Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Wakuu naomba mwenye kufahamu jina la nyimbo hii na alieimba anisaidie naitafuta sana niliwahi pia kuisikia ikipigwa kwenye movie ya Predator ya Arnold Schwarzenegger naisaka bila mafanikio msaada pls
Hii ngoma imepigwa na Richard inaitwa long tall sally.

Ninayo kwenye maktaba yangu hii...unapenda nikutumie kwa means ipi?
 
Kuna wimbo unaitwa huja juu wa juwatta jazz band umeimbwa maliim gurumo
Mwenye nao anisaidie kuupata
 
Jamani naomba kama kuna mtu ana wimbo wa VijanaJazz nahisi unaitwa HESIMA YA NDOA, baadhi ya mashairi "enyi wote wake zangu mapenzi yangu kwenu ni sawa mpendane ndio hesima ya ndoa eee" Bi mkubwa analamika jamaa analala kwa bi mdogo tu, kuna sehemu jamaa anajitetea wakati anaenda kulala kwa bi mkubwa akamgonga bata njiani
Na mm pia natafuta wimbo wa vijana jazz unaitwa massaki
 
Wimbo wa zamani kidogo lakini sikumbuki kaimba nani nakumbuka mistari ya mwanzo tu

Mara ya kwanza kukuona ilikua coco beach,
Nikawauliza washikaji wakasema wewe ni bitch,
 
Wimbo wa zamani kidogo lakini sikumbuki kaimba nani nakumbuka mistari ya mwanzo tu

Mara ya kwanza kukuona ilikua coco beach,
Nikawauliza washikaji wakasema wewe ni bitch,
Una kiitikio kinasema...sio kwamba mi sitaki dem, ila sikumwona mwenye sifaa. Nadhani Unaitwa Sina Demu au Sitaki demu. Ni wa long time kabla ya Staki dem ya Juma Nature.
 
Natafuta nyimbo za renee ramila na wimbo wa nasma khamisi kidogo subakheri huu ambao kina aslay na nandy wameusample sasa nataka wa nasma
 
Mii natafuta nyimbo mbili ambazo nakumbuka choruses zake na jina la wimbo wa pili.
1. Mgambo tuheshimiwe, tuthaminiwe ee, migao na mikoko nasi tupewe , tupendelewe
2. Eeh kuna mambo mengi ni, nimekufanyia weee mpenzi waangu
Lakini kuna kitu ki, moja nimesahau, kukueleza.
Huu wa pili kama sikosei unaitwa "uko bize" . Nyimbo zote mbili sijui waimbaji na mahali pa kuzipata.
 
Una kiitikio kinasema...sio kwamba mi sitaki dem, ila sikumwona mwenye sifaa. Nadhani Unaitwa Sina Demu au Sitaki demu. Ni wa long time kabla ya Staki dem ya Juma Nature.
Yap ndo huo chief.Sijajua jina na nitaupataje...

Mkuu wewe utakua muhenga kama mie (joking)
 
Back
Top Bottom