Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Niende Capetown, Pretoria au Johannesburg?

Mimi nimempa kisa ili ajifunze kitu! Pia unatakiwa ujue kuwa visa vya vijana kuishia kwenye Poda na Kupata UKIMWI Sauzi ni vingi. Pia jifunze kuwa muungwana acha matusi.
Hiko sio kisa, huo ni umama, kisa toa chako wewe, kuja hapa kusema mshkaji wako ana HIV mara teja, hayatuhusu. Wewe eleze ni mji gani una fursa nyingi kulinganisha na aliyoitaja yy na zaidi unaweza mtajia mji mwingine tofauti na anayoihitaji yy kama nyongeza.

Acha umama.
 
Hili nalo bwabwa daah jamii sasa hivi mabwabwa yamejaa,naona mnataka kwenda kutafuta mabwana wapya,ok kazi kwenu maana kule wamejaa wengi kama nyie,tanzania hatutaki mabwabwa naona mnakimbilia South,eti nawe umekaa bondeni hadithi za masikani zinawachanganya vitoto vya sasa hiv
Hivi mbona unateseka sana wakati tunaoenda ni sisi!!!
 
Daaaa ttz wabingo c waaminifuu ukishapewa dili uko south amkawii kuharibuu,ningekuunganisha na mwanangu mmoja yupo south anafanyaa dili la kuuza magazeti Yale yalishasomwa anayafata kiwandan na kuyaleta mpkn mwa nchi zilizopakana na south nakuyauzaa kwa jumla ....
 
Hiko sio kisa, huo ni umama, kisa toa chako wewe, kuja hapa kusema mshkaji wako ana HIV mara teja, hayatuhusu. Wewe eleze ni mji gani una fursa nyingi kulinganisha na aliyoitaja yy na zaidi unaweza mtajia mji mwingine tofauti na anayoihitaji yy kama nyongeza.

Acha umama.

Mbona kama kisa cha HIV kama kinakugusa sana? Unataka tumwambia huyu "Baharia" mwenzetu habari "Johannesburg Stock exchange" wakati anaenda "kutafuta maisha". 😂
 
Johannesburg kazi unayoweza kufanya inatakiwa uende wanakotengeneza magari uwe unaweza umeme wa magari kupaka rangi vizuri na kunyoosha body maana wageni wengi wanafanya kazi ya kununua gari zilizogongwa na kupeleka kunyoosha Jeepe street ukiwa sawa kwenye hizo fani hasa kupaka rangi utagombewa...ishu ya kuuza vitu mtaani haipo hao Metro wanakamata sana na pia ili uende sawa na document zako ukifika Messina unaomba wakugongee siku 90 hata kwa rushwa ndani ya hizo siku utakua umepata deal la kufanya.. wanaojihusisha na gereji za magari ni Watanzania na Warundi hao mataifa ya magharibi hautaenda nao sawa hata kama haujui huko utapewa kazi ya msasa kusafisha bodi ukiweza unajifunza rangi hiyo ndio inawatoa vijana wengi wanaotafuta maisha...maeneo ya Mabonenng kule na mbele ya Jeepe street au Commissioner ndio mambo ya ufundi na Watanzania utawakuta huko zipo gereji kibao za kina Baba Sofia na wengineo na ukifika hapo ukiomba kazi unapewa na maisha yataendelea ila kwa Johannesburg usijihusishe na vitu au kazi ya tamaa sijui kuiba,unga au majani utaambiwa kutoka Swazi jua utapotea maana Polisi wakijua mgeni wengi wanauawa labda mtuhumiwa awe na pesa...na hilo Jiji usipende kutembea usiku ukitoka job nenda home usiku una mambo mengi sana hao polisi wenyewe wanageuka wazee wa mishe na pia ishu ya kutunza hela kuwa msiri sana sio unatangaza nina kiasi fulani vijana wa kazi watatumwa kuja kuzichukua all in all kazi salama zipo ukiwa na fani yako kama huna fani labda ukajifunze kule kwa gharama ya kutumikiswa tuu mpaka ujue...Karibu Gauteng Province..
 
Hapa hapa kwa nyerere,ya nini niende ulaya,sijui hata misele ya huko,kuishi kama dikidiki kwenye msitu wa simba mimi siwezi, zamani palikuwa panaishu huko sio sasa hivi binadamu wametengeneza roho mbaya,nisije bure nikatolewa bandana na Figo yangu,ugali wa mlenda na daga wa mwanza nitawapati wapi nikienda huko,daah eti nikabebe maboks,mara town kuuza vinywaji kwenye magari mmhhh nani anataka maisha ya kiwaki hivyoo,naseti mipango na toboa hapa hapa bongo,mbona wazazi wangu wamenilea vinzuri bila ya kwenda South??hauna ndugu wala jamaa sindo unaenda kuwa bwabwa 🤭🤭🤭
Wewe Ni jinsia gani ?Samahani tuanzie hapo
 
Cape Town ni jiji la kitalii hasa huko Water Front na Camps bay watu wengi waliopo kule kwa miaka ya karibuni wanajishughulisha na viduka vidogo vidogo kazi za hotel,kuuza mafuta garage na security ingawaje hii kazi ina hatari sana huko Cape Town warangi rangi wanaishi kwa kuiba kwenye maghara tena kwa kuvzmia na siraha nzito wakiiba chochote wao sawa tuu palikua na kazi kule Docks za Meli pale pale hazard maline,globe na wengineo sema nao wenyeji wana njaa imekua vita kugombaniana ndio maana wageni wanajikita kwenye kazi za kujiajiri na pia wanasimamia sana mtu atakaeajiriwa ishu ya working permit iwe sawa tofauti na miaka ya nyuma...Mitchels Plain,Gugulethu Mandalay na Khayelitsha ndio maeneo wanayoishi wageni wengi hasa Watanzania hapo Kroos road maeneo ya Phillip pana Mbongo toka miaka hiyo wanamwita Shabby na huko huko wapo wakina Ally Kichwa ila kukupokea mpaka wapewe taarifa kutoka kwa mtu wanaemfahamu ila kwa kuishi Cape ni kugumu kuliko Jozi kutokana mishe zipo mbali na maeneo ya makazi inabidi uwe na nauli ya kutosha wakati Jobeq unaweza kukaa nyumba za mjini na ukatembea kwenda kwenye misele ya kazi yako...
 
Pretoria mishe za maisha zipo Jacob marley Sunside na mitaa ya Brown huko hilo Jiji kwa sasa hivi nadhani ndio jiji gumu kutafuta hela kuliko hayo mengine kutokana na mzunguko wa pesa upo chini harafu kodi ya nyumba haishuki na polisi wanawajua wageni karibu wengi mishe zao wao ni kwenda kuchukua hela kila wanapojisikia na wengi wanafanya kazi za kunyoa saloon zinazomilikiwa na Watanzania na Waghana...na pia wengine wanapewa Pick up kwa kupeleka hela kila wiki nayo hii mpaka uwe unaujua mji na pia usalama wa kuibiwa hiyo gari upo nje nje wakati wowote wanaichukua wezi..hii ishu ya kuendesha magari hata Jozi ipo pia...wengi waliopo hasa Jozi ni kuwa wao wanatafuta machimbo ya vitu bei rahisi harafu anatuma Tanzania kwa matruck ya Watanzania wakimuuzia anatumiwa hela hii nayo inataka uwe na mtu kweli huko daslm...maana vitu vya bei nzuri vingi vipo Dragon,China City,China Mall,Macro,Cash and Carry na kwingineko ni wewe kuumiza kichwa kisilale hii kazi inataka uwe na mtaji hata wa 2m hivi kila Truck ikiondoka inakua na mzigo wako wowote...
 
Daaaa ttz wabingo c waaminifuu ukishapewa dili uko south amkawii kuharibuu,ningekuunganisha na mwanangu mmoja yupo south anafanyaa dili la kuuza magazeti Yale yalishasomwa anayafata kiwandan na kuyaleta mpkn mwa nchi zilizopakana na south nakuyauzaa kwa jumla ....
Usijali mkuu....kama ikiwezekana sawa kama isipowezekana sio mbaya...Mungu ndiye mpangaji wa riziki...ni suala la muda tu
 
Halafu nilisahau kumwita [mention]Isanga family [/mention] afadhali umejitokeza kutoa muongozo Ndagha mwalafyale, Ndagha sana nadhani mwamba amepata muongozo mzuri nakazia uhalifu haulipi
"Crime does not pay"...yah...alisema Lucky Dube piaa....na hai apply kwa south africa tu hata wewe uliyeamua kutafutia riziki Tanzania pekee inakuhusu....
 
Pretoria mishe za maisha zipo Jacob marley Sunside na mitaa ya Brown huko hilo Jiji kwa sasa hivi nadhani ndio jiji gumu kutafuta hela kuliko hayo mengine kutokana na mzunguko wa pesa upo chini harafu kodi ya nyumba haishuki na polisi wanawajua wageni karibu wengi mishe zao wao ni kwenda kuchukua hela kila wanapojisikia na wengi wanafanya kazi za kunyoa saloon zinazomilikiwa na Watanzania na Waghana...na pia wengine wanapewa Pick up kwa kupeleka hela kila wiki nayo hii mpaka uwe unaujua mji na pia usalama wa kuibiwa hiyo gari upo nje nje wakati wowote wanaichukua wezi..hii ishu ya kuendesha magari hata Jozi ipo pia...wengi waliopo hasa Jozi ni kuwa wao wanatafuta machimbo ya vitu bei rahisi harafu anatuma Tanzania kwa matruck ya Watanzania wakimuuzia anatumiwa hela hii nayo inataka uwe na mtu kweli huko daslm...maana vitu vya bei nzuri vingi vipo Dragon,China City,China Mall,Macro,Cash and Carry na kwingineko ni wewe kuumiza kichwa kisilale hii kazi inataka uwe na mtaji hata wa 2m hivi kila Truck ikiondoka inakua na mzigo wako wowote...
Aha wazo zuri mkuu...ntalifanyia utafiti nikifika
 
Back
Top Bottom