Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Pre GE2025 Ni wazi CHADEMA sasa imegawanyika, kuirudisha kuwa pamoja ni Mbowe kutogombea uenyekiti tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
simjui Mbowe, ila matendo ya Lisu yamenitoa imani kwake. He was one of my favorite politician. Kumbe ni mropokaji...... juzi kasema hawezi kugombea uenyekti na Mbowe, leo anagombea...utamwamini mtu kama huyo?
Huu utetezi achana nao maana utaingia aibu ya bure? Unakumbuka yule mgombea wa kuokoteza uchaguzi mkuu wa 2015 kutokana na pesa zake? Unakumbuka waliokuwa wanamuIta fisadi, na kuishia kubadili gia angani?
 
Maana yake Mbowe ameshindwa kuitengeneza CHADEMA kuwa chombo kinachojiendesha kwa mifumo ya kitaasisi. Ni one man show mliyo ikataa kwa Magufuli.
Taasisi lazima kuwe succession ya uongozi tena ni seamless.
Tafsiri yake siyo hiyo.huwezi kumlinganisha mbowe na lissu
 
Kasema haendi popote,
Na anasema kuna wananchi, viongozi, na wengine wengi tu wamemfata kumuomba agombee😅🤣🤣.
Anagombea nini sasa huku kaapa haondoki.
 
Mbowe hawezi kuachia uwenyekiti CHADEMA kirahisi. Miaka yote alifanikiwa kuturubuni kwamba waliokuwa wanaitaka nafasi ya uwenyekiti ndani ya CHADEMA tofauti na yeye kwamba walikuwa hawafai na wakorofi. Na kwa ujinga wetu alifaulu sana kutuaminisha hivyo.
 
Mambo aliyoyaongea Lissu kuonyesha weaknesses kadhaa za kimfumo ndani ya Chama ni "indirect" attack kwa Mbowe.

Kama Mbowe ataamua kugombea na Lissu akashindwa (kihalali au kwa figisu), most likely Lissu ataondoka CHADEMA na chama kitapoteza mvuto wake kwa kiasi kikubwa sana

Miaka 20 ni mingi na Mh. Mbowe angekaa kando tu na kuwa mshauri wa chama.
Hamna kitu kama hicho.Lissu ni ngoma inayopigwa sana, itapasuka tu, anatiwa kichwa anakubali.
Nyie mnaamini sana wanaharakati, mabadiriko ni zaidi ya maneno mengi na kuropoka..check mwanaharakati Mwabugusi wa kipindi kile na huyu wa sasa baada ya kupewa kijiti amekuwa mwanafalsafa...mabadiriko sio kitu kidogo kama Lissu anavyoropoka.
Na mapungufu yako everywhere sio CHADEMA tu
 
Back
Top Bottom