Unamaanisha huu mkuu...?

Mkuu kuna wimbo mmoja hivi umeimbwa na wadada wawili hivi kama wapo msituni wapo na DJ na washkaji zao kama wanaparty hivi.

Siujui jina wala waimbaji ila ni RNB ya mbelembele huko mkuu. Msaada aisee.
 
Kuna zile nyimbo za Colombo Disco chart volume 2...Zilikuwa zikitoka mpaka 11 na kuendelea...

Ila kama kuna mwenye Colombo disco chart vol 2....naomba tafadhalini viongozi...
Huu ni Uzi Maalum kwa MwanaJF kutoa Wimbo wake ambao amekuwa akiutafuta kwa miaka mingi, Bila ya Mafanikio. Kwa yule aliyenao anaweza kumsaidia mwenzie kwa kumtumia wimbo huo hapa.

View attachment 628965

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waungwana msaada hapa jamani.
Papito mbala jb mpiana.
Cristina.bushoke.
Neema.bushoke.
Solitude.extra musica.
Fanta papi kocha.
 
Kuna mwingine ulikuwa unapigwa kama kionjo cha kipindi cha radio uhuru kipindi hicho kulikuwa kuna kipindi cha vichekesho kiliitwa Chelsea pina walikuwa wanapiga wimbo huo wa chelea pina naomba mwenye kumbukumbu nao au kama anao autume itakuwa poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mwenye shibe kumkumbuka mwenye njaa/
naona ni zaidi ya upendo duniani mpaka kwa jah/
Inanifanya niamini mimi na wew sambamba/
Kwa kumshirikisha na Mungu kwa kumwomba/
Meli ya yetu haigongi mwamba/
Ndo mana ukipata shida kila unaponambia/
Naona sio yako tu hata mimi inanihusu pia/
Utanzania ndo nguzo/
uzalendo/
kama utawekwa mbele wakat wa matatizo/
ndo mwendo/
kubwa litakuwa dogo/
Mimi na wew tuna uwezo wa kishindo/
Undugu si kufanana/
Undugu ni kusaidiana/
Kumpa mwenye kuhitaji ni kumkopesha maulana/
atalipa bwanaaa

Afande sele alitisha sana hii verse
Kuna wimbo mmoja sikumbuki jina ameimba dudu baya Afande sele na wasanii wengine wa bongo msaada tafadhali ni wa kitambo kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wadau habari....nisaidieni
Kuna wimbo zamani tbc walikua wanaupiga sana .....wanaimba "yarabana sikuiba ya raaabana sikuua....."...
Sikumbuki vizuri ni lugha gan ila sio wa kidini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…