Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Nicole Joy Berry mrembo aliyejulikana kwa kilimo cha vitunguu akamatwa na Polisi kwa tuhuma za utapeli

Wakuu,

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicole Joyberry kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.

Soma pia: Nicole Berry, mwanadada anayepiga mamilioni kwenye kilimo cha vitunguu Iringa

Taarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro na kusema matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wakati mwingine nje ya mkoa wa Dar es Salaam.


"Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-grouup hayo kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia," amesema Kamanda Muliro

Kilimo siyo Mchezo wewe, bado mmoja anayejifanya Mchungaji
 
Polisi wamuachie huyo katumia akili maana wajinga ni wengi Nchi hii acha wakomeshwe.
Yani na Akili zako unamtumia hela Lidemu la dizaini iyo eti badae akupe nyingi zaidi jamani jamani WaTanzania nani kawaloga.
Kweli kabisa, tena matapeli kama hao nashauri wapewe mitaji na wapate vibali vya kufanya kazi bila kulipa kodi mana wanawachangamsha wapuuzi wapate japo akili ndogo.
 
Hapo hakuna kesi ,account official yake Nicole haina hayo matangazo ya upato ,so ni easy kuwakataa kwamba wametapeliwa na so called Nicole Feki.

Ila wabongo sijui wakoje hapo washapigwa na Nicole ,akija niffa akianzishwa watapigwa za uso ,akija wema au wolper akianzisha watapigwa tena yaani hawakomi tu.
 
Kama unaikumbuka ile nyimbo ya sumalee hakunaga yule video kile kidem jamaa alikua anakibembeleza na kucheza nako ndio huyu kwa sasa"
Mmmh mbona sura tofauti
 

Attachments

  • IMG_4355.jpeg
    IMG_4355.jpeg
    119.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom