Akhsante Mkuu kwani hapo nimemsikia vizuri kabisa Mghani / Rapa / Atalaku / Animateur Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE )ambaye ' ID ' hii ninayoitumia hapa imetokana na Mimi ' Kumpenda ' mno akifanya Vitu vyake katika ' Kunogesha ' huo Wimbo kule katika ' Sebene ' huku akisaidiwa kwa mbali na ' Role Model ' wake katika ' Kughani ' huko na Mwalimu wa 85% ya Waghani ( Marapa ) wote wa Congo DR ya sasa Yombo Lumbu ( Tutu Calugi Kalunjiste ) pamoja na Marapa ( Waghani ) wawili walioimba pia hapo vipande kidogo katika huo Wimbo akina Noah Jeune ( Kilimandjaro ) na Marehemu Faustine Nzinga Yankobo ( Cellulaire Mokili Mobimba )

Bado sijaona Bendi nzuri, yenye Vipaji na inayonifanya Siku zote niwe na furaha nayo kama ya Wenge Musica BCBG chini yake Mwenyewe Jean Bedele Tshituka Mpiana a.k.a Mukulu ya Bamukulu a.k.a Souverain Premiere a.k.a Sulutani a.k.a Mareshale Mukulu a.k.a Papa Cheri a.k.a Lonkia Milo Dan Nkokoo a.k.a De la Patria a.k.a Bin Adam.

Ukiona tu GENTAMYCINE anakipenda Kitu fulani sana jua ya kwamba kwa 100% ni Kizuri, Bora na hata Mwenyezi Mungu na Malaika wake akina Jibril na Mikaela nao wanakipenda. Sijawahi na sina Historia ya Kupenda Vitu ' vibovu vibovu ' katika Maisha yangu. Mnaopenda Miziki ya Kikongo nawaombeni msitafute ' Kuboreka ' huko Kwingineko na anzeni sasa kuwa ' Wafuasi ' wa Wenge Musica BCBG.
 
Kuna hiz pia jaribu kusikiliza extra musica- Fred , extra musica masambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hiz pia jaribu kusikiliza extra musica- Fred , extra musica masambo

Sent using Jamii Forums mobile app

Extra Musica hawajawahi Kutoa Wimbo uitwao ' Masambo ' kama ulivyoandika hapo bali walitoa Wimbo maarufu na ambao uliwatambulisha vilivyo uitwao ' Losambo ' ukiwa na maana ya ' Maombi ' Kwake Mwenyezi Mungu. Ni bendi nzuri na naiheshimu sana ila walikuja Kunikera pale walipogombana na wakagawana hadi kupelekea Kuwepo kwa Extra Musica Internationale aliyobaki nayo Mpiga Gitaa la Rhythm Durel Luemba na ile Extra Musica Zangul Zangul aliyobaki nayo Mpiga Solo ' Tishio ' kabisa Congo Brazaville Ibambi Ikombi ( wengi mnamjua kama Roga Roga )
 

Attachments

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…