Nifanye nini kufuta kumbukumbu za matukio mabaya kwa watoto wangu?

Kwahiyo asingekufukuza ungeendelea kuvumilia kipigo!![emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Bahati mbaya hiyo haitokaa ifutike kamwee, ni kama kuchora tatoo. Hiyo ni kumbukumbu ya kudumu kwenye maisha yao. Wewe cha msingi sasa ni kuanza kuzungumza nao kuhusu na kuwaonyesha upendo. Waonyeshe madhara ya ulichopitia na kama ni wa kiume wasije kuwa kama baba yao na kama ni wa kike wasijevumilia kipigo.
 
kasome uzi wa Mwasapile

akivurugwa na mchepuko hasira anaenda kumalizia kwa mke na watoto

sasa hapo sijui na mke wa mwasapile alikuwa anachepuka
 
Kwa nini unawafundisha watoto kuwa baba anayempiga mama ni baba mzuri,,acha kuwafundisha hivyo wao wameona na wanajua kuwa siyo vizuri.Ila watasahau wakikua
 
Hivi nyie hamkuwa watoto? Baba yako anampiga mama yako anavimba uso ukiwa na miaka 5,6,7, 8... halafu usahau? Kama una akili ya kawaida ya binadamu, hauwezi kusahau. Unaweza kupotezea tu lakini siyo kusahau. Wapo pia wasioweza kupotezea. Wanakuwa maadui mpaka kifo.
Kwa nini unawafundisha watoto kuwa baba anayempiga mama ni baba mzuri,,acha kuwafundisha hivyo wao wameona na wanajua kuwa siyo vizuri.Ila watasahau wakikua
 
Pole sana kwa hayo ila kwakuwa watoto walikuwa wanashuhudia hayo yote, ni vigumu sana kuwaaminisha kitu kingine mbali na uhalisia.

Haujachelewa hao wanao acha waamini kile wanachoamini mpaka utakapoona sasa ni watu wazima au tayari wanajielewa zaidi, wakumbushe uhalisia wote ila waeleze after all ni baba yao so wamsamehe na kuendelea na mambo mengine.

Stop stop kuwaaminisha kisicho unaweza sababisha tatizo lingine.

Ushauri tu

TEKERI.
 
Pole.Ila siungi mkono watoto kuitwa jina la baba mpya mana wa kwanza hajawakataa.Kukubali hilo manake watoto ndiyo umetaka wakuongoze ktk maamuzi kitu ambacho kitaleta mtafaruku badaye mana hujawaasili kisheri(kurasimisha kwa baba mpya).Kingine ulipaswa kuchukuwa hatua za kisaikolojia kwa watoto.
 
Sasa huyo mwanamke mwingine amemuoa?
 
Kwani umeambiwa mtoa mada anataka kuwapa jina la baba wa kambo? Kasome tena...
 
Mm mwenyew nilishi maisha Kama ya hao wanao HV mzee wangu r.i.p alikuwa mtata San yaani nilimuona Mara kibao mzee wangu akimpiga maza na matuzi juu kwa juu .nilishaingilia kati lkn wapi tuliishiwa kupigwa wote mm na dad angu na mdg wetu tunabaki tunalia tu na mam pia mzee alipiga aise siyo utani kiliniumiza sna Kuna wakt nilianza kuvuta bangi ili niweze kupamabana na ukatili wa mzee wangu lkn wapi nilipigwa Zaid na ukatili ulizid wa mzee

Nilisha muona mam angu akikunnja nguo tayari kwenda kwao duh tulilia sna tukaenda kumuomba mzew mtu mzima aje amzuie mam asiondoke Hapo mzee Alisha sema aondoke ataki kumuona hapa

Mzee wetu alikuja kupunguza ukorofi around 2006 HV tayari kak zangu wako vyio vikuu na sis Yuko secondary

Automatically mzee alikuja San kurejesha upendo kwetu na kutuambia kuwa tuungane na tupendane San na kumjali mam yetu
Sijui pepo la ukorofi alilipata wapi mnk mama anasema hi tabia hajawia kuona

Mama alisema alichelewa San kupata watot alikaa miaka 6 Bila kuwa na watot na mzee alimvumilia sna bila kumnyanyaza Wala kutak kuoa Tena pmj na kushinikizwa na bb kuwa aoe mke mwingine sas anashanga mbna kabadili katikat hapo tulishangilia sna na kushangazwa kwa ukorofi wa mzee wetu wa gafla

Mpk mzee wetu anakuja kufariki aise alikuwa na upendo mkubwa sna kwetu ss na kutuasa kupendana na kumjali mama na ss pia tulimpenda Sana Bab yetu mno kwa jins alivyokuwa anatumbambania

Pole sana kwako huwenda Bab yule atabadilika sikutegemea mzee wangu kuja kubadilika na kurudisha upendo kwetu ss na kutupa kila kitu na elimu pia
 
Waache wakikua kila mtu na akili zake kichwani, huwezi futa hizo kumbukumbu kichwani mwao kilichobaki ni kika mtu atahukumu anavyoona sahihi.
 
Big up Sana.. nimependa ulivyo mjibu.. congratulations for such wisert you have in case of giving someone's counseling.
 
Maana ya kusahau hapa siyo kupoteza kumbukumbu ni ile waswahili wanasema "Yaliyopita sii ndwele tugange yajayo"
 
Ni ngumu hao watoto kusahau my dear..kikubwa wewe walee tu kwenye misingi mizuri mengine muachie Mungu..nilipita huko sijawahi sahau hata moja.
 
Hivi kuna mwanaume mwenye akili timamu anaweza kumpiga mkewe bila sababu yeyote!?, yaani unafika tu nyumbani unaanza kumpiga mke wako?!,labda mwanaume huyo awe na matatizo ya akili lkn kinyume na hapo Hapana,wanawake huwa wanajifanya innocent sana lakini ndio chanzo cha matatizo yote
 
Kiukweli wanaume sijui tuwaelimishe mpaka lini ili muelewe kuwa ikiwa mwanamke ni chanzo cha matatizo suluhisho lake si kupigwa. Kuna wanawake ni vimeo tena vimeo kweli kweli sitaki hata kuwatetea, ila unachotakiwa kufahamu ni implications unazozizalisha katika kumpiga, kumbuka huyo mwanamke ambaye ni kimeo ni MAMA wa mtu mwingine, unapompiga madhara hayabaki kwake tu yanaenda hadi kwa wale wote wanaomuhusu, (watoto wake, ndugu zake, marafiki zake etc).

Sasa turudi kwako mr. muadabishaji kama una mama utajisikiaje kumuona anapigwa na baba yako kwa kile kinachoitwa chanzo cha matatizo? Tujaribu kutokuongea lugha ya ubinafsi katika hili. Usiongee as if duniani uko pekeako na hauhusiani na mtu yeyote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…