Niezeke bati la kiwanda gani kati ya Alaf na Sunshare?

Usiezeke na bati kabisa. Kuna ujenzi aina mpya umeanzishwa Tanzania na mzee wa Madrassa, hauna haja ya bati na nafasi yote ya kuezeka bati unapata kuitumia.
Tupe elimu na ufafanuzi juu ya huu ujenzi ili nasi tunufaike mkuu.
 
Tupe elimu na ufafanuzi juu ya huu ujenzi ili nasi tunufaike mkuu.
Nakushaauri uwasiliane na mtaalam wa huo ujenzi, anajitangaza sana humu na ameweka namba za kuwasiliana nae kwa whats app, anaitwa Abdul Ghafur 0625249605
 
Wewe ndio umeharibu kabisa? Kwahiyo kama uzito wa slabs na tofali waweza kuhimilika, ndio tuongezee mzigo mwingine bila ulazima wowote? Inaelekea hujui hesabu za kujumlisha na kutoa. Halafu unatuletea mambo ya mahesabu ya mainjinia kama vile hujui ujenzi wa watanzania walio wengi ulivyo. Kifupi jamaa kachambua kimantiki na kitaalamu kabisa. Ulichofanya wewe ni uvurugaji wa hoja.
 
Nakushaauri uwasiliane na mtaalam wa huo ujenzi, anajitangaza sana humu na ameweka namba za kuwasiliana nae kwa whats app, anaitwa Abdul Ghafur 0625249605
Tuelezee wewe jinsi unavyojua kutokana na maelezo yao tuyapime hapa. Haya mambo ya ku-refer naona kama ni ukanjanja tu.
 
Wewe ndio umeharibu kabisa? Kwahiyo kama uzito wa slabs na tofali waweza kuhimilika, ndio tuongezee mzigo mwingine bila ulazima wowote?

Mwisho wa siku utauliza "kwa hiyo kama uzito wa slab na tofali unaweza himilika ndio tuongeze uzito nondo?"...
 
Yaani mama sikunyengine nenda tu pale Sunshare moja Kwa moja patana mwenyewe unasubiria bati Zako unaondoka hakuna cha Alaf wala mnyama Simba.

Kikubwa nikuhakikisha bati umenunua kiwandani mwenyewe hapo Sunshare ni madhubuti mno fundi wala hajakundanganya nimeezeka Chanika Taliani mwaka wa 7 halijapauka mvua ikipiga ndo yanazidi kung'aa kama limepauliwa Leo Ila ndo ivo ushafanya maamuzi usibabaike na majina.
 
Tuelezee wewe jinsi unavyojua kutokana na maelezo yao tuyapime hapa. Haya mambo ya ku-refer naona kama ni ukanjanja tu.
Una haki ya kuona vyovyote uonavyo baada ya kufanya tafiti japo ndogo. Bila tafiti utabaki kuwa wewe kanjanja.

Wasilaiana nao, nimeweka namba zao juu hapo, na wamo humu JF. Kama huwezi, mimi siwezi kukusaidia zaidi ya kukupa mawasiliano nao. Tatizo nini?
 
Tuelezee wewe jinsi unavyojua kutokana na maelezo yao tuyapime hapa. Haya mambo ya ku-refer naona kama ni ukanjanja tu.
Hajafanya vibaya kukuelekeza kwetu. Tupo hapa JF na namba alizokupa ni zangu binafsi.

Nadhani Umewahi kusikia kuwa siku hizi Tanzania watu wanaezeka kwa mtindo ambao bati halionekani. Sisi tumeenda mbali na kisasa zaidi ya bati kutoonekana. Tunaunda (precast) vifaa maalum vya zege kwenye kiwanda chetu kidogo hapa Misugusugu, Kibaha. Pia tuna uwezo wa kuundà vifaa hivyo site ya mteja ili kupunguza gharama za usafirishaji vifaa.

Vifaa hivyo (slabs) vinakua mbadala wa bati na mbadala wa gypsum boards kwa pamoja.

Kwa vifaa hivyo Unapunguza gharama za kuezeka kwa bati, zinapunguza gharama za.mbao za bati, zinapunguza gharama za gypsum boards na mbao zake. Pia utapata nafasi juu ya kufanya chochote upendacho. Tuna supply vifaa na pia tuna mafundi wazoefu.

Programme yetu inaitwa Abraar Bricks Nyumba kwa wote. Ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa whatsqpp 0625249605.

Pia tunaweza kukujibu hapa swali lolote ulilonalo.

Karibu sana.
 
Ningeonapo kapicha ka nyumba iliyopauliwa kwa mtindo huo ningeweza kuhamasika zaidi,nina nyumba ya kupaua nakusanya nguvu
 
Kupauka kwa bati hakutegemei imetengenezwa wapi. Angalia specs . Omicron ni kipimo muhimu kwenye Kupauka kwa rangi. Kinacho wabeba ALAF ni brand na siyo ubora. Ando na Sunshare wana quality bora. Ask ALAF to give you a written guarantee ya hate miaka mitano. Kama hela ipo nenda Nabaki Decra.
 
kapicha mzee Ghafur
 
Ujengewe sanamu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…