Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo sijui kaimba nani,
Kama vile banana zolo lakini nimeutafuta YouTube siuoni Labda nakosea jina la wimbo, anaimba

'Sogea nikushike mkono,Sogea nikushike kiuono,Sogea tuonge,tuzungumze nakupenda baby'
Sogea nikushike kiuno,Sogea nikushike mkono,Sogea tuongee tuzungumze nakupenda saana'
 
Naitafuta ile Beat ya Radio tumaini Asbh kwenye kipindi cha Kumbukumbu.
 
Ndugu wazee kuna wimbo mmoja nautafuta sana wa bendi ya zamani (nadhani Jamhuzi au Western Jazz). Siukumbuki jina lake lakini chorus yake inaimbika kama nilivyorekodi kwenye audio (attached). Naomba aliye nao au anayefahamu tittle ya huo wimbo anisaidie jamani. Natanguliza shukrani.
Unaitwa Simba Tamu!
 
Nisaidieni hizi
1.nguvu za giza - Bwana misosi.
2.Jipe moyo - Bwana misosi.
3. Tucheze wote - Bwana misosi
4. Mnauliza nini - Bwana misosi.
 
Wanajamii kama Heading inavyosema nisaidieni Mwenzenu Nahitaji nyimbo za kwaya/Dini ya Roman Catholic kama unazo nisaidie ku upload hapa nami nitasave!
Mbarikiwe katika Jina La Bwana!
MKATOLIKI
Kati ya Gospel ambazo ni "The Best" kwa RC, ni zile walizoimba mwaka 1990 wakati wa ujio wa Baba Mtakataifu Papa Yohanne Paul II. Nasikia ukienda pale St. Joseph Cathedral zipo wanaweza kukuuzia.
Mojawapo ya nyimbo zilizopigwa kipindi hicho ni huu hapa:

Kweli aisee
 
Kweli aisee
Sasa hizo nyimbo zipo na ni Album nzima, na nyimbo zote ni kali muno.

Vipi unaweza ukawa una idea hawa waimbaji walioimba hapa siku ya kusimikwa Baba Askofu Gervas Nyaisonga huko Mbeya; ni kwaya gani? Kuna wimbo waliimba hapa ni mzuri sana; sema tu wimbo hausikiki vizuri sana. Jaribu kuusikiliza huu hapa:

Ni kwaya ya Mt Judethadeus jimbo kuu mbeya, Mashahidi wa Uganda nzovwe na Mwenyeheri anuarite
 
Habari wa kuu, kunawimbo wa machozi band kwa jina siujui , nimejaribu kuutafuta kwa lyrics zake bila mafanikio , kwa anayeujua naomba anisaidie . Baadhi ya maneno ya wimbo huo ni haya "moyo ni nyama tupu , ukioza wapotea haibaki mifupa , nakukabidhi uutunze" inawezekana lyrics sijapangilia vizuri , natanguliza shukrani
Lady Jaydee ft Banza Stone.
"Moyo ungekuwa na mfupa, mabaki ningeyapata.
Lakini kamili u-nyama, ukioza umeoza"
 
Ni kwaya ya Mt Judethadeus jimbo kuu mbeya, Mashahidi wa Uganda nzovwe na Mwenyeheri anuarite
Wanaimba vizuri sana. Unaweza kunitafutia wimbo huo kwenye youtube

Sikiliza mwingine huu hapa wa Kapotive Singers Bukoba. Hawa ndiyo wale wale walioimba ule wimbo maarufu wa MIMINA

Halafu kuna wimbo mwingine wa kwaya ya masista watupu, wanaimba huku wakiwa wanapiga tarumbeta, wamevaa mavazi yao ya u-Sister halafu wamependeza utadhani ni Malaika wameshuka kutoka mbinguni. Nilikuwa nao niliurekodi kutoka kwenye Tv lakini bahati mbaya baadaye nikaupoteza, na title yake siikumbuki na hivyo siwezi hata kuutafuta kwenye youtube
 
Back
Top Bottom