Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hadi wewe mkuu bado unaamini katika diplomacy kwenye kudili na michezo michafu ya sisiem katika nchi hii? Utakuwa kati ya watu wenye maslahi binafsi na Mbowe, na inastaajabisha.
simjui Mbowe, ila matendo ya Lisu yamenitoa imani kwake. He was one of my favorite politician. Kumbe ni mropokaji...... juzi kasema hawezi kugombea uenyekti na Mbowe, leo anagombea...utamwamini mtu kama huyo?
 
Attachments

  • SINA MPANGO WA KUGOMBEA UENYEKITI LISU.mp4
    7.1 MB
Maneno aliyozungumza Lissu leo wakati anarudisha fomu ni mazito sana, anasema mtu aliyemleta Abdul kwake ampe pesa na akamwambia hata wengine wameshapewa pesa ndiye anagombea kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na anamuunga mkono Mbowe kuwa mwenyekiti!

Katika hili jambo kama ni kweli ni baya sana kwa CHADEMA kwa maana chama kinapoteza imani mbele ya umma. Kwa upande mwingine kama Lissu ni muongo basi hawezi kuaminiwa kuwa kiongozi tena na wenzake ndani ya CHADEMA maana ni dhahiri atakuwa ana nia mbaya sana dhidi ya chama na hii inamaanisha safari yake ya kugombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2025 inaweza kuwa imefika mwisho.

Pia amekejeli mtindo wa mwenyekiti Mbowe ambao huwa anaombwa na wapambe kila uchaguzi kugombea.

Lissu asipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA atajaribu kuanzisha chama kingine, ataelekea ACT au ataachana na siasa kabisa.

Mwamba ni kama sikio la kufa.

Ushauri wa bure, Lissu aongezewe ulinzi.

Cc: imhotep, JokaKuu, binti kiziwi
 
nani kamshawishi? Mbowe? True Wenje hafai kwa nafasi hiyo........
Lissu hakua direct ni nani kamshawishi wenje. Ila alisema tu kwa jumla kuwa wenje alishawishiwa kugombea umakamu

Unasema hafai wakati anagombea peke yake na ana baraka za mwenyekiti. Inategemea nini? Kujivua na kilichotokea ilipaswa wenje azuiliwe kugombqa ili kukisafisha chama
 
simjui Mbowe, ila matendo ya Lisu yamenitoa imani kwake. He was one of my favorite politician. Kumbe ni mropokaji...... juzi kasema hawezi kugombea uenyekti na Mbowe, leo anagombea...utamwamini mtu kama huyo?
Vitu vidogo sana kwenye siasa hivi, huyo Mbowe unayemuamini hajawahi kugeuka?

Nimekufahamu humu siku nyingi, sikuwahi kufikiri upo weak kiasi hicho
 
Lissu asipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA atajaribu kuanzisha chama kingine, ataelekea ACT au ataachana na siasa kabisa.
Una maana CHADEMA itakayo kuwa inaongozwa na nani, Mbowe? Hapo bado kutakuwepo na CHADEMA kweli?

Sioni sababu ya Lissu kuanzisha chama, au kujiunga na chama kingine chochote. Hii CHADEMA itakayo salia bila ya Mbowe, hicho ndicho chama pekee atakacho kuwemo Lissu; hata kama kitakuwa kinaongozwa na mtu mwingine, mbali ya Mbowe.
 
Ni Lisu kuacha kugombea...Mbowe ana diplomacy, siyo kama lisu anayeropoka
Kweli kipendacho roho ni dawa!.
Mkuu 'Ritired' hii' loyalty' isiyo tikiswa na jambo lolote lile, hii ni ya kitofauti sana.

Mbowe is compromised. Mbowe alikengeuka muda kitambo sana; na alama zote zipo wazi kabisa, lakini 'loyalty' uliyo mwekea naona ni kubwa kiasi kwamba hakuna kinacho weza kuitikisa.

Lililo bora sasa hivi, ni kuiachia hiyo inayo itwa demokrasia ifanye kazi. Acha watu wafanye maamuzi ya haki na huru kati ya hawa watu wawili, "mropokaji" (Lissu), na huyo ambaye umemwekea kinga ya kutotikiswa na uovu wowote.

Sioni njia nyingine yoyote zaidi ya hiyo ya watu kuamua wenyewe

Lissu "aache kugombea"? That is asking too much..
 
Mbowe hatagombea na ni dhahiri walikubaliana na Lissu ppasipo kushirikisha watu fulani, sasa vijana wa Mbowe kwa kuwa hawakutaraji wala kulijua hilo wakataharuki na kuungana na CCM kuanza kumchafua na kumdharirisha Lissu.

Ngoja jumamosi atoe tamko.

Hapo ndiyo utajua maana ya luba kuitwa king'ang'anizi!
 
simjui Mbowe, ila matendo ya Lisu yamenitoa imani kwake. He was one of my favorite politician. Kumbe ni mropokaji...... juzi kasema hawezi kugombea uenyekti na Mbowe, leo anagombea...utamwamini mtu kama huyo?
Mazingira yanabadilika, hata Mbowe alisema angestaafu endapo CHADEMA ingefanya vibaya 2020.
 
Maneno aliyozungumza Lissu leo wakati anarudisha fomu ni mazito sana, anasema mtu aliyemleta Abdul kwake ampe pesa na akamwambia hata wengine wameshapewa pesa ndiye anagombea kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na anamuunga mkono Mbowe kuwa mwenyekiti!

Katika hili jambo kama ni kweli ni baya sana kwa CHADEMA kwa maana chama kinapoteza imani mbele ya umma. Kwa upande mwingine kama Lissu ni muongo basi hawezi kuaminiwa kuwa kiongozi tena na wenzake ndani ya CHADEMA maana ni dhahiri atakuwa ana nia mbaya sana dhidi ya chama na hii inamaanisha safari yake ya kugombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2025 inaweza kuwa imefika mwisho.

Pia amekejeli mtindo wa mwenyekiti Mbowe ambao huwa anaombwa na wapambe kila uchaguzi kugombea.

Lissu asipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA atajaribu kuanzisha chama kingine, ataelekea ACT au ataachana na siasa kabisa.
Hapana, Lissu na Mbowe wanajua wanachofanya, sio serious kama unavyofikiria.

Mbowe ataendelea na u mwenyekiti, na Lissu atagombea uraisi kupitia CHADEMA.
 
Back
Top Bottom