Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Kuna wimbo mmoja hivi miaka ya 90 uli hit, wakati huo Disco zilikuwa zinatawaliwa sana na ngoma za nje haswa US lakini hii ilipenya.

Ngoma ilikuwa inaimba "nimeinama nimeinuka nimeokota kidude...kilakshari kilakshari Pugu Kariakoo" , sijui ni nani walipiga hii ila ilibamba kinoma kwenye Madisco enzi hizo.
 
Kuna ule wimbo ulikuwa unaibwa "wazungu ni wetu walituletea shanga za kuvaa shingon" sijui hata aliimba nan
 
Kuna ile biti moja hiv ya sebene wanapiga sana ngoma na filimbi,nakumbuka waliwahi kuicheza akina Joti,Masele Chapombe,Mkwere,Mpoki,Masanja wakati wanachuja wasanii wa kuunda kundi la Ze comedy
 
Hivi kwaya gani iliimba “Nitaimba siku zote kwa Yesu Moyo Mkuu, kulikoo... kuliko vitu vyote....
 
Vitu
 

Attachments

Mimi natafuta wimbo niliousikia nipo msogo sana.
Sijui unaitwaje na sijui kaimba nani.
Nanukuu.

Aiya iya iya ii! Aiyaooo, aiyaoooo.

Nilijisikia wimbo huu miaka 19 iliopita. Msaada jamani japo link au jina la msanii na wimbo husika.
 
Mimi natafuta wimbo niliousikia nipo msogo sana.
Sijui unaitwaje na sijui kaimba nani.
Nanukuu.

Aiya iya iya ii! Aiyaooo, aiyaoooo.

Nilijisikia wimbo huu miaka 19 iliopita. Msaada jamani japo link au jina la msanii na wimbo husika.
OBSESSION- JANGU
upo youtube
 
Nihurumie eeh nipo mashakani nisije nikaumia ooh nipo mashakani


Maneno ya nyimbo nimeitafuta bila mafanikio iliimbwa live aliyeimba alisema imeibwa na kilwa jazz lakn sijaipata
 
Natafuta wimbo huu wa mshenga ni zilipendwa

.....Kumbe mshenga katoroka pesa na mali hakupeleka yeyeee ..ooho
..Tulipofika mahakamani eee....mshanga aruka, adai hakupokea pesaaa....aliuliza ushahidi uko wapiiii...."
 
Back
Top Bottom