Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

Wakati Ngorongoro inaanzishwa 1959 hao Wamasai walikuwepo ndani ya hifadhi au hawakuwepo?
Kwenye mbuga za wanyama karibia zote kulikuwa na watu wanaishi; ila baada ya sheria ya kuzilinda kupitishwa watu wote waliokuwa wanaishi ndani ya maeneo yenye wanyama walihamishwa na ndipo mipaka ikawekwa. Wamasai pia ilikuwa wahamishwe, ila ikaonekana kuwa, walikuwa wachache sana; na utamaduni wao wa kutokula wanyama pori na nyumba zao zilizokuwa rafiki wa mazingira zilionesha kuwa, hawakuwa na madhara kwa mazingira na kwa wanyama.
Sasa hivi wamasai wameongezeka sana, hadi huko morogoro wamejaa lakini pia, utamaduni wao unaenda ukibadilika, kula na hata kujenga nyumba za kisasa ambazo sio rafiki wa mazingira yale .....
 
Wakidai hiyo nchi yao basi itabidi wafukuzwe sehemu zote zingine nchini. Sijui kama watatosha na kuelewana kwenye hiyo ‘nchi yao’🙂
Watatosha vizuri tu. Unajua watu wote duniani wanaweza kuishi ndani ya Tunisia na wasikanyagane?

Kilimanjaro ni pakubwa sana. Hata wakirudishwa wote hawatafikia population density ya Bangladesh
 
Naomba nikuelimishe tu kuwa; Huwezi kabisa kulinganisha Kilimanjaro na Ngorongoro
Kilimanjaro ule mlima umezungukwa na mbuga ya wanyama (Kilimanjaro National park) na hakuna mtu hata mmoja anaishi ndani ya eneo la mbuga; watu wote (wachaga) wapo nje kabisa ya mipaka ya National park; sawa tu na watu waliopakana na serengeti, tarangire, Mikumi, nk nk nk. Kwa upande wa Ngorongoro, Wamasai wanaishi NDANI YA PARK pamoja na wanyama!
Vitu viwili tofauti kabisa!
Exquisite comment [emoji7]

Kudos

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Niulize....
Ngorongoro nani alimfuata nani?
Wanayama waliwafuata wamasai au Wamasai waliwafuata wanyama...

Maana hao tangu enzi na enzi wanaishi hivyo....
Binadamu wamewafuata wanyama kwani mbinguni hakuna wanyama....wametoka kwao huko mbinguni kuja kuwasumbua wanyama tu [emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye mbuga za wanyama karibia zote kulikuwa na watu wanaishi; ila baada ya sheria ya kuzilinda kupitishwa (baada ya uhuru) watu wote waliokuwa wanaishi ndani ya maeneo yenye wanyama walihamishwa na ndipo mipaka ikawekwa. Wamasai pia ilikuwa wahamishwe, ila ikaonekana kuwa, walikuwa wachache sana; na utamaduni wao wa kutokula wanyama pori na nyumba zao zilizokuwa rafiki wa mazingira zilionesha kuwa, hawakuwa na madhara kwa mazingira na kwa wanyama.
Sasa hivi wamasai wameongezeka sana, huko morogoro wamejaa lakini pia, utamaduni unaenda ukibadilika, kula na hata kujenga nyumba za kisasa ambazo sio rafiki wa mazingira yale.....
Watanzania wote wangesapoti wamasai kuondolewa ikiwa wangekua hawapewi waarabu. Yani hicho ni kigezo tu na sababu. Hakuna uhalisia kabisa. Uondoe Mtanzania umueweke Mzungu au mwarabu? No way!
 
Back
Top Bottom