Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Ni vema na mtalakishwa naye akaleta uthibitisho hapa juu ya ukubali wake kwenye uamzi wenu ili yule jamaa wa 40yrs aliyejipambanua hapa kuwa sasa ameamua kuwa mwaka kesho ataoa basi awe huru kuwasilisha fomu za maombi ya nafasi ya kuishi moyoni mwako bila wasiwasi.
 
Back
Top Bottom