GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Akhsante Mkuu kwani hapo nimemsikia vizuri kabisa Mghani / Rapa / Atalaku / Animateur Pitshou Lisimo ( GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE )ambaye ' ID ' hii ninayoitumia hapa imetokana na Mimi ' Kumpenda ' mno akifanya Vitu vyake katika ' Kunogesha ' huo Wimbo kule katika ' Sebene ' huku akisaidiwa kwa mbali na ' Role Model ' wake katika ' Kughani ' huko na Mwalimu wa 85% ya Waghani ( Marapa ) wote wa Congo DR ya sasa Yombo Lumbu ( Tutu Calugi Kalunjiste ) pamoja na Marapa ( Waghani ) wawili walioimba pia hapo vipande kidogo katika huo Wimbo akina Noah Jeune ( Kilimandjaro ) na Marehemu Faustine Nzinga Yankobo ( Cellulaire Mokili Mobimba )
Bado sijaona Bendi nzuri, yenye Vipaji na inayonifanya Siku zote niwe na furaha nayo kama ya Wenge Musica BCBG chini yake Mwenyewe Jean Bedele Tshituka Mpiana a.k.a Mukulu ya Bamukulu a.k.a Souverain Premiere a.k.a Sulutani a.k.a Mareshale Mukulu a.k.a Papa Cheri a.k.a Lonkia Milo Dan Nkokoo a.k.a De la Patria a.k.a Bin Adam.
Ukiona tu GENTAMYCINE anakipenda Kitu fulani sana jua ya kwamba kwa 100% ni Kizuri, Bora na hata Mwenyezi Mungu na Malaika wake akina Jibril na Mikaela nao wanakipenda. Sijawahi na sina Historia ya Kupenda Vitu ' vibovu vibovu ' katika Maisha yangu. Mnaopenda Miziki ya Kikongo nawaombeni msitafute ' Kuboreka ' huko Kwingineko na anzeni sasa kuwa ' Wafuasi ' wa Wenge Musica BCBG.