Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Msaada wa jina la huu wimbo au kama kuna mtu anao.
 
Kuna nyimbo sijui imeimbwa na nani ila nahisi ni wakongo,kwenye verse inasikia hivi Danse danse eeeh mwenye nayo aitupie hapa
 
Natafuta wimbo,..flan zilipendwa..nakumbuka mistari tu ,

Kitanda kipo wananilaza chini
Chakula kipo wananipa makombo
Mama fanyeni hima mje mnichukue..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu vipi ulipata wimbo wa ney wa mitego..kama ulifanikiwa nidondoshee hapa nausaka sana huo
Kaka Mkuu KIOO ahsante sana, leo toka asubuhi nimepitia page zote 403 nimevuna OLD which is GOLD. Muziki unaoishi. Ahsante Secret Star kwa uzi huu.
OMBI.
1. Ngoma ya Ney wa Mitego alfanya Bongo Record mapema sana inatembea hivi, ".... Kuishi Manzese imekuwa shida, mambo yanavyokwenda baby sijui kama utaweza...."
2.
Crazy GK Feat Fid Q sikumbuki jina ila "..... wamevunja makanisa ili wajenge casino...."

Shukurani kwa madini wana JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani mwenye access ya wimbo wa POWER 001 wa FALLY IPUPA nauomba.
 
kuna ngoma moja inasikika saut kama ya papii kocha...
chorus yake inaimba..
"nimpate wapiii, nimtafute eeeh wapi ntamuona wapiii
nitulize nisiwe na wasiwasi"
kama kunamtu anaijua anisave
Kama sijakosea ni wimbo ambao Papi kocha ameshirikiana na lady jaydee. Jina silifahamu so ingia you tube waulize tu Papi Kocha ft.lady jay dee yawezekana upo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna ngoma moja inasikika saut kama ya papii kocha...
chorus yake inaimba..
"nimpate wapiii, nimtafute eeeh wapi ntamuona wapiii
nitulize nisiwe na wasiwasi"
kama kunamtu anaijua anisave
Anaitwa

Richie Ritch ft Jay dee_Caroline


Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
 
Back
Top Bottom