Ni zipi mbinu za kudhibiti wizi kwenye duka la jumla?

Fsnya investment badala ya business au nenda pale Mlimani ity uone wanvyofanya tumia barcode
 
Ushauri huu mzuri.. thanks mkuu
 
P POINT ya mwaka
 
Boss hakuna njia ya kuzui kuibiwa ila kuna njia za kupunguza kuibida yaaani wizi ufanyike kwa uchache

1) tenganisha duka na stooo weka kumbuku kumbu ya mali inayoingia stoo

2) funga kamera mlangoni stoo kisha kila mali inayotoka stoo kwenda dukani/ kuuzwa lazima iandikwe

3)kazi yako kubwa iwe kuangalia ni mali kiasi gani inatoka/tafuta kijana wa stoo atakuwa anatoa mzigo

Mfumo huu unapinguza wizi wanatumia sana watu wa moshi mfano kwa MARENGA pale au Kwa LASWAI
 
Naona mpaka Sasa....jamaa hajapata mbinu sahihi...,....wapo waliosema mifumo,wengine camera.....zote zinamapungufu......kifupi binadamu ameshindikana.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hii nimeichukua
 
Duuh aisee pole na hongera kwa machale. Napata wazo jipya pia hapa kwa kusoma hili
 
Ngoja ni-nene nliyojifunza hapa kwa faida ya wengine sharing is caring.

1. Dukani pawe na software nzuri yenye maingizo/mauzo/stock kifupi moments zote za dukani ziwe systematically.

2. Tenga muda, au weka mkakati au utaratibu wa kufungua box uangalie kilichomo ndani (Fanya randomly) na ukague mara kwa mara hata mpigaji onamjengea kuwa boss anakagua uchakachuzi. Beba box kadha wa kadha kupima uzito unafanana au unatofautiana.

NB kifupi uwe na utaratibu fulani wa kuwa Fanya waone boss yupo serious.

3. Kama utaweza ukatengeneza sole tape fulani unique yenye logo ya duka ukaimiliki only you mwenye duka. Ukapiga tape maeneo ya kufungua box Ili ukiona sign ya ujanja ujanja inakua rahisi kugundua ubadhilofu.

4. Camera muhimu kama walivyosema wadau wengine. Mdau mmoja akasema stoo na duka vitengane. Changamoto wkt mwingine zikiwa mbali mbali Kuna room ya manoeuvre ila ni kupambana TU.

5. Panga utaratibu wa kupita na stock na mauzo uone je mauzo na vilivyobaki vinaongea lugha moja au la! Wasikukariri kwamba Kila ijumaa boss anapita, Fanya mambo ya ghafla itawajengea vijana kujua wapo kwenye kikaango wkt wowote.

6. Kwa kweli nawashukuru nyote mliotoa nondo za kueleweka. Mmenipa new experience ikiwa nipo mbioni kufanya biashara hii. Mmbarikiwe na hayo hapo juu ni ambayo nimeona kama ni mkakati fulani wa kupunguza kupigwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…