Nichague mwanamke yupi wa kuoa kati ya hawa wawili?

Nichague mwanamke yupi wa kuoa kati ya hawa wawili?

Hongera sanaa mkuu kwa kufika hatua hiyo.. ila mwenzio yamenikuta mwaka jana 2024. Kwakifupi nikupe ABC

Kwanza kabisa.. utafiti wako kuhusu wachumba wako wa ef2 naona very weak, Yaani ujafanya utafiti wowote.. Bado unamuda wa kuwachunguza, ingia deeply mkuu.. tembelea maeneo wanakoishi fanya tafiti kuhusu familia zao na hata ukoo kwa ufupi.. ukifanya hayo njoo utupe feedback.

Pia mwanamke wakuoa unachagua wewe sio mtu akuchagulie , watu wengine wahusike kwenye kupendekeza tu, sio kukuchagulia..

NB: usikubali kumuoa mwanamke ambaye anatabia fulani ambayo huipendi, na ukitegemea atabadilika akiwa ndani ya ndoa,ilo sahau mkuu. Ukiwa na wasiwasi/hofu juu yake piga chini.
Na watu wakisema lolote juu ya mwanamke, usibishane nao,tafakari kwa kina, lisemwalo lipo , kama halipo litakuja.
 
NB: usikubali kumuoa mwanamke ambaye anatabia fulani ambayo huipendi, na ukitegemea atabadilika akiwa ndani ya ndoa,ilo sahau mkuu.
Kama ana masikio, huu ni ushauri muhimu sana imempatia. Atakuja kukushuru au kujilaumu kwanini aliupuuza
Ukiwa na wasiwasi/hofu juu yake piga chini
Hii nyongeza yako nakazia. Huo wasiwasi ni sauti ya Mungu. Aheshimu, wanawake ni wasanii wazuri

Na watu wakisema lolote juu ya mwanamke, usibishane nao,tafakari kwa kina, lisemwalo lipo ,
Chukua na hiyo
 
Chukua ambaye moyo wako unampenda, hata akiwa na mapungufu hutayaona ila ambaye humpendi utakua ukimtafutia makosa bure
 
Kama ana masikio, huu ni ushauri muhimu sana imempatia. Atakuja kukushuru au kujilaumu kwanini aliupuuza

Hii nyongeza yako nakazia. Huo wasiwasi ni sauti ya Mungu. Aheshimu, wanawake ni wasanii wazuri

Chukua na hiyo
Asante kwa kuniunga mkono mkuu..
 
Chukua ambaye moyo wako unampenda, hata akiwa na mapungufu hutayaona ila ambaye humpendi utakua ukimtafutia makosa bure
Mithali 31:30
[30]Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
 
Back
Top Bottom