Rafiki ukiona mimi ninajibu swali gani utagundua kuwa jibu langu linasahihisha kuwa Mangula siyo Mkinga ni Mbena! Maneno yote hayo ya nini!?
Sio kila mtu anayeitwa Sanga ni mkinga
Sio kila mtu anayeitwa Abdallah ni muislam
Sio kila mtu anayeitwa John ni mkristo
Sio kila mtu anayeitwa Nyoni, Ngonyani, Mapunda au Nyati ni mngoni au ana uhusiano na Songea Ruvuma
Mangula anaishi Njombe, Ninakubali
Kuthibitisha Mangula ni mbena au Mpangwa ni kazi ngumu sana
Mimi nimeishi huko kaskazini, Watu wanajua mimi ni wa huko. Hata nikikutana na watu kwenye channel za Deal wanajua mimi wa huko, Ni ngumu sana Kuthibitisha kabila la mtu au mahusiano ya dini na jina lake mpaka mtu mwenyewe athibitishe
Mfano:Zakaria kakobe tunamfaham vizuri sana kama mchungaji na mtanzania, Aliombwa athibitishe Uraia wake kama yeye ni mtanzania kwa kuonyesha makaburi ya Babu mzaaa Babu aliyezaa Babu wa mzaa Babu. Kakobe alishindwa
Mfano:Jeneral Ulimwengu amewahi kuwa Mkuu wa wilaya Tanzania, Wakati wa Mkapa Aliombwa athibitishe Uraia wake na kabila akashindwa
Hivyo usimsemee Mangula kuwa ni Mbena ingawa nakubali Manguli anaishi Njombe
Achana na mambo ambayo huna Hakika
Achana na mambo ya kusikia, Ishi maisha yako ya kweli