Nifanye nini kuhusu changamoto hii ya usaili?

Nifanye nini kuhusu changamoto hii ya usaili?

Umeshayakoroga alafu unaomba ushauri...hio ni cheating na unaweza kufungiwa kabisa...
Ulishindwa nin kwenda ofisini?
Kwasababu nilikuwa sijui zilipo apo awali saivi najua nitaenda uko jumatatu.
 
Inshort, hauna akili njema.
Presentation of any forgery certificate will be stated as breach of laws, consequence to disqualified.
Kuna kasehemu kwenye mfumo unatiki kabox kuonyesha unayopresent ni sahihi na kweli kabisa. Na utawajibika ikiwa tofauti. Akaunt jina lingine na vyeti ni vya mtu mwingine ukienda kwenye interview utatakiwa uwe na kitambulisho chako lakini utatakiwa kunote s/n kwenye list ili upewe namba mficho ya kufanyia mtihani. Utakamatika hapo. Na utumishi wapo serious sana na interview.

Kuna jamaa alikuja kwenye interview akiamini amebeba vyeti vyote kumbe kimojawapo amekisahau na amesafiri mbali. Hawakumruhusu kuingia ingawa alitoka dodoma mpaka morogoro.
Haya asante, hongera wewe mwenye akili njema
 
Wakati unaomba nafasi na ikakubali najua ulijiona mjanja sana na ukafurahi, ila umefanya upumbavu mkubwa sana na huwezi kutoboa mana jina lako halipo kwenye list yao bali wana jina la huyo jamaa mwenye akaunti.
Kutokujua
 
Hapa mkuu hebu tueleze vizuri maana ajira portal ukishajaaza ukafikia 70% unaaply! Tatizo lako lilikuwa ni ndogo sana maana sehemu ambapo ulikuwa unajichanganya ni kwenye program na categories kitu ambacho ulipaswa kukileta hata hapa jf wataalam tukusaidie! Maswali yangu kwako haya

1: unasemaje kuwa ulitumia accout ya rafiki yako je ulitumia email ya nani??? Je ulitumia nida ipi??? Maana nida yako tiyari ilishatumika kwenye account yako!

2: vyeti vyako wakati unappload wewe hukureview cv yako uone kuwa cv inasoma ya rafiki yako??? Maana hata picha naamini ilikuwa ya rafiki yako???

3: huyo rafiki yako ninashaka na yeye amekusaliti maana haya yote yanapofanyika lazima unapokea email ya kukujulisha kuwa umetuma maombi je hiyo email ilitumwa kwa nan?????

4: uliwezaje kuapply kwa rafiki yako yeye vyeti vyake alivifuta au ilikuaje?? Maana kwa hali yakawaida hiki kitu naona kama hakiwezekani mkuu!!


Mwisho: kitu kama hukijui uliza kwa wanaojua mkuu! Ulichokifanya kitu ambacho kinatia shaka hata elimu yako wewe na huyo rafiki yako! Cha kukusaidia ni kuitengeneza account yako ili kwa mwingine uombe lakini kwa sasa hiyo haiwezekani mkuu! Ulifanya mistake kubwa sana !!maana majina yako na vyeti ni vyitu viwili tofauti!! Aliyekusaliti ni rafiki yako!
1. Email yake na NIDA yake, jina lake limetokea kwa sababu NIDA yake ilitumika

2. Hakuwahi kufungua account na hajihusishi na masomo haya ya afya wala fans nyngne yoyote ni mwanakijiji tu wa mtaani mwenye nida namba na email ndo mana niliweza kufnya vyote ivyo na picha ni una upload ww mwenyewe so niliweza kuweka picha yangu

3. Kabla ya kufanya yote hayo nilimuomba na akanikubalia

4. No 2

Mwisho: Nimekuelewa sana mkuu, Asante ubarikiwe
 
Duuuuh pole kwa changamoto

1. Usiende kwenye huo usaili, wala huyo rafiki yako asiende.

2. Hakikisha vile vyeti unavifanyia mabadiliko, virudi vya muhusika, huyo rafiki yako.

3. Ukikwama, hakikisha unawapata ajira Portal wenyewe wakusaidie. Ukishindwa kabisa fika ofisini kwao au nenda Ofisi ya Mkuu wa mkoa ulipo, Ofisi za Utumishi wanaweza kukusaidia kuwapata wahusika.

4. Usirudie kufanya ulichofanya, maana ni kosa kisheria. Ukikutwa na hatia unaweza kufungwa.

Kila la kheri Mkuu.
 
Duuuuh pole kwa changamoto

1. Usiende kwenye huo usaili, wala huyo rafiki yako asiende.

2. Hakikisha vile vyeti unavifanyia mabadiliko, virudi vya muhusika, huyo rafiki yako.

3. Ukikwama, hakikisha unawapata ajira Portal wenyewe wakusaidie. Ukishindwa kabisa fika ofisini kwao au nenda Ofisi ya Mkuu wa mkoa ulipo, Ofisi za Utumishi wanaweza kukusaidia kuwapata wahusika.

4. Usirudie kufanya ulichofanya, maana ni kosa kisheria. Ukikutwa na hatia unaweza kufungwa.

Kila la kheri Mkuu.
Shukrani sana ubarikiwe
 
Back
Top Bottom