Ni wakinga wachache tupo kwenye mambo ya Siasa, Siasa ni kazi ya ziada kwa wakinga

Ahsante kwa ufafanuzi huu, una dada single ila asiwe na mtoto uniunganishie?
 
Ni kweli lakini Kumbuka sisi wakinga huwa tunaoana sisi kwa sisi

Mwanamke wa Kikinga ni tofauti sana ukimuoa, Wanakomaa na Biashara sana,

Anafahamu malengo yenu, Na hakuna utani kwenye ishu za pesa
Na ufugaji mandondocha vipi, wanakomaa kuwalisha ili biashara iendelee ikiwa wewe mumewe mfugaji umekufa?
 
Na ufugaji mandondocha vipi, wanakomaa kuwalisha ili biashara iendelee ikiwa wewe mumewe mfugaji umekufa?
Nimecheka sana
Hizi story za Ndondocha kila mkoa nazisikia. Kila kabila hapa Tanzania kuna story mara vibwengu

Ukiishi Arusha utasikia wachaga wana ndondocha

Ukiishi Mbeya hivyo hivyo utasikia yule Bibi wa kinyakyusa ana Ndondocha

Nyumba kukiwa na mtu mwenye tatizo la akili utasikia amefanya Msukule, Haya mambo ni kila sehemu

Elimu inahitajika sana kwa watanzania kuhusu magonjwa ya Akili, Kila mgonjwa wa akili kwenye nyumba anaitwa Ndondocha au amefanywa msukule
 
Lakini kwa Wapemba, Wakinga, Wapare, Wachagga ni jambo la kawaida sana kwao kufuga aliens (ndondocha), sijawahi amini hawa watu hata siku moja.
 
Rafiki ukiona mimi ninajibu swali gani utagundua kuwa jibu langu linasahihisha kuwa Mangula siyo Mkinga ni Mbena! Maneno yote hayo ya nini!?
 
Rafiki ukiona mimi ninajibu swali gani utagundua kuwa jibu langu linasahihisha kuwa Mangula siyo Mkinga ni Mbena! Maneno yote hayo ya nini!?
Sio kila mtu anayeitwa Sanga ni mkinga

Sio kila mtu anayeitwa Abdallah ni muislam

Sio kila mtu anayeitwa John ni mkristo

Sio kila mtu anayeitwa Nyoni, Ngonyani, Mapunda au Nyati ni mngoni au ana uhusiano na Songea Ruvuma

Mangula anaishi Njombe, Ninakubali
Kuthibitisha Mangula ni mbena au Mpangwa ni kazi ngumu sana

Mimi nimeishi huko kaskazini, Watu wanajua mimi ni wa huko. Hata nikikutana na watu kwenye channel za Deal wanajua mimi wa huko, Ni ngumu sana Kuthibitisha kabila la mtu au mahusiano ya dini na jina lake mpaka mtu mwenyewe athibitishe

Mfano:Zakaria kakobe tunamfaham vizuri sana kama mchungaji na mtanzania, Aliombwa athibitishe Uraia wake kama yeye ni mtanzania kwa kuonyesha makaburi ya Babu mzaaa Babu aliyezaa Babu wa mzaa Babu. Kakobe alishindwa

Mfano:Jeneral Ulimwengu amewahi kuwa Mkuu wa wilaya Tanzania, Wakati wa Mkapa Aliombwa athibitishe Uraia wake na kabila akashindwa

Hivyo usimsemee Mangula kuwa ni Mbena ingawa nakubali Manguli anaishi Njombe

Achana na mambo ambayo huna Hakika

Achana na mambo ya kusikia, Ishi maisha yako ya kweli
 
Kwa akili hii, hata Mangula mwenyewe angekataa kuwa siyo Mkinga ungebisha!!
 
Sasa huo si ni ujinga?
 
Alichoeleza mtoa somo leo kuhusu Wakinga ni kweli kabisa. Yaani jamaa wanajituma ni balaa. Utakuta Mkinga ni Mkurugenzi wa Shirika fulani lakini bado ana biashara za mbao, viazi na maduka. Halafu kwa miaka ya kuanzia 90 Wakinga wamesomesha sana watoto wao ili waje wasimamie biashara zao. Binafsi nina rafiki zangu ambao walipeleka watoto wao kusoma Nairobi - Kenya, Afrika ya Kusini na hata Uingereza, leo ndio wasimamizi wa biashara za wazazi wao. Hiki ndio chanzo cha Kariakoo kutekwa na Wakinga.
 
Widambe alikuwa ni Mbena sio Mkinga!
 
Yale maghorofa Kariakoo ni ya wakinga

Onyesha ya kwenu
Usipanic mkuu Mimi sijazungumza kuhusu kabila,nisome vizuri hakuna sehemu ata moja nimetaja kabila, Mimi napinga na kuunga hoja Tu!!

Uhalisia usipojidhihirisha kwenye Jambo lolote ujue kuna lililofichwa ndani yake
 
Kutaka kumantain mtaji wa ml.100 kwa kuuza kahawa na kashata,Kula kwa mama ntilie ni kanuni ambayo haina uhalisia kwangu, ninukuu "kwangu" sijakulazimisha huo ndio MSIMAMO wangu.
 
@Kinuju , Super Sub Steve huo ndio uhalisia watu tunataka tujifunze ili tuwe matajiri. Sio kunambia mtu anaingia mjini na ml.100 anausoma mji kwa kuuza kahawa na kashata, kula kwa mama ntilie ndio aweze kumantain kuja kuwa tajiri ,

brazaz iyo ni risk unaweza poteza pesa yako kwa kujiuguza ,afya hulindwa na pesa kwa Kula vizuri,kulala pazuri, kuvaa nadhifu.

Kama utatafuta pesa adi kupata mtaji wa ml.100 alafu uje Dar ufanye biashara ya kahawa na kashata, ule mama ntilie,ulale chumba cha elfu 40 jangwani kumantain mtaji wako usipungue, Mimi siwakatalii kila mtu na mtazamo wake.( Narudia tena kwa mtazamo wangu mtu huyo ni mlozi ao akili haipo Sawa)

Uhalisia ni kama ameacha shamba lake la miti kaja mjini na kauza kahawa miaka mitatu ,mti umekomaa kauza kapata ml. 100 obviously atabadili biashara.
 
Thubutu!

Wachagga wengi wanafuga mandondocha majumbani mwao!
Mimi ni shuhuda wa tukio la ROMBO/ Leto kuna mfanyabiashara ambaye tulizika mdogo wake baada ya miezi miwili marehemu akatolewa dukani kwa Kaka yake.

Kaburi lilifukuliwa wakafanya matambiko ya kuchinja kondoo kaburini .

Jamaa Catholic wamemtenga, kanisa katoliki Leto.

Na zaidi ya yote ni eneo lenye mazezeta wakutosha ,watu wapo mijini wanachuma mali Tu.
 
Hakuna uhalisia iyo mali ina makando mengi,

Aseme aliacha shamba la miti wakati anasubiri ikomae akaja mjini kuuza kahawa,akavuna na kwa kuwa kapata mtaji na watu anaoshinda nao mazingira yake ya kahawa na kashata ni wafanyabiashara basi wakamsaidia mawazo kulingana na mtaji wake iyo haina makandokando inaeleweka.

Hesabu rahisi tu kwa wastani duka frame+bidhaa =Ml.100

Kahawa ameuza miaka mitano
Siku165 × miaka5= siku 1,825

Sh.100,000,000 ÷ siku1,825= Sh. 54,794.5

Ni muujiza yaani auze kahawa na kashatakwa siku atunze Sh.54,794.5 kwa muda wa miaka mitano ndio atafungua frame moja.

Swali: je biashara ya kahawa inaweza kumpa mtu akiba ya 54,000 kwa siku?
 
No, kahawa na kashata inakupa change ya shillingi 3,000 mpaka 10,000 kwa siku na inategemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…