Niagize gari Afrika Kusini Vs Japan?

Niagize gari Afrika Kusini Vs Japan?

Vipi kuhusu usafirishaji wa gari toka Sauz Hali ipoje barabarani? Zimbabwe walivyo na Njaa si itakua jau Sana hiyo route?
Tunapita Gaborone, Nata,Mahalapye,Pahalapye mpaka Kazungura huwezi kupita Zimbabwe kama unakuja unaendesha kutoka SA wanataka rushwa sana na wana Road block nyingi..gari nzuri nunua Auction Nation kwa gari ndogo..
 
Vipi kuhusu usafirishaji wa gari toka Sauz Hali ipoje barabarani? Zimbabwe walivyo na Njaa si itakua jau Sana hiyo route?
Nilikua napita bara bara fupi sana Beitbridge, Bulawayo,Masvigo mpaka Chirundu hii bara bara ni fupi sana kuliko kuzunguka Harare ila shida ni Polisi wao ni wasumbufu sana sana...wakitoka polisi wa bars barani wa Zimbabwe ndio wanafata Watanzania unaweza kutoka Tunduma mpaka Mbeya umesimamishwa mara zaidi ya mara tano na wazipenda sana namba za Nje..
 
Hivi siwezi ifanyia usajiri mpakani ikaingia na plate za bongo ili hawa viwavi jeshi wasinisumbue?
 
TRA wapo bro hata vibao unapata ni wewe tu toka enzi za Mzee Jakaya...
Kumbe wanakuwa wameshaviandaa tayari? [emoji848]

Point yangu kama umenielewa ni kwamba nataka kwamba nimekwenda kuchukua gari sasa nataka nikikaribia Tanzania pale tunduma gari iwe na usajiri na nifunge kabisa plate namba ili hawa mbayuwayu wetu wasianze kutolea macho plates namba za taifa lingine na kupata sababu ya kusimamisha gari kila dakika maana katika kitu sipendi safarini especially safari ya mbali ni kusimamishwa hovyo humo barabarani na hawa jamaa wakati nimechoka nataka kuwahi home nikapumzike.
 
Kwa bei za 36m - 38m kwa model za 2013/14 sioni kama zinatofauti na kuagiza Japan. Labda utakachookoa ni muda na labda kama ubora ni tofauti.
Hiyo ya bei hiyo kwa south Africa unapata zero milage kabisa au ambayo haijatembea hata km10,000 mzee. Tofauti yake ni ubora wa gari.

Gari ya mjapani ukikuta ina milage ya 20,000km tu balaa lake ni bei utajuta.
 
Sasa kwanini watu wanapenda kuagiza gari Japan? Vipi ubora wa Gari za SA na JAPAN?
Mazoea na miundombinu. Japan miaka ya nyuma hapo watu hata hawakuwa wakijua kuwa wanaweza agiza magari huko ila hivi sasa baada ya teknolojia kukua na sheria na taratibu za kibiashara kukaa kwenye mstari ndio unaona kuna idadi kubwa ya makampuni na mawakala na madalali wakileta gari huko.
 
Unapandishaje gari meli kutokea South Africa mzee?
kwenye Scania sio gari ndogo...
0km SA yenye deef 2.8 kwa pesa ya Tsh ni kiasi Gani?,,kabla haijasafirishwa?
Screenshot_20240328-235130.png
 
Back
Top Bottom