Charlie Luciano
Member
- Sep 15, 2022
- 12
- 36
Nakukubali sana mwamba kimtazamo nakufananisha na malemaNaenda mazoezini ntakuja kukupa mrejesho wa sehemu zote maisha ni kuhangaika na kuangalia fursa zako zipo wapi na ikiwezekana kukueleza sehemu sahihi ya kwenda au ukiwa huko ufanye nini au kabla ya kwenda ujiandae na nini?
Johannesburg kazi unayoweza kufanya inatakiwa uende wanakotengeneza magari uwe unaweza umeme wa magari kupaka rangi vizuri na kunyoosha body maana wageni wengi wanafanya kazi ya kununua gari zilizogongwa na kupeleka kunyoosha Jeepe street ukiwa sawa kwenye hizo fani hasa kupaka rangi utagombewa...ishu ya kuuza vitu mtaani haipo hao Metro wanakamata sana na pia ili uende sawa na document zako ukifika Messina unaomba wakugongee siku 90 hata kwa rushwa ndani ya hizo siku utakua umepata deal la kufanya.. wanaojihusisha na gereji za magari ni Watanzania na Warundi hao mataifa ya magharibi hautaenda nao sawa hata kama haujui huko utapewa kazi ya msasa kusafisha bodi ukiweza unajifunza rangi hiyo ndio inawatoa vijana wengi wanaotafuta maisha...maeneo ya Mabonenng kule na mbele ya Jeepe street au Commissioner ndio mambo ya ufundi na Watanzania utawakuta huko zipo gereji kibao za kina Baba Sofia na wengineo na ukifika hapo ukiomba kazi unapewa na maisha yataendelea ila kwa Johannesburg usijihusishe na vitu au kazi ya tamaa sijui kuiba,unga au majani utaambiwa kutoka Swazi jua utapotea maana Polisi wakijua mgeni wengi wanauawa labda mtuhumiwa awe na pesa...na hilo Jiji usipende kutembea usiku ukitoka job nenda home usiku una mambo mengi sana hao polisi wenyewe wanageuka wazee wa mishe na pia ishu ya kutunza hela kuwa msiri sana sio unatangaza nina kiasi fulani vijana wa kazi watatumwa kuja kuzichukua all in all kazi salama zipo ukiwa na fani yako kama huna fani labda ukajifunze kule kwa gharama ya kutumikiswa tuu mpaka ujue...Karibu Gauteng Province..
Sehemu gani yenye zero risk, yaani isiyo na risk hapa duniani unaeza safiri ama ambayo unapenda.Mimi pia huwa napenda kusafiri mkuu ila sehemu zenye risks kubwa za waziwazi sikanyagi aisee,hiyo inakuwa ni kulazimisha ili mradi tu uonekane uko nje ya nchi.
Nicheki Pm mkuu nikutumie picha za magari na bei zake hapa uzi wa mtu anatafuta sehemu ya kufikia harafu tutume picha za Range sio sawa..Sorry mkuu .hivi yale ma Range kama ya kajala yameindikwa GP hadi nalishika mkononi tz inaweza kuwa sh ngapi.naulizia Mpya au Used
Ujumbe kwao tafadhali.Salamu za kwanza kwa wanaochangia kwenye uzi wangu kabla ya kuusoma vizuri na kujua nini nataka
Salamu za pili kwa wanaofikiri kuwa kisa baadhi ya watanzania walipata/wanapata shida SA basi by default Ina apply kwa watanzania wote
Salamu za tatu kwa watoto wa kiume wote wanaojikita kuongelea hatari hatari hatari za SA kama vile wananionea huruma sana kana kwamba nikibaki bongo sitakufa au kupata tabu yoyote au watanisaidia chochote kwenye maisha yangu....
Asante kwa mtazamo wako,watu kama nyie najua mpo ndo maana nilishaelezea mapema kwenye uzi kuhusu hili la mtazamo.... kwahiyo usijalikijana wa hovyo anaeona aibu kuuza vitu mtaani kwake na kwenda nchi za wenzake akidhani kuna urahisi wa maisha[emoji38][emoji38][emoji38]
nyie ndo mnabanduliwaga mkifika nchi za wenzenu
Aha fresh mkuu haina nomaaMzee cape town ngumu kidogo kwa mgeni, Pretoria na jo'burg zinafanana kidogo, so jaribu jo'burg
Risks za sehemu nyingine zitakudhuru kama ukizitafuta mwenyewe,lakini risks za South Africa zinakufuata hata kama huna hatia tofautisha hapo ndugu.Sehemu gani yenye zero risk, yaani isiyo na risk hapa duniani unaeza safiri ama ambayo unapenda.
Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
Sawa jifanye mbishi nenda huko sauzi Waka kumwakwelekwele.Kama point ni kifo bro...."Death is inevitable" popote unakufa tu....hata states watu wanakufa sana tuu!!
Afu mimi na wewe yaan tumepishana[emoji4][emoji4] mimi natamani nikipata ndo niende states ku enjoy....af wewe unataka ukatafute states ukipata urudi ku enjoy SA sehemu ambayo tayari umesema imejaa ujambazi [emoji23][emoji23][emoji1373][emoji1373][emoji1373]
Hii ndicho nilichomwambia jamaa leta uziRisks za sehemu nyingine zitakudhuru kama ukizitafuta mwenyewe,lakini risks za South Africa zinakufuata hata kama huna hatia tofautisha hapo ndugu.
South Africa unatoka ndani kwako kwenda dukani tu wazee wa kazi wanavamia silaha za moto yeyote watakayemkuta mbele yao ni halali yao hawaangalii una hela au huna hela wanakuwashia za moto,unatembea na simu ya laki 3 mtaani wenyeji wanakusimamisha wanakupora na kukuchapa na mapanga bila kosa lolote sasa hayo ni maisha gani
OkaySawa jifanye mbishi nenda huko sauzi Waka kumwakwelekwele.
Hatukukatazi.
Safari moja huanzisha nyingine.... bytheway unataka kwenda US kwa njia ipi?? Halali ama kuzamia???Mkuu twende U.S bora south utaenda chezea shaba kizembe sna
before haujaenda s.a eb kwanza zama you tube andika " KUTOKA UGHAIBUNI " sikiliza kwanza story za wana uko kiwanjani zikoje ukihisi unaziweza basi nakushauri nenda ila kama hauziwezi stay home jigga.Wakuu heshima zenu.
Moja kwa moja kwenye mada husika.
Nataka kwenda South Africa kujaribu bahati yangu huko pia,maana uwanja wa nyumbani naona maji yananizidi kina kila uchwao...simaanishi kwamba nimejaribu kila kitu hapa nyumbani bongo "hapana" ,ila kuna baadhi ya vitu ambavyo huwa wanaume tunavifanya pale tunapokuwa desperate kuelekea the point of hitting-the-rock-bottom kwaajili ya kupata chochote kitu...sasa kusema ule ukweli siwezi kuvifanya hapa nyumbani(na hii ni kwasababu zangu binafsi ambazo kwako huenda ukaona ni sababu za kipuuzi,ila utofauti huu wa kimtazamo ndio sifa moja ya binadamu kamili right?)....
Sasa baadhi ya vitu ambavyo nipo tayari kuvifanya nje na sio hapa nyumbani ni kama kubeba mizigo bandarini/viwandani,kuuza vitu kwenye traffic jam,kutembeza bidhaa kitaa(street vendoring),....nk nahisi ushapata picha nini namaanisha.
Sasa kati ya nchi zote nimeichagua south africa sababu ya diversity ya hustlers waliopo kule, sasa shida ni kwamba siyajui kiundani majiji haya matatu Capetown, Pretoria na Johannesburg.
Hivo kwa mwenye kujua au anayeishi katika moja ya majiji hayo naomba kujuzwa taarifa za msingi kuhusu majiji haya matatu.
Asante.
"We're born to suffer"
Lucky Dube
Kama ni hivyo kusingekuwa na wageni kabisa SA..... anyways wewe point yako haswa ni ipi???? Maana mimi ninachotaka kujua niende Pretoria/Capetown/Johannesburg??? BasiiRisks za sehemu nyingine zitakudhuru kama ukizitafuta mwenyewe,lakini risks za South Africa zinakufuata hata kama huna hatia tofautisha hapo ndugu.
South Africa unatoka ndani kwako kwenda dukani tu wazee wa kazi wanavamia silaha za moto yeyote watakayemkuta mbele yao ni halali yao hawaangalii una hela au huna hela wanakuwashia za moto,unatembea na simu ya laki 3 mtaani wenyeji wanakusimamisha wanakupora na kukuchapa na mapanga bila kosa lolote sasa hayo ni maisha gani