Nicole joyberry apandishwa kizimbani, akosa dhamana apelekwa segerea

Nicole joyberry apandishwa kizimbani, akosa dhamana apelekwa segerea

Joyce Mbaga (32) maarufu kwa jina la (Nicole Berry) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Ramadhan Rugemalira kwa tuhuma za kupokea Shilingi milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Mbali na Berry, mshtakiwa mwingine ni Rehema Mahanyu (31). Kwa pamoja wanatuhumiwa kwa makosa matatu, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa umma na kupokea amana kutoka kwa umma bila leseni.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24, 2025, ambapo washtakiwa hao wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili na kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.


View attachment 3266353View attachment 3266355View attachment 3266356View attachment 3266357
Ndiyo yule mkulima wa vitunguu kule Iringa? Ht sura ya mkulima anaijua huyo
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga linaendelea na uchunguzi wa tukio la bondia Hassan Mwakinyo (29) anyetuhumiwa kwa kumjeruhi na kumshambulia mvuvi Mussa Ally (21) mkazi wa Sahare Jijini Tanga

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema baada ya tukio hilo wameanza uchunguzi huku wakiendelea kumshikilia Mwakinyo.
Kwahyo mwaknyo bado ana miaka 29 tu😂
 
Watu serikalini kila kukicha wanaiba na kutapeli billions of money hawakamatwi wala kufikishwa mahakani lakini wanyonge ukiiba hata kuku moja saa hiishi umeshafunguliwa kesi...

Mambo ya kipumbavu kweli kweli. Hii inchi ni ya wanasiasa tu na royal families na koo zao.
 
Watu serikalini kila kukicha wanaiba na kutapeli billions of money hawakamatwi wala kufikishwa mahakani lakini wanyonge ukiiba hata kuku moja saa hiishi umeshafunguliwa kesi...

Mambo ya kipumbavu kweli kweli. Hii inchi ni ya wanasiasa tu na royal families na koo zao.
Sheria inatambua evidence si nadharia na hisia, dad amanasa kwenye mtego live, hao unaofai wanaiba wamefunguliwa kesi na vielelezo?

Just because fulani anaiba haimaanishi na ww ndio uibe, else utaishia kwenye mikono ya sheria
 
Ndio ujifunze, wanakuzunguka na kukusifia leo, ndio hao hao watakaa pembeni wakati wa matatizo

Nadhani nicole akitoka huko itakuwa ni life change experience
Moja au mawili akaendelea au akabadilika,kichwa chake ndio ubongovwake ulipo!
 
Back
Top Bottom