Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Kupitia yale mliyoyafanya kipindi cha nyuma yanaweza kukusaidia kupata zawadi itakayomfurahisha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera sana mkuu kwa kuona umuhimu wa kumpa mkeo zawadi kwa changamoto alizopitiaNawaza zawadi ya kumpatia mke wangu kama 'surprise' tu, kutokana na changamoto alizopitia mwaka jana, mwezi kama huu, mpaka ikafikia hatua ya kukata tamaa ya kuishi.
Alifiwa na mzazi wake aliyempenda sana; aliyekuwa akimuuguza muda mrefu.
Kabla ya mzazi wake hajafariki, ndani ya wiki mbili hivi, 'wife' akafanyiwa upasuaji mkubwa, hajamaliza hata wiki, akatakiwa kufanyiwa tiba ya mionzi. Ile kuanza tu tiba ya mionzi, mzazi wake akafariki.
Ndani ya muda mfupi, vichwa vilikuwa vimevurugika sana; lakini tuliweza kuhimili ingawa changamoto zilikuwa nyingi.
Sasa nawaza, nimpe zawadi gani itakayomsababisha kutoa machozi ya furaha, iwe kama 'surprise'.
Kama gari, yeye siyo mpenzi sana, hata lililopo huwa halitumii; kama ni nyumba, anaweza asione kama zawadi, kwa sababu itakuwa kama sehemu ya familia (yeye na watoto).
Nawaza, zawadi ambayo yeye ataiona inamgusa yeye tu.
Karibuni kwa mawazo.
Fuata ushauri wa huyu jamaa!.. ni ushauri Bora kabisaTafuta eneo zuri ambalo limetulia hasa hotel zilizopo kwenye mbuga za wanyama huko au hoteli zilizo karibu na mwambao wa ziwa lolote kwenye Beach nzuri na tulivu, kaeni chini nunua chakula anachokipenda na kaa mkao wa kumwangalia kisha mwambie namna unampenda mwambie hata kama kutakuwa na changamoto ya zile zilizopita bado utaendelea kuwa nae tumia siku hata 3 na ikiwezekana zima hata simu tumia mda huo kuongea nae, kama ni mkristo nunua zawadi Bible mpe mwambie nakupa neno la uzima baki nalo duniani na mbinguni
Uchawi wote uko hapa. Ongeza mapenzi na kujali. Ongeza muda wa kuwa pamoja. Material thing hayana mchango mkubwa sana.Muonyeshe mapenzi ya dhati,mjali na mpe faraja.