Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Mkuu nimekusoma uzuri na umejieleza uzuri sana. Mimi ni mfanyabiashara na napenda kuinvest vijipesa vidogo vidogo sehemu nyingi na kupata small return. Target yako ya kuinvest 1M na upate return ya 80% per month, though from up to a six month period, its 99.99% impossible. Unless iwe ni biashara haramu!
 
Haramu ukitusua mara moja achana nayo usije somewa ramani.
 
Nipo Dodoma, ni mfanyakaz pia. Nimekodi greenhouse, nimelima nyanya ya aina ndefu inaitwa Uwezo F1, kila alhamis ya kila wèek navuna kila zisizopungua 250, kila kwa sasa ni 1000 kwa wasambazaji wa hotels km Dodoma Carnival, Dodoma hotel na Fantasy village.
Karibu kwenye fursa ya kilimo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unalimia dodoma wapi kiongozi...
 
Boda boda labda aendeshe mwenyewe boss


Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu BodaBoda zote unazoziona mtaani zinaendeshwa na wenyewe? Kama sio kwanini sasa bado zipo zinatembea? Inamaana wamiliki wanadhulumiwa? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Biashara yoyote ile inahitaji Umakini,ukishakuwa makini mfatiliaji hakuna kitakachoharibika


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu kwenye Apps (Application) watu wanapiga elaa sana sikuizi, ningekushauri uangalie upande huo, watu wanapiga zaidi ya dollar 1000 kwa mwezi. Kama ukihitaji kujua zaidi kuhusu application nitafute hapa kiongozi 0692941440
Apps gani? Viewer wa Youtube au ndio zile ngonjera za Ad-sense
 

Yani we ndiyo hujui kabisa.....Supu ya Pweza huwa inapendeza kwenye mazingira ya hovyohovyo...pale ndipo watu wanapiga pesa....nenda pale kwa Msisiri uone jamaa anavyopiga pesa ukilinganisha na mazingira yake
 
Hujaeleza gharama na changamoto ulizopitia mkuu....maelezo yako yamekaa kichai chai
 
nENDA
Nenda Q-net
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…