Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Kibugumo ipo mji mwema au iko wapi? Maana hata Dege hufiki.Ahaa kumbe Kibugumo. Hapo Sawa.
Habari Wana JF,
Natafuta Kiwanja Dar es salaam Cha bei poa Chini ya Mil 4
Vigezo;
- Eneo liwe lina upatikanaji wa maji na umeme
- Pasiwe mbali sana na Mji(Ndani ya dar es salaam)
- Eneo la kutosha vyuma ya vyumba 3 na choo 2.
Maeneo yapo mengi Sana.Huwezi kupata eneo ndani ya dar es salaam kwa hela hio mzee! Maeneo yapo Mkuranga kwa hio pesa unapata eneo kubwa tu la kutosha.
Uko sahihi,Kuna watu wako Magomeni,mwenge,Sinza na Kariakoo wanafikiri ndo mwisho wa Dar .Kuwa na subra hata kimara huko ndani unapata. Hii mentality ya kwamba Dar ni expensive kote sio sawa.
Kisemvule siyo DarKuna maeneo ya Kisemvule nayafahamu unapata kiwanja tena kikubwa tu kizuri hakipo bondeni na kimepimwa. Pi pameendelea maji umeme na daladala zipo.
Ila ndani ya Dar es Salaam mmmmmh ni ngumu sana.
Naishi Dar ila kwa maeneo nayoishi mm bila Mil 15 na kuendelea wala usifikirie kuhusu kiwanja
Karibu
Iko Kibamba,ukifika Kibamba shule ukitokea Mbezi unaingia kulia .Kuna kibwegere ,kibweheri na hondogo.Nadhani iko mbezi mwisho kama unaenda kibamba upande wa kushoto
Nitafute nikupe kiwanja madale kwa 7.8 unilipe kwa awamu
Kigamboni mji mwema patakufaa zaidi, 20 kwa 20 unapata na ni karibu na mjini bora adha ya kuvuka pantoni kuliko kwenda kujenga Chanika utajuta.
Ukishamalizana na matapeli wote ukiwa upo tayari kununuwa kiwanja nicheck nitakukabidhi kwa mwenyekiti wa mtaa unamaliza shida yako.
Hakuna mjanja yoyote anayekaa mbali na city center, viwanja vipo tatizo wabongo ujuwaji mwingi.
Mkuu mbona huku ndio kwenyewe kwanini unauza?Njoo nikupe changu kipo Kiluvya maeneo ya kwa Sumaye Kule kipo 35*35
Nina ujenzi pahali nahitaji hela kumalizia, nina viwanja kama 5 hv vyote vimepimwa tayari naviuzaMkuu mbona huku ndio kwenyewe kwanini unauza?
Misumi vyote hivo viko sokoniMadale ipi boss
Misumi vyote hivo viko sokoniView attachment 1959249
Am not sure lakini ni upande wakulia ukitokea wazoMisumi ni kama unaingilia madale maskauti ama wapi?
Sio mto shekh ni channel kidogo tu ya maji hauna athari yoyoteUwo mto unaokatiza hapo hauna athari pindi mvua zikinyeesha?
Au aende mbele ya Kigamboni kunaitwa Buyuni na vimepimwa. Kwa bei hiyo atapata kizuri tu..Huwezi kupata eneo ndani ya Dar es salaam kwa hela hio mzee! Maeneo yapo Mkuranga kwa hio pesa unapata eneo kubwa tu la kutosha. Hio ni Kilwa road!
Upande wa Bagamoyo road pia yapo maeneo Vikawe ni mbele kidogo ya bunju unapata eneo freshi kubwa tu 20*20 au zaidi!
Morogoro road ni kuanzia mbele ya kibaha hapo. Kama upo tayari tunaweka wese tunaenda kamata eneo chap!
Kwa hiyo bei, unachokitafuta utakipata. Usirudi humu kutililia.......Habari Wana JF,
Natafuta Kiwanja Dar es salaam Cha bei poa Chini ya Mil 4
Vigezo;
- Eneo liwe lina upatikanaji wa maji na umeme
- Pasiwe mbali sana na Mji(Ndani ya dar es salaam)
- Eneo la kutosha vyuma ya vyumba 3 na choo 2.