risiti kwa School Basa unarudishiwa fedha zako. Siku ya kufunga shule unapewa warrant una safiri bure.

Chuo Kikuu, pia kasomeshwa bure LL.B , UDSM
P
 
Aliyesema tutashitakiwa Miga aombwe msamaha kwa lipi au atuombe radhi sisi kwa aliyotuhadaa kwa kutaka kututia uwoga

Na JPM angeliogopa tusingepata 700b yetu

Yeye Lissu atuombe msamaha sisi
 
Sasa aombwe msamaha wa nini?
Kwani msamaha tafsiri yake ni nini?

Ukisema kusomeshwa nje ni kigezo cha kutokosoa aliyekusomesha ni ujinga mpevu.
Imagine hapo pichani kuna msomi aliyesomeshwa kwa kodi za watanzania Urusi miaka 7 ila wewe unasema ni "bure" alisema hakuna umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO bali watanzania wanywe michanyato ya tangawizi na mananasi je watu watanzania wangapi walipoteza wapendwa wao lini wataombwa msamaha kwa upotoshaji mkubwa kama huu.?
 
Wewe unajulikana una chuki binafsi na Tundu Lissu hilo halina mjadala. Mbona best wako Mwigulu Nchemba alivyochana bajeti kivuli ya kambi ya upinzani kwa maneno ya kejeli kubwa Bungeni hukutia neno? Wewe una chuki binafsi na Tundu Lissu na unaichukia Chadema kwa nguvu zako zote.
 
Behind the scene inasemekana ripoti ya Prof Mruma ilikuwa vizuri. Ila yeye Jiwe ndiyo akaiharibu especially pale kwenye content ya gold ndani ya container. Mruma aliandika 0.7 Kg of gold per 20 ft container. Akamuambia toa hiyo point, ndipo Mruma akatoa na ikabakia 7.0 Kg per container.


Kama Tsh 360 Trillion ni thamani ya kodi waliyokwepa ACACIA kwa containers hizo tu za 1998-2017, kiasi cha gold ambayo imetoka Tanzania basi kilikuwa kinafikia 110,000 Tons through makinikia leave alone zile bars wanazo declare mgodini. Kama magufuli angekua na akili sawasawa angejiuliza vizuri je ni kweli tunayo dhahabu hiyo kwenye migodi yetu? Pili angeangalia deposits za gold Dunia nzima kwa 2017 zilikuwa 230,000 Tons. Meaning Tanzania ime supply 50% ya Gold duniani. Something that is not true! Tanzania haipo kati ya top 5 countries zenye gold minerals.

Halafu kabla hajapeleka madai ya USD 190 B angejiuliza Networth ya Barrick na Acacia ni ngapi? Maana makampuni yaliyo na net worth zaidi ya USD 100 Billion ni akina Tesla, Bill Gates, Warren Buffet na Bloomberg. Anyway Mungu alijuwa kati ya Lissu na Magufuli nani ndiyo mkweli, then March 17, 2021 akatoa hukumu ya kweli. Magufuli yuko Jehanam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…