CCM wanajua kama Chadema itaendelea kuongozwa na Mbowe haina madhara kwao na hata kama yatakuwepo ni madogo sana.
Wanajua Mbowe si mzuri kwenye mikakati ndio maana hawataki kumfanyia figisu za kisiasa ili wamwondoe. Sababu ni mmoja tu, Hawajui ukimwondoa Mbowe pale Chadema nani atakaye kuja kumrithi?
Wanajua wanaweza wakamwondoa Mbowe akaja mtu kwenye uwezo na tishio kwao kama alivyokua Dr Slaa. Ila kwa akili za Mbowe na baadhi ya wanachadema wanaamini Mbowe yupo pale kwakua ana nguvu za kisiasa na hilo sikweli.
CCM wameona bora washindane na Mbowe na Mashinji kuliko ile Chadema ya Dr Slaa, Mnyika, Zito kabwe, marehemu Chacha wangwe ile Chadema ilikua hatari zaidi kwa CCM kuliko hii ya Mbowe, Mashinji, Msigwa na Lema.
Kwa aina ya watu waliopo Chadema kwa sasa ninafuu sana kwa CCM kuliko kipindi cha nyuma. Ndio maana unakuta wakina Makamba, Mwigulu, Kinana na wengine Nyota wa CCM katika siasa wametulia na mudamwingine watu wanawaulizia humu jukwaani.
Ni kwasababu ndugu Polepole anaimudu bila shaka Chadema ya sasa.
Angalia NCCR na CUF za kipindi kile zilivyokua hatari kwa CCM, Uhatari wa ivyo vyama kwa CCM Ndio umepelekea visambaratishwe ki mkakati.
Kwa nionavyo Mbowe kwakua hana Sumu katika siasa za Sasa basi CCM wataendelea kufurahia uwepowake mbaka pale Chadema watakapo stuka.