Nifanye nini kuhusu changamoto hii ya usaili?

Nifanye nini kuhusu changamoto hii ya usaili?

Umeshayakoroga alafu unaomba ushauri...hio ni cheating na unaweza kufungiwa kabisa...
Ulishindwa nin kwenda ofisini?
 
Wakati unaomba nafasi na ikakubali najua ulijiona mjanja sana na ukafurahi, ila umefanya upumbavu mkubwa sana na huwezi kutoboa mana jina lako halipo kwenye list yao bali wana jina la huyo jamaa mwenye akaunti.
 
Wewe jamaa wakikushika wanaweza kukuzingua.

Halafu system nay imeshindwa kuligundua hilo
System hawezi kujua hilo mana yenyewe imewekwa kugundua academic qualifications na sio majina na ndio mana siku ya usaili ndo wasimamizi wanafatilia khs mambo ya majina
 
Mkuu mbona kuna ukakasi. Iweje akaunti inasoma majina mengine na document zililzoaplodiwa ziwe na majina mengine halafu mtu aitwe kwenye usahili hili linawezekanaje??
Ndugu inawezekana waombaji wengi wanachoangalia cheti kinamuhuli wa mwanasheria imeisha hiyooo awaangalii majina na cheti yanafanana huo muda akuna .
Hapo ni lipu lipu tuonane kwenye vituo vya usahili
 
Uliwezaje kufanya kitu kama hiki ndugu? Kuna Mambo mengine ni miracle etii..vijana mna hekaheka sana[emoji23][emoji119]
Bila shaka muhusika ka graduate mwaka Jana bado mgeni mtaani ana mengi ya kujifunza.
 
Umeshafanya kosa Moja.Usije ukafanya kosa lingine ukaenda usahili yatakayokukuta utasimulia na wajukuu.
 
Niko shortlisted mkoa X ajira za afya changamoto ni kwamba akaunti yangu iligoma katika ku-apply ilikuwa inasema am not qualified, licha ya kuwapigia lkn hawakupokea kunitatulia iyo shida hivyo ikabidi nitumie akaunt ya mtu mwngne ku-apply japokuwa vyeti CV barua ni vyangu lkn jina linasoma lake maana ni akaunt yake kwaio ata jina lililowekwa ktk majina ya usaili ni lake ndo limetokea.

Naombeni msaada wa kiushauri zaidi; j,e niende kwenye usaili hivy hivy kama maelezo niwaelekeze mbele ya safari au nifanyeje wakuu.

Nawasilisha kwenu, asanteni.
We nenda tu. Kuna maajabu huko. Kuna wanaojaribu kuingia ktk akaunti zao waombe kazi inagoma kuwa vyeti vilishatumika. Ndio nakuambia hawa mafisadi wanatumia vyeti vya watu kuomba nafasi. Sasa wewe nenda ila fanya njia yoyote uende utumishi kabla ya interview. Watakuelewa. Na utagundua tatizo la kutoweza kufungua akaunti yako.
 
Wakati unaomba nafasi na ikakubali najua ulijiona mjanja sana na ukafurahi, ila umefanya upumbavu mkubwa sana na huwezi kutoboa mana jina lako halipo kwenye list yao bali wana jina la huyo jamaa mwenye akaunti.
Sasa huyo jamaa mwenye akaunti vyeti vinasoma jina lake ambalo limeitwa ktk usaili. Ina maana huko utumishi wanakubali majina tofauti ya mwombaji na vyeti? Kama ni hivyo ndio sababu waombaji wanakuta akaunti zao tayari zimetumika na vyeti vyao. Nenda utumishi utagundua mengi. Wanasema kama ulishawahi kuomba kazi mahali ukaacha nakala ya vyeti ndio watu wanatumia. Sasa hiyo namba yako ya form four ndio inayotumika.
 
No short cut in life.
Ungeomba msaada wa kitaalam ili utumie akaunti yako.

No point of return, na hivyo vyeti vyako vinaweza kufungiwa.
 
Nina wasi wasi hii story ni fictional yenye lengo la kujaribu kuverify kama hiki kitu kinawezekana. Nadhani hakiwezekani. Dont sweat.​
 
Back
Top Bottom