Ni wakati wa Watanzania Bara kuanza kuteuliwa Zanzibar

Hivi ni lini Zanzibar itajitangazia uhuru wake kamili na kujitegemea kwa 100%?

Mimi naona kama huu Muungano unawapendelea zaidi kuliko sisi! Haiwezekani tuna nchi ya Tanzania na Zanzibar, huku Tanganyika ikiwa haijulikani ilipo!
Mbona hueleweki na unajichanganya mkuu. Kwa mujibu wa post yako hii, Zanzibar inatawaliwa, sasa nchi inayotawaliwa inawezaje kujipendelea?
 
Naunga mkono hoja tena na huu muungano uvunjwe haraka
Ndjo hili lilifanya mchakato wa katiba uvunjike. Serikali 3 vs serikali 2, nashauri serikali itafute na ifuate ushauri wa chadema.
Ushauri wa chadema ungeondoa kabisa hizi drama za chief hangaya
 
Kwanini iwe hivyo ..tunaepusha kitu gani na kwa faida IPI?
Nisome vizuri, ili kulinda maslahi ya eneo kubwa la nchi (Tanganyika), ulishawahi kusikia kiongozi wa dola la kichina akatokea hongkong.....hongkong ni semi-autonomous na ina kiongozi wake mkuu ambaye anawekwa pale na china........
 
Tatizo limeanzia kwa viongozi wetu.
Tanganyika ina viongozi wezi na mafisadi yasiyojali chochote.
Ni waigizaji tu kwa wananchi.
Zanzibar ina watu million 1 inaweza kutoa Rais wa Tanzania, huku Tanganyika ina wananchi million 57 haina uwezo hata wa kumweka mwenyekiti wa mtaa huko Zanzibar.
Watanganyika ni wapumbavu
Samahani kwa lugha niliyoitumia.
 
Nisome vizuri, ili kulinda maslahi ya eneo kubwa la nchi (Tanganyika), ulishawahi kusikia kiongozi wa dola la kichina akatokea hongkong.....hongkong ni semi-autonomous na ina kiongozi wake mkuu ambaye anawekwa pale na china........
OK sawa lakini hebu tutazame mpaka sasa tangu mzanzibar amekuwa rais hapa Tanzania je sisi Tanganyika( eneo kubwa) tumepoteza maslahi gani ambayo yapelekee kuona ipo haja ya kuweka utaratibu wakuzuia wazanzibar kutawala Tanzania.
 
Mkuu si kulaumu kwa kuwa hujui asili ya muungano wetu na nani alipendekeza na kwanini hayo mapendekezo ya mtindo huo yakubaliwe...! Ukitafuta utajua mkuu pengine ukaelewa busara za mzee wetu Nyerere wakati huo.
 
Kwa muktadha huo kwa nini china wasiruhusu mtu wa kutoka hongkong, Taiwan au Singapore kuongoza dola la kichina kwa kuwa ni wachina walewale, tumia japo akili kidogo basi.....
 
Sawa
 
Mkuu kuhusu wizi na ufisadi hata Zanzibar upo sana, si uliona raisi Mwinyi alivyotumbua waliofisadi zile pesa. Shida wapo wachache na budget zao ndogo hivyo kuwa issue kubwa kwenye media inakuwa ngumu.
 
Chetu chao chao chao kuku hao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa muktadha huo kwa nini china wasiruhusu mtu wa kutoka hongkong, Taiwan au Singapore kuongoza dola la kichina kwa kuwa ni wachina walewale, tumia japo akili kidogo basi.....
Yaani ipo hivi sababu za jamhuri ya watu wa China kuungana si sawa na zetu, pili tamaduni, na tabia za wachina na sisi ni tofauti hivyo sisi hatutakiwi kufanya maamuzi eti kwa sababu tu wachina wamefanya maamuzi kama hayo. Sisi lazima tupate sababu za kwetu wenyewe na si kuiga mahali Fulani ...sisemi kwamba napinga hoja yako ...hapana bali nahitaji hoja makini zitazobainisha uhitaji wa kuzuia wazanzibar wasiongoze Tanzania.
 
Kule watu wa bara wanaofanya kazi ni Polisi na Jeshi tu
 
Mkuu si kulaumu kwa kuwa hujui asili ya muungano wetu na nani alipendekeza na kwanini hayo mapendekezo ya mtindo huo yakubaliwe...! Ukitafuta utajua mkuu pengine ukaelewa busara za mzee wetu Nyerere wakati huo.
Tatizo ni wa Tanganyika kuuonea aibu asili yao. Huu muungano ni sawa na mwanaume kumpenda mwanamke asiyekupenda . Utafanya mambo mengi ya kujikomba kwenye mahusiano yenu. Tanganyika imejitolea kwa hali na mali kuulinda muungano tofauti na Zanzibar .

Kikubwa kuna siku isiyo na jina . Utavunjika
 
Hata ajira za kawaida tu za serikali kama uwalimu, uhandisi, unesi, haupati Kama sio Mzanzibar, lakini huku Bara wamejazana kibao.
Bara ndio wapi wewe! Sema huku Tanganyika. Wazanzibari wanajielewa sio nyinyi hata jina la nchi yenu hamlijui.
 
Hizi comments humu mtandaoni za wazanzibari kuanza kupendelewa dhidi ya wabara bado hujazisoma? wee jamaa bhanaa.......endelea kuamini tu unavyoamini.
 
Hizi comments humu mtandaoni za wazanzibari kuanza kupendelewa dhidi ya wabara bado hujazisoma? wee jamaa bhanaa.......endelea kuamini tu unavyoamini.
Hayo mambo ya watu kulalamikia kiongozi kupendelea watu fulani yalisemwa hata wakati wa JPM kupendelea wasukuma..lkn mbona hatukutaka kuzuia rais asitoke chato(usukumani) tena??? Tusiamue mambo kwa mihemko mkuu.
 
Mzanaki kwa uoga wake alifosi ka-nchi kadogo kuwa sehemu ya nchi kubwa na lakini kajiongoze kenyewe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzanaki kwa uoga wake alifosi ka-nchi kadogo kuwa sehemu ya nchi kubwa na lakini kajiongoze kanywe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Alisababisha usumbufu ambao hauna maana wakati alikuwa na upper hand kwenye jambo lenyewe....
 
Kwa hili tumkumbuke Rev. Mtikila. Pamoja na upendeleo wanaoupata, kila siku wanajiliza liza tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…