Mnachanganya na kushindwa kutofautisha Kati ya "Serikali", "Taifa", "nchi" na "dola"(state)
Mwaka 1964 kilichounganishwa ni siyo nchi, Serikali wala Taifa, bali ziliungana dola mbili, Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania.
Kimsingi, raia ni wa "dola" ndiyo yenye raia na siyo Taifa, wala Serikali (japo kwa kiswahili, tunatamka "nchi" kimaanisha "dola").
Kisheria, dola ziitwazo Tanganyika na Zanzibar zilifikia kikomo za kuzikwa mwaka 1964,kwa hiyo hazipo tena.
Hakuna ubishi kwamba Tanganyika haupo. Je, dola ya Zanzibar ipo? Ili kitu kiitwe dola kinakuwaje?
Ni, dola huundwa na 1.Serikali, 2.Mipaka, 3. Watu na 4. Uhuru (Uhuru wa ndani na nje).
Zanzibar, ina Serikali, mipaka na watu, ila inakosa kipengele kimoja tu cha uhuru ili iwe dola kamili.
Kwa hiyo dola ya Zanzibar haipo, na kwa kuwa haipo,basi hakuna raia wa Zanzibar, bali tuna raia wa Tanzania wenye asili ya Zanzibar, na moja wapo ni Rais Samia, S.H.
Zanzibar haina uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake kitaifa na kimataifa. Hiki kigezo kingekuwepo, basi Zanzibar ingekuwa dola kamili, na Wazanzibar wangekuwa raia wa kigeni.