Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Kipindi hiko Mishahara wakisubiri mpaka tarehe 15 ya mwezi ulifuata kudadeki na maallamiko juu huku wakilia na kusaga meno, hela ya kulipa mishahara mpaka ikikopwa
Mfuate huko huko sasa
 
Nimekusoma mara 2 halafu nikarudia na UZI but sijaona uhusiano wa mchango wako na UZI tunao changia; kwanini usifungue uzi wako mpya wa kumtukana Mbowe ili tuje tuchangie huko!? Anyway, kimjazacho mtu ndicho kimtokacho. Inaelekea Mbowe kupiga machine ya Joyce inawauma wengi sana, nadhani itabidi nitafute picha Joyce nimuone na mimi, huenda ni pisi kali sana.
 
Huyo dogo ni pandikizi jipya lenye lengo la kuharibu thread zote zinazo kosoa mambo ya jiwe
 
Mtu yupi huyo atakaesema msoga chap! Acha ulevi..ww uliumizwa kwa sabab ulikuwa mwiz enz za msoga..mtanzania wakawaida aliezoea kujiatia kipato chake kwa njia halali kamwee hawez kuwa upande wa msoga na genge lake la madawa ya kulevyaa..ww ulikuwa mkwepa kodi..kama sio bas ulikuwa unapata kipato kwa njia isiyo sahh..au ulikutwa na cheti bandia..
 
Weee msukuma acha propaganda! Meko alikuwa mtu hatari kuliko shetani.
 

Mkuu mwaga nondo nakukubali
 
 
 
Mkuu fungua hiyo link
 
Lowasa yupi?
Lowasa aliyetukanwa matusi ya ajabu na uvccm?
Ndio huyo huyo, Lowassa alisafishwa vizuri tu alipoenda Chadema maana kabla ya hapo alikuwa anatambulika kuwa ni fisadi tu hakuna ambaye angefikiri kwamba fisadi huyo anaweza kugombea urais nje ya Ccm ila Chadema walimfanyia kazi nzuri sana huyu mzee hadi raia wakampigia deki barabarani na inasemwa kuwa alishinda uchaguzi kihalali kama si ccm basi pengine hadi sasa angekuwa ndio rais wa Tanzania.

Kwahiyo kwa record hizo mimi naona kabisa hii kazi ya kumsafisha Jiwe wapewe tu Chadema.
 
Ndugu yangu nikuambie kama kitu Mwendazake aliharibu ni kwenye eneo la kuumiza watu kwa kisingizio cha maendeleo.

Ukiachana na waliobomolewa nyumba Kimara - Kibaha kwa ajili ya uhenzi wa barabara wa njia nane. Wengi wa aliowaumiza aliwaumiza kwasababu za kisiasa tu. Wengi ni wale walijaribu kuanika ufisadi wake au kukosoa sera zake za kukurupuka katika kufikia maamuzi ambazo matokeo yake yanakuja kuligharimu taifa.

Ukiwa ni mkweli usieongozwa na mapenzi kwa Mwendazake utakubaliana na mimi kwamba nchi hii tangu tupate uhuru nchi yetu haijawahi kuongozwa na chama kingine zaidi ya ccm.
Na ufisadi wote uliofanyika kwenye nchi hii tunaoujua na ambao hatuujui umefanywa na viongozi na wanachama wa ccm.

Lakini cha ajabu Mwendazake aliamua kuelekeza mashambulizi yake yote kwa wapinzani wake wa kisiasa kama vile ndio walikuwa wamefanya ufisasi na kuifilisi hii nchi.
Yeye aliwachukulia wapinzani kuwa ni maadui wa tanzania na aliwaambukiza hiyo mentality viongozi wengi na wafuasi wengi wa ccm.

Angalia mambo yalitomtokea Lissu na viongozi wote wa chadema. Mauaji na utekaji na kunyang'anywa au kufilisiwa mali hasa kwa watu walionekana kuzipinga sera zake hakika wamepitia wakati mgumu kwenye utawala wake.

Zaidi amejenga chuki na kuhubiri ubaguzi bila aibu.(Kiongozi unawezaje kusema eti hapa sitawaletea maji au kuwajengea kituo cha afya kwasababu nyie mlichagua upinzani) Ni aibu na hatari kwa kiongozi kuhubiri ubaguzi kwenye nchi ya kidemokrasia.

Kilichofanyika 2019 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na hitimisho lake kwenye uchaguzi mkuu 2020 ni kielelezo tosha kwamba yeye hakuwa kiongozi wa kutuweka watanzania pamoja bila kijali itikadi zetu ila yeye aliamini katika ubinafsi na kutaka watu wote wawe wanamuabudu.

Matendo hayo ndiyo yanayoharibu kabisa hata maendeleo aliyoyafanya. Angeachana na hizo tabia hala akajikita kwenye mambo ya maendeleo nakuhakikishia angejizolea sifa kubwa sana.

Uhuru,na haki vinaleta amani ya kweli. Sio barabara, reli, ndege au majengo makubwa makubwa ya hospitali au stendi.
 
Baada ya kuhamia cdm uvccm wakiongozwa na wewe na mwenzako msukuma kasheku na polepole mlimtukana sana matusi ya hovyo kisa kahama ccm.

Baadae mwenye chama chake na mmiliki wa ccm akaamua kumridisha ndani ya chama nasikia wewe na wenzako mkalazimishwa kumramba miguu.
 
Kama hatokuelewa basi msamehe
 
Umeshinda mkuu
 
Hakuna mema aliyo Fanya zaidi ya kutekeleza miradi yoote iliyo anzishwa na mh kikwete

Hawawezi kukuelewa....na hata kwa dawa huyo Meko acha aende zake tuu amekunyanyasa sana mno. na hata malimbizo ya mali hakujua jinsi ya kuzitumia alibaki kujenga airport ambayo kamwe haitakaa itumike zaidi ya mara 1 kwa mwaka. mwacheni Mwendazake aende tuu angalao watoto na mama Janet wapumue
 
Well said
 
Eti maendeleo ndani ya miaka 5, mpuuzi kabisa labda maendeleo umeletewa nyumbani kwako
 
Natamani sana kumfahamu huyo mfqdhili wenu anaye isimamia hii show mwanzo mwisho!

Maana nyuzi za kumfagilia marehemu na kumponda JK, zimetamalaki sana humu jukwaani kutoka kwa members wapya kabisa!
Mfadhili ni Polepole mbunge wa viti maalamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…