Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
KUBU au KANYAMA nyimbo Inaitwa -MENU au MENYU

Huu ni Bongofleva Hiphop ya kitambo sana
 
Wadau wimbo wa Kwetu Mbeya wa mwanamama SISTER DAS wimbo unaitwa SEMA NO/USIKUBALI DADA.

Mwenye nao plz atume hapa
 
Natafuta nyimbo ya mwansasu inaimbwa hivi,(Aiye,aiye masiha aaaa,x 2) napokosa mahitaji ktk maisha yangu ,napokosa mahitajii katika nyumba yanguu, yesu ndio kimbilio.....


Nimehaingika sana jina la wimbo huo
 
Wakuu naomba anayefahamu wimbo huu unaitwaje au uliimbwa na nani anisaidie.

 
Samahani wadau
Nautafuta wimbo wenye mashairi yafuatayo.
" Nguo chakula malazi ni buree, uliona raahaa, saasa mambo yamebadilika unatafuta mwenyewe umepata wakukutunza ni heri uishi nae,
Kwani maisha ya sasa uhuni hauna maana wazazi wako ni waungwana utawaletea aibu uu"

Wimbo nautafuta saaana, hata bend iliopiga nimeisahau sijui ni washirika Tanzania stars au Marquis original

Mwenye nao pliiiiz
 
Wadau wote kwenye uzi huu, natafuta wimbo wa diamond sound - ikibinda nkoi, huwenda umewekwa hapa ila uzi ushakuwa mrefu.

Nimeona Neema na Kimalumalu natanguliza shukrani
 
Wanajamvi kheri?
Nina ugonjwa wa moyo tiba yake ni wimbo wa Stara Thomas ft Chid benz unaitwa "Nini sina " producer Lamar.

Natanguliza shukrani za dhati kabisa [emoji120]
 
"Nilipokuona mara ya kwanza Jackie nilijiuliza Malaika katoka wapi kweli Baba Mungu alikuumba nywele za kuanguka uko mrembo Jackie........
Mungu akulinde mama akusaidie pia ....."
Nautafuta sana wimbo huu,umeimbwa na Mwanamziki wa kike nadhani kutoka Kongo
 
"Japo ni maskini lilikupenda kwa dhati
Niliamini moyoni mapenzi siyo pesa
Wapo wenye pesa wameshindwa kununua penzi
Ulinidharau ......
Aeee
Ulidharau nazi wakati embe ni tunda la msimu
Kufika mjini ukageuka pazia huwezi toka ndani kama hujaletewa mdundiko ukipita unauchezea ndani ......
...................mdundiko ukipita unakatikia ndani ......
Aeee uligeuka mwali wakati wewe ulisha chezwa ngoma
Oh nyamala mwanangu ................
Oh nyamala mwanangu utapata mwali mwingine Baba
...kwanza mtu mwenyewe mdomo fremu......"
Mwenye huo wimbo nautafuta sana
 
Wadau nahitaji msaada wa kupata beat zingine ambazo zote zilikuwa kwenye album hii zilitumika Sana kwenye masherehe miaka ya 95 hadi 2000 zote zilikuwa ni beat tu, nimebahatika kupata moja tu ambayo ndiyo hiyo mnaisikia, naomba ambae nazifahu nanisaidie wapendwa..hata kama ni jina la album aniambie maana hata jina silifahamu nazikumbuka tu beat zote, naombeni msaada wenu wadau,
 
Back
Top Bottom