Ni wakati wa Watanzania Bara kuanza kuteuliwa Zanzibar

Ni wakati wa Watanzania Bara kuanza kuteuliwa Zanzibar

Ndio. Hawa waZanzibar waishie kutawala huko huko kwao na sio pande lote hili la huku Bara. Umakamu unawatosha.
Hata umakamu ni upendeleo mkubwa sana, wao wapewe uwezo tu wa kuchagua rais wao ambaye anakuwa mjumbe wa baraza la mawaziri la Tanzania.....na wapewe nafasi kwenye maswala ya kimuungano kama wizara ya mambo ya nje, kwenye maeneo yasiyo ya muungano kama wakiomba nafasi waombe kama wengine siyo kwa upendeleo maalumu au kuona kwamba ni haki yao.....na hivyo hivyo watoe nafasi kwa watu wa bara kuomba huko kwao ili kuleta muingiliano wa watu. Kukishakuwa na muingiliano wa watu nchi itabaki kuwa moja tu, Tanzania...​
 
Haiingii akilini keki ya Zanzibar ni kwajili ya wazanzibari pekee ila keki ya huku bara Wazanzibari nao wana hila, yani chao ni chao peke yao ila chetu ni chao.

Yani huko Zanzibar uongozi kuanzia uraisi, mahakamu wa rais, wakurugenzi wa mashirika, teuzi, n.k ni wao tu ila ukija huku si ajabu kumkuta mzanzibar ni wazirri, mkurugenzi au mkuu wa shirika flani, n.k

Hata kwenye ajira za kawaida hizi za udaktari, uhandisi, uhasibu, ualimu, n.k huko kwao hizi ajira ni kwajili yao ila ukija huku wapo kibao kwene idara tofauti.

Sijui ni nini hiki.

Mwalimu nae alikuwa ni mtu tu kama wengine na sio kila kitu alichofanya kiwe kama msaafu, kiukweli kuna vitu ni lazima vibadilike.
Nimefurahi kuona kuwa baada ya miaka zaidi ya 40 kuna baadhi ya watanganyika wameanza kuamka juu ya huu muungano. Suali lako ni rahisi kulijibu, wewe huwezi kuwa kiongozi katika serikali ya mapinduzi kwa sababu wewe si mzanzibari, ila mzanzibari anaweza kuwa katika serikali ya Tanzania kwa sababu yeye pia ni mtanzania. Sasa wewe unataka uwe kiongozi katika serikali ambayo hata hujashiriki katika kura za kuichagua, inaingia akilini wewe? Unataka uwe kiongozi katika nchi ambayo wewe si mwananchi? Wazanzibari ni wananchi wa Tanzania na ndio maana wanapewa uongozi Tanzania. Wazanzibari tulipiga kelele zamani tukitaka serikali tatu lakini mkawa mnatucheka, sasa naona mnaamka. Mkitaka serikali ambayo haitokuwa na wazanzibari basi mukubali kuwa na serikali ya tanganyika, serikali ambayo itakuwa inashuhulikia masuali ya tanganyika, ikiongozwa na watanganyika na rais wa kitanganyika. Halafu kuwepo na serikali ya Tanzania ikishuhulikia masuali ya Tanzania ikiongozwa na watanzania i.e wazanzibari na watanganyika.
 
Tanganyika ni shamba la Bibi, halina mwenyewe.

Watavuna sana tu!
Mgao wa Covid-19 umenichanganya sana, halafu ndugai anasema tuangalie population sio majimbo, Zanzibar labda wangepewa $20m, sio$100m, kwa kweli hapa hamna haki, kwa wingi wa watu na uchangiaji wa kodi, naamini mchango wa kodi hauzidi 10% kwenye mfuko mkuu!
 
Kama muungano wa Tanzania umeanza kuwa na ubinafsi..itakuwa ikitokea wa kikanda au afrika kwa ujmla..

Ngozi nyeusi zina ubinafsi sana haijalishi anaelimu hana, mshika dini au hana dini, anacheo au hana, ni mtawala au mtawaliwa...wabinafsi kuanzia mali za urithi nyumbani hadi urithi wa Taifa..

Mchawi wa mwafrika ni mwafrika mwenyewe!
Ngojqa niishie hapo, maana ngozi nyeusi tuna laana ya asili. turudi kwa muumba atusamehe😂😂😂
 
Tusilaumu Wazanzibari kwa ujinga uliofanywa na viongozi wetu wakati wa kuungana maana Zanzibar ilibaki na mamlaka ya nchi yao kwa baadhi ya mambo lakini Tanganyika tukajifanya wajanja tukajigeuza serikali yetu ndio ya muungano sasa matokeo yake Wazanzibari wanaingia kwenye serikali yetu kwa mgongo wa muungano maana ndani ya hiyo serikali ya muungano hakuna mipaka kipi kinatakiwa kiwahusu Watanganyika tu na kipi kinaweza kuchukuliwa na mtu toka upande wowote tofauti na wenzetu.
 
Haiingii akilini keki ya Zanzibar ni kwajili ya wazanzibari pekee ila keki ya huku bara Wazanzibari nao wana hila, yani chao ni chao peke yao ila chetu ni chao.

Yani huko Zanzibar uongozi kuanzia uraisi, mahakamu wa rais, wakurugenzi wa mashirika, teuzi, n.k ni wao tu ila ukija huku si ajabu kumkuta mzanzibar ni wazirri, mkurugenzi au mkuu wa shirika flani, n.k

Hata kwenye ajira za kawaida hizi za udaktari, uhandisi, uhasibu, ualimu, n.k huko kwao hizi ajira ni kwajili yao ila ukija huku wapo kibao kwene idara tofauti.

Sijui ni nini hiki.

Mwalimu nae alikuwa ni mtu tu kama wengine na sio kila kitu alichofanya kiwe kama msaafu, kiukweli kuna vitu ni lazima vibadilike.
Watu wachache sana hata wangeajiriwa wote huku bara mimi sioni kama kuna tatizo lolote wanaosema zanzibar ni nchi ndiyo wanaotuharibia wangesema ni sehemu ya Tanzania tuu kama ilivyo rukwa au mafia
 
Mgao wa Covid-19 umenichanganya sana, halafu ndugai anasema tuangalie population sio majimbo, Zanzibar labda wangepewa $20m, sio$100m, kwa kweli hapa hamna haki, kwa wingi wa watu na uchangiaji wa kodi, naamini mchango wa kodi hauzidi 10% kwenye mfuko mkuu!
Yaani population yoote ya zenji ni sawa na ya wilaya moja tu ya Temeke baasi
 
MIMI NASHAURI IITISHWE KURA YA MAONI KUHUSU MUUNGANO.Sisi wananchi wa Tanganyika na Zanzibar tuamue Aina ya muungano tunaoutaka.Kura hizo za Maoni zipigwe kwa Uhuru na kwa HAKI.Na matokeo ya Hiyo kura yaheshimiwe.Sisi wananchi tuamue Ni jinsi gani tunataka kutawaliwa.
 
Tusilaumu Wazanzibari kwa ujinga uliofanywa na viongozi wetu wakati wa kuungana maana Zanzibar ilibaki na mamlaka ya nchi yao kwa baadhi ya mambo lakini Tanganyika tukajifanya wajanja tukajigeuza serikali yetu ndio ya muungano sasa matokeo yake Wazanzibari wanaingia kwenye serikali yetu kwa mgongo wa muungano maana ndani ya hiyo serikali ya muungano hakuna mipaka kipi kinatakiwa kiwahusu Watanganyika tu na kipi kinaweza kuchukuliwa na mtu toka upande wowote tofauti na wenzetu.
Hili ni funzo kwa wahafidhina wa ccm na muungano wao
 
Back
Top Bottom