SoC02 Ni wakati sasa wa kumaliza vita hii ya vijana dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia

SoC02 Ni wakati sasa wa kumaliza vita hii ya vijana dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
VITA YA VIJANA DHIDI YA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Chemsha bongo!
Je! Umewahi kujiuliza kuwa licha ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kusaidia katika kuboresha maisha ya binadamu kiujumla lakini bado yameacha malumbano makubwa dhidi ya vijana mbalimbali?
Ukweli ni kwamba vijana wengi hususani wanaotaraji kuajiriwa, walioajiriwa na hata ambao wamejiajiri wamezua vita baridi dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia katika sekta mbalimbali wakiamini kuwa ukuaji huo umekwenda kuchukua nafasi zao walizokuwa wakitaraji kuzitumikia.

Je! Ni kweli kuwa kitafika kipindi ambacho kutakuwa na mapinduzi makubwa ya kisayansi na teknolojia ambayo yataondoa watu wote katika nyanja mbalimbali huku kazi zote zikiendeshwa na mashine zenye teknolojia ya hali ya juu?
Haya ni baadhi ya maswali yaliyoacha sintofahamu kwa baadhi ya vijana mbalimbali ambayo yanahitaji ufumbuzi ili kuwaweka huru na kujenga imani kwa vijana ili waweze kuona manufaa na uhitaji wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Hivi sasa mapinduzi ya sayansi na teknolojia yamefanikiwa kuathiri karibu kila sekta huku yakiwaacha nyuma watu wengi ambao baadhi yao hugeuka na kutupa lawama zao katika mapinduzi hayo ya sayansi na teknolojia pasipo kujali manufaa tele yaliyoletwa kwao.

Je, ni kweli kuwa mapinduzi ya sayansi na teknojia yamesababisha wimbi kubwa la vijana wasio na ajira mtaani?
Ukweli ni kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yametia chachu katika ukuaji wa maendeleo nchini hususani katika maboresho ya utoaji wa huduma mbalimbali ambapo imechangia pia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa ajira mbalimbali. Lakini pia mapinduzi hayo yameongeza wimbi kubwa la upotevu wa baadhi ya ajira za vijana katika sekta mbalimbali. Lakini ni dhahiri kuwa bado maendeleo hayo yameleta matokeo chanya zaidi kuliko athari hasi.

Tazama picha zifuatazo kwa umakini kisha ung’amue dhamira kuhusiana na athari ya maendeleo ya sayansi na teknolojia katika jamii.
IMG_202208216_134727533.jpeg

Picha ikiwaonesha matabibu wakitoa huduma kwa mgonjwa.
(Melnick Medical Museum)

Tazama pia picha ifuatayo kisha jaribu kuhusianisha na picha iliyoainishwa hapo juu.
IMG_202208216_012453731.jpeg
Picha ikimuonesha mtoa huduma ya afya akiwa na mgonjwa. (Picha yangu, Chuo cha Afya, Muhimbili)
Je! umegundua nini kutoka kwenye picha hapo juu?
Dhahiri utagundua kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yameweza kuboresha urahisi wa utoaji huduma yenye ubora wenye kiwango cha hali ya juu lakini ikiambatana na upunguzaji wa uhitaji wa watoa huduma katika sekta mbalimbali kama ilivyooneshwa katika picha. (matabibu watano hadi tabibu mmoja kwa mgonjwa).

Mapinduzi ya sayansi na teknolojia yameweka wimbi kubwa la maswali hususani kwa vijana ambao wameweka imani na matumaini yao juu ya kuajiriwa katika sekta mbalimabali. Mfano mzuri huonekana hata katika baadhi ya makampuni yaliyokuwa yakiajiri watu wengi kupunguza idadi ya waajiriwa kwa kiwango fulani , kwasababu baadhi ya kazi zikionekana kurithiwa na nguvu kazi mashine badala ya nguvu kazi watu.

Je! umewahi kufikiria, jinsi kamera za ulinzi (kamera za CCTV) zilivyopunguza idadi ya walinzi katika taasisi au kampuni fulani? Mashine za kufanyia usafi zilivyopunguza idadi ya wafanyakazi katika sehemu husika?
Matumizi ya mitandao katika kupakua filamu mbalimbali yalivyo athiri soko la Mikanda ya filamu/video CD(Compact Disc).
Haya ni baadhi ya maeneo machache yaliyoacha sitonfahamu juu ya watu waliokuwa wakiyatumia kama chanzo kikuu cha mapato yao katika maisha yao ya kila siku.

Je, ni nani atakayeibuka mshindi katika vita hii?
Hadi sasa kumekuwa na vita baridi juu ya pande mbili zinazolumbana (watu wasio na ajira dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia). Lakini, Kitu kikubwa tunachopaswa kufahamu ni kuwa kamwe mapinduzi yote haya yakiteknolojia bado yanahitaji uwepo wa nguvu kazi watu.

Pia tukumbuke kuwa mapinduzi yote haya ni matunda yanayozalishwa kutoka katika fikra zetu wenyewe, hivyo kwani hata wahenga walisema “usiogope kivuli chako kwakuwa kinyago ulichochonga mwenyewe hakiwezi kukutisha.”

Ukweli utabaki kuwa, mapinduzi ya sayansi na teknolojia hayana budi kutujia kwahiyo ni wakati wetu sahihi wa kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko hayo ili tuweze kufaa na kubaki katika mifumo stahiki itakayo tuwezesha kufanya kazi katika mazingira hayo ya makuzi ya sayansi na teknolojia. Hivyo basi, ni wakati sahihi kwetu kutafakari njia thabiti zitakazotuwezesha kufikia tamati ya vita hii baridi baina ya sayansi/teknolojia dhidi ya vijana wenye kusaka ajira katika sekta mbalimbali.

Nini kifanyike kumaliza vita hii?
  • Ni wakati sasa kwetu kutambua na kushiriki fursa au matukio mbalimbali yahusuyo vumbuzi mbalimbali zenye kuleta tija na manufaa kwa jamii. Mfano katika sekta ya afya, uvumbuzi wa “mkanda salama” uliofanywa na wanafunzi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, kama ilivyoainishwa katika picha hapa chini.​
image_search_1659552812640.jpg

Picha inayoonesha wanafunzi wa chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi wakielezea kuhusu uvumbuzi wa mkanda salama unavyoweza kuzuia tatizo la kutokwa na damu nyingi kwa wanawake wanaojifungua.(picha kutoka mtandaoni)


image_search_1659552998445.jpg

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Usafirishaji (NIT) wakionesha gari walilobuni jinsi linavyofanya kazi.teknolojia.(picha kutoka mtandaoni)
Haya ni baadhi ya maeneo machache yanayoonesha jitihada za vijana dhidi ya ukuaji wa teknolojia.

  • Pia, ni wakati sahihi kwetu kushiriki matamasha au makongamano mbalimbali yanayohusu uelimishaji dhidi ya mabadiliko na ukuaji wa sayansi na teknolojia. Mfano, katika sekta ya afya, kongamano la kisayansi lililofanyika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili tarehe 14-15/07/2022. Hii husaidia kuandaa fikra zetu dhidi ya mabadiliko mbalimbali yahusuyo mapinduzi ya sayansi na teknolojia, kwani ni heri kuitangulia teknolojia kuliko ikufike ukiwa hujaandaa fikra zako kuhusu mabadiliko hayo maana hata wahenga walisema “zimwi likujualo halikuli likakwisha”.​
  • Lakini pia, kitu muhimu zaidi ni kuruhusu au kufungua akili zetu kupokea mafunzo mbalimbali bila kujali kiwango chako cha elimu au aina ya elimu tuliyoipata. Mfano, unaweza kuwa umesomea masuala yahusuyo afya, elimu, sheria, kilimo n.k lakini pia ukajihusisha na mafunzo mbalimbali kuhusu tehama. Hii itasaidia kupata ujuzi mbalimbali utakaowezesha kuendesha baadhi ya shughuli za kiteknolojia katika sekta zetu husika, kama vile ufundishaji kwa kutumia kompyuta (tarakilishi) mfano vipindi kupitia mtandao (Zoom), matumizi ya nyenzo bora za kisasa katika kilimo, utumiaji wa mitandao katika biashara n.k. hivyo kumfanya mtu kufaa katika maeneo mbalimbali.​
  • Sambamba na yote kitu kikubwa zaidi ni kuwa kamwe hatuwezi kufikia tamati ya vita hii kama hatutakubaliana na hali halisi ya dunia ya sasa hivyo ni wakati sahihi sasa wa kukubaliana na ukweli uliopo, ni lazima tuendane na mabadiliko hayo kwani tusipo ambatana nayo ni dhahiri kuwa tutaachwa nyuma mwishowe tunaweza kuondolewa katika mifumo mbalimbali ambayo tumekuwa tukifikiria kila siku.​
Mwisho wa yote, japo si kwa ubaya tunaiomba pia serikali itambue vipaji mbalimbali vya vijana wenye uthubutu katika vumbuzi mbalimbali za kiteknolojia kwa kuwashika mikono ili kuwatia moyo kwa kutambua jitihada na uthubutu wao ili waweze kutimiza malengo yao. Mfano, kuwapatia mafunzo endelevu katika nchi zilizoendelea ili kuendana na mifumo halisi ya jinsi dunia inavyokwenda na mahala ilipofikia.
 
Upvote 32
VITA YA VIJANA DHIDI YA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Chemsha bongo!

Je! Umewahi kujiuliza kuwa licha ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kusaidia katika kuboresha maisha ya binadamu kiujumla lakini bado yameacha malumbano makubwa dhidi ya vijana mbalimbali...
 
Vita hii ni kaliiii sana! Watu wanasikilizia tu wakisikia serikali imeleta vifaa fulani, wanaanza kuwaza vibarua vyao.
 
This is great idea! Congratulations tunahitaji vijana wenye kiu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
 
Tena, kwenye suala la vijana wanaofanya vumbuzi mbalimbali ndio la kutilia mkazo, kuna yule kijana aliyekuwa na Redio yake kule Kigoma asiishie tu pale serikali impeleke mbali zaidi maana ana kipaji kikubwa sana. Hongera kijana kwa kufungua fikra zetu.
 
Vita hii ni kaliiii sana! Watu wanasikilizia tu wakisikia serikali imeleta vifaa fulani, wanaanza kuwaza vibarua vyao.
Kweli Kiongozi ndio maana nimependekeza iwepo haja ya kuwaona vijana wanufaike na maendeleo hayo ya Sayansi na teknolojia aan kiufupi vijana wanahitaji sana kutiwa moyo
 
Tena, kwenye suala la vijana wanaofanya vumbuzi mbalimbali ndio la kutilia mkazo, kuna yule kijana aliyekuwa na Redio yake kule Kigoma asiishie tu pale serikali impeleke mbali zaidi maana ana kipaji kikubwa sana. Hongera kijana kwa kufungua fikra zetu.
Yaaap inasemekana yupo chuo kwa ajili ya kuongeza kwanza ujuzi then after atafika mbali akisimamiwa vema.
 
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71
 
Pamojaa sanaaa mkuuu! Usisahau kugusa kidude kilichoandikwa vote ^
 
Gud idea,Vita ni kubwa sana,viongozi wengi wanaogopa mapinduz ya technologia ,kuna vumbuzi nyingi sana ila Cha ajabu viongozi wameshindwa kuzipitisha kutokana na hofu kwamba zita wanyima upigaji na rushwa.
 
Gud idea,Vita ni kubwa sana,viongozi wengi wanaogopa mapinduz ya technologia ,kuna vumbuzi nyingi sana ila Cha ajabu viongozi wameshindwa kuzipitisha kutokana na hofu kwamba zita wanyima upigaji na rushwa.
Yeah ni kweli kabisa mkuu! Ni lazima tukubali tu hali halisi iliyopo. Mapinduzi ya sayansi na teknolojia ndio msingi wa kila kitu kwa sasa
 
Kumbe hata sisi tunaweza, hao vijana waliotengeneza mkanda salama niliwaona kwenye Tv wakiwa na waziri wa Afya ningependa unifafanulie huo mkanda salama mkuu...........ila kongole sana kwa idea nzuri
 
Nikitazama hiyo picha ya madaktari hakika tumetoka mbali sana kweli ipo haja kubwa ya kuinua teknolojia yetu.
 
Samahani nikiangalia hapo picha uliyorejea kwa kusema ni picha yako! Ningependa kufahamu wasifu wako. Pia ningependa unifafanulie kidg kuhusu hizo picha mbili
 
Kumbe hata sisi tunaweza, hao vijana waliotengeneza mkanda salama niliwaona kwenye Tv wakiwa na waziri wa Afya ningependa unifafanulie huo mkanda salama mkuu...........ila kongole sana kwa idea nzuri
Asante mkuu! Kwa kuifuatilia kiundani chapisho langu,
Mkanda salama ni vumbuzi iliyofanywa na wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ukiwa na lengo thabiti la kupambana na vifo vitokanavyo na akina mama hususani wakati wa kujifungua........Mkanda huu huvalishwa kwa akina mama hao baada tu ya kujifungua hivyo husaidia katika kufanya masaji ya mfuko wa uzazi. Kizuri zaidi ni kuwa mpaka sasa walijaribu kutumia katika baadhi ya hospitali na ukeleta matokeo chanya!

Nina imani kuwa nimejaribu kukujibu Kiongozi, usisahau kugusa kidude kilichoandikwa vote^
 
Back
Top Bottom