Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!


 

Attachments

  • IMG-20240821-WA0004.jpg
    96.2 KB · Views: 5

Naomba nikuelimishe tu kuwa; Huwezi kabisa kulinganisha Kilimanjaro na Ngorongoro
Kilimanjaro ule mlima umezungukwa na mbuga ya wanyama (Kilimanjaro National park) na hakuna mtu hata mmoja anaishi ndani ya eneo la mbuga; watu wote (wachaga) wapo nje kabisa ya mipaka ya National park; sawa tu na watu waliopakana na serengeti, tarangire, Mikumi, nk nk nk. Kwa upande wa Ngorongoro, Wamasai wanaishi NDANI YA PARK pamoja na wanyama!
Vitu viwili tofauti kabisa!
 
Niulize....
Ngorongoro nani alimfuata nani?
Wanayama waliwafuata wamasai au Wamasai waliwafuata wanyama...

Maana hao tangu enzi na enzi wanaishi hivyo....
 
Niulize....
Ngorongoro nani alimfuata nani?
Wanayama waliwafuata wamasai au Wamasai waliwafuata wanyama...

Maana hao tangu enzi na enzi wanaishi hivyo....
Kwenye mbuga za wanyama karibia zote kulikuwa na watu wanaishi; ila baada ya sheria ya kuzilinda kupitishwa (baada ya uhuru) watu wote waliokuwa wanaishi ndani ya maeneo yenye wanyama walihamishwa na ndipo mipaka ikawekwa. Wamasai pia ilikuwa wahamishwe, ila ikaonekana kuwa, walikuwa wachache sana; na utamaduni wao wa kutokula wanyama pori na nyumba zao zilizokuwa rafiki wa mazingira zilionesha kuwa, hawakuwa na madhara kwa mazingira na kwa wanyama.
Sasa hivi wamasai wameongezeka sana, huko morogoro wamejaa lakini pia, utamaduni unaenda ukibadilika, kula na hata kujenga nyumba za kisasa ambazo sio rafiki wa mazingira yale.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…