Unaweza nitajia sababu zinazo mpa mwanaume uhalali wa kumpiga mkewe??Wewe ni mkorofi sana. Haiwezekani mme akupige pasipo sababu na kuishi na watoto wako lazima utawaambukiza tabia yako ya hovyo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaweza nitajia sababu zinazo mpa mwanaume uhalali wa kumpiga mkewe??Wewe ni mkorofi sana. Haiwezekani mme akupige pasipo sababu na kuishi na watoto wako lazima utawaambukiza tabia yako ya hovyo.
Acheni kumsema vibaya kama vile ninyi mnaishi sayari nyingine kwamba ayo matukio ya wanawake kupigwa pasipo kosa hamuyaoni.Wewe ni mkorofi sana. Haiwezekani mme akupige pasipo sababu na kuishi na watoto wako lazima utawaambukiza tabia yako ya hovyo.
Uonavyo msimbe, ni sahihi. Siwezi oingaKuchepuka ndo unipige mpk uniue?? NONSENSE
I think I love youNikwambie tu ukweli...HAWATOSAHAU....mimi nakumbuka matukio ya toka nikiwa darasa la 1..2..3 ya wazazi wangu...now nna 36 years sisahau na sitosahau..japo simchukii mzaz wangu ila matendo siyasahau.....
Never ever...na wala sihitaj kulishwa maneno..ni kwamba niliona kwa macho...picha zipo kichwan
1. UkorofiUnaweza nitajia sababu zinazo mpa mwanaume uhalali wa kumpiga mkewe??
Ukimpiga akakupeleka mahakamani unahisi hivyo ulivyovitaja vitasimama kama utetezi wako?1. Ukorofi
2. Umalaya
3. Kidomodomo
4. Uchafu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Pole sana, kwa nini mnapigana?
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana, sasa wanapigania nini...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah! Mkuu huwa unaniacha hoi na comments zako, ni fupi halafu unavyo comment ni kama vile unahimiza watoto wadogo, mfano:
Pole sana, kwanini mnapigana?
Ngoja waje kukupa mwongozo!
Usirudie kumkaripia mtoto mdogo!
Dah! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Pole sana mkuuSalaam wakuu
Miaka michache iliyopita nilipitia mambo mengi kwenye ndoa ambayo nikiri kuwa hayakuwa mazuri kwa ukuaji wa watoto wetu kisaikolojia.
Watoto walishuhudia nikipigwa mara nyingi sana, nikitukanwa au kusemwa vibaya. Na hata kuna wakati ugomvi ukitokea chumbani walikuwa wanakuja kusikiliza mlangoni kwetu na kujua ndani kuna ugomvi au kusikia kilio na milio ya makofi na mangumi. Na pia walikuwa wanaona nikiwa nimevimba uso macho au michubuko iliyotokana na vipigo. Na mara kadhaa kama mlango haukufungwa walikuwa wakiingia chumbani kunitetea ili nisiumizwe zaidi.
Hawana umri mkubwa wote watatu bado wako shule za msingi. Mara nyingi walikuwa wakiona baba yao akifika tu na upepo wa ndani unabadilika kama sio wao kupigwa basi ni mama maana alikuwa mkali sana kwa watoto na kwangu.
Nilianza kuhisi tatizo kwao kipindi ambacho bado tupo pamoja hatujaachana. Siku moja mwanangu aliniuliza swali, MAMA KWANINI TUSIENDE KWA BIBI ILI BABA ASIKUUE? ( Kauli kubwa wakati akinipiga alikuwa anasema IPO SIKU NITAKUUA) na watoto walikuwa wanasikia hivyo kuoata hofu ya mimi kuuawa siku moja. Nikaamua kuongea na baba yao kuhusu swala hilo kuwa watoto wanahofu aache kunipiga ila akajibu nimewajaza sumu kuwa baba yao mbaya nk ioa sijawahi fanya hivyo na ukatokea ugomvi akanipiga na kunifukiza kabisa ili nisimwqribie watoto wake.
Japo baadaye niliwapata watoto na kuanza kuishi nao maana tangu hapo tuliachana moja kwa moja na sasa naishi maisha mengine. Ila tatizo limebaki owa watoto kioa mara wanaomhelea jinsi nilivyopigwa na yote.
Mnaweza kuwa mmekaa unaona mtu anasema mama bora tulivyokuja huku hata hupigwi tena, au wala sisi hatupigwi tena nk najaribu kuwaambia baba yenu anawapemda, ni mtu mzuri nk ila hawaeleqi na wananibishia na kumfananisha na monster wa kwenye movie. Binafsi siongelei chochote kibaya kwao ioa wao hawasahau katu. Na hata akipiga simu kutaka kuwasalimia hawakubali hadi nakata siki, nikimwambia hawataki ananilaumu kuwa wqnajaza sumu kitu ambacho sifanyi.
Naandika haya nikiwa nimeshajitahidi kufanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja kuwaamisha kwamba baba yao ni mtu mwema, na anawapenda ila hawakubali.
Binafsi nilishaolewa, sasa wanampenda baba yao mpya na wanasemq ndio baba yao na si yule mwingine( huwa wanamwambia wao wakiwa wanapiga naye stori, wanamwambia shule waitwe fulani bin jina la baba mpya) hataki kusikia kuhusu baba yao kabisa.
Je, hii inaweza saidika kifuta hizi kumbukumbh au niwaache tu walivyo?
Nimesoma huu uzi na nimegundua watu wengi humu wana Trauma lakini ni ngumu kujua na hawawezi kusema wazi lakini bado wanaumia kimyakimya.
Nashauri JamiiForums waanzishe jukwaa maalum la maswala ya afya ya akili tu, ushauri na matibabu na pia watu waweze kushare matatizo yao yanayohusu afya ya akili kama msongo wa mawazo, depression, anxiety na disorders nyingine.
Mtaokoa wengi wenye vidonda moyoni ukizingatia Tanzania haina mkazo kwenye maswala ya afya ya akili.
Maxence Melo