Nicole joyberry apandishwa kizimbani, akosa dhamana apelekwa segerea

Nicole joyberry apandishwa kizimbani, akosa dhamana apelekwa segerea

Joyce Mbaga (32) maarufu kwa jina la (Nicole Berry) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Ramadhan Rugemalira kwa tuhuma za kupokea Shilingi milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Mbali na Berry, mshtakiwa mwingine ni Rehema Mahanyu (31). Kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makosa matatu, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa umma na kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24, 2025, ambapo washtakiwa hao wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili na kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.


View attachment 3266353View attachment 3266355View attachment 3266356View attachment 3266357
Hizi filter yunapigwa sana sie wanaume malaaya 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Demu kakongoroka sana siku chache tu, Je akikaa miezi huko, nimepita page ya IG duh nimebaki natoa macho tu, Mungu amsaidie
 
Sasa kama anaitwa Joyce Mbaga hiyo Nicole Berry alilitoa wapi?
20250311_034424.jpg
 
Wanajifunza basi? mbwembwe zotee kufake maisha hana hata Don mmoja wa kumwekea dhamana.
Sio tu Don,hata yeye ina maana hana mali ya zaidi ya million 46?!mboba huwa anapiga picha na majeep,majumba ya kifahari aisee mtandaoni huku
 
Sio tu Don,hata yeye ina maana hana mali ya zaidi ya million 46?!mboba huwa anapiga picha na majeep,majumba ya kifahari aisee mtandaoni huku
Hapo sasa, yaani ukiwafatisha hawa unaweza kudhani kuwa una laana inakutafuna ili usifanikiwe, unaangalia kipaso chako unasema hivi na mimi nitakuja kuendesha hilo jeep kweli kumbe waaaiiiiii hamna kitu
 
Back
Top Bottom