Nifanye nini niepuke kivuli cha ex husband asiyekubali kuachana?

Hii taarifa ilibidi uwape polisi chukua RB ...AITWE polisi kuwa lolote baya likitoke yeye wa kwanza
 
Sijui kwanini Tz restraining order huwa hazina mashiko.

Ukijichukulia kuwa ni muhanga na dhaifu kwake, daima atakupanda kichwani na kukufanya atakavyo.

Huyo jamaa yako ni bully, muonevu. Njia pekee ya kumdhibiti mtu kama huyo ni kumkabili. Jitoe ufahamu umjazie watu kila pale anapokuandama. Ukimdhalilisha mara mbili tatu, ataondoka na asirudi tena.

Najua ni ngumu kumchagua wa kumpenda, ila ifikie wakati uchague mwanaume anaejimudu kiubavu kuingia nae kwenye mahusiano. Maana kumpenda mtu asieweza hata kujitetea kiasi cha kudundwa kizembe hapo kuna walakini pia.

Kila la heri mama.
 
Aende polisi.

Hii ya kutafuta mume mbabe ni ukatili kwa huyo mwanaume. Unatafuta mume ili amdhibiti mume wako wa kale, akishamdhibiti? Aende polisi.
 
Haupo serious wewe, na anakujua udhaifu wako hivyo atazidi kukuchezea akili na kukuharibia.
Mkichoka na mkiona hamuendani ni jambo jema sana kuachana. Kuachana ni kila upande kuwa huru au kuwa na uhuru wa maisha mapya, ili yawe huru kwa nyie mliokuwa na ndoa ni lazima ndoa hizo zivunjwe. Fuata taratibu za kuvunjwa kwa ndoa kisheria na huko mtaelekezwa namna ya kulea watoto na taratibu nyingine.
Lakini hiyo ya kuachana kihuni kwa ku copy na ku paste, siku mtakayoenda kuvunja hiyo ndoa, jiandae kugawana naye hilo duka lako. Hata huyo unayesema alitaka kukuoa , ingetokea amekuoa basi na yeye mngegawana na huyo mume wake, maana na yeye angekuwa ni mali iliyopatikana kwenye ndoa hivyo atatumika vile anafaa kutumika
Fuata utaratibu wa kisheria, mambo yataenda kwa wepesi kuliko hii misuli mnayotunishiana
 
Asithubutu kufanya hivyo.
Wengi wa namna hii ni Mental case
Anaweza kumjazia watu, Jamaa akatengeneza kisasi kitakachoweza kumdhuru kabisa Mdada..
Cha kwanza, amripoti Polish Kwa ajili ya usalama wake.
Cha Pili, ahame eneo analokaa ambalo anahisi Jamaa Yuko comfortable kufika Kila wakati.. Ikiwezekana arudi kwao kwanza wakati anajipanga zaidi... Ila asikae mazingira ya peke yake, Huyo Mumewe ni Mgonjwa wa akili..
 
Nenda Polisi. Halafu tafuta msaada wa kisheria. kama unaweza weka wakili kama huwezi tafuta msaada kuna taasisi zinatoa misaada ya kisheria.

Huyo ni kumkatia RB. Anawekwa ndani unamfungulia kesi ya kutaka kukuua au kukudhuru. Na usimuache endelea na kesi lakini usimfunge jela. wakati kesi inaendelea wewe kuwa serious akiona uko serious ataita watu kuomba usuluhishi. Mkubalie usuluhishi kuwa utaondoa kesi pale tu atakapoahidi kwa maandishi kuwa hatakusumbua tena.

Kuna mwanamke namfahamu alikuwa anapigwa na mume wake kila wakati, siku moja akaenda kwa wanasheria wakamuweka mumewe ndani na kesi ikapelekwa mahakamani. Mwanaume alipoona kuna wanasheria wameshikilia kesi na wako serious akaomba suluhu nje ya mahakama kwa kumbembeleza sana mkewe na kesi ikaondolewa. Mpaka leo kashika adabu na hajampiga tena mkewe
 
Ndoa za kiislam mitihani mikubwa sana. Mtu anadai talaka hata akiwa BAFUNI
usiombe ukaoa wale wanaovaa vihikabu tena katoto kamwisho
Ukienda hapo BAKWATA ni mauza uza tupu mtu anajadili maswala ya ndoa ya mtu akiwa na hukumu mkononi. Yaani kuna mzee yeye ndiyo polisi, hakimu na mahakama.
I nashangaza
 
Pole kwa kuangukia katika ndoa ya mwanaume asiyejitambua.

Ndoa ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke kuishi pamoja au siyo?

Ndoa hailazimishwi, mmoja akitaka kuivunja, inavunjika na kila upande kupata haki yake.

Huyo X-mmeo ni kati ya wanaume wapumbaf wanaochukulia mke ni kama bidhaa ya kumiliki na kuhodhi na si muunganiko wa wapendanao wenye haki sawa mbele za Mungu na mbele za sheria.

Cha kufanya, anzisha mahusiano mengine ili aingie kwenye mfumo kama ataendelea kukuzoea.

Atakapoingila uhuru wako tena, tengeneza ushahidi uliokamilika, buruza mahakamani kama unaua nyani bila kumuangalia usoni, pia dai talaka yako kisheria haraka iwezekanavyo.

Tatizo nimeliona katika mada yako ni kwamba, unamlegezea sana huyo bazazi.

Talaka uliyoidai, uliidai kwa nani na kwa njia gani, mbona haujatupatia mwendelezo wake?

Huyo unampetpet kama mume au ndugu, huyo ni adui yako, kaza fuvu ili kumuondoa kabisa katika mzunguko wa maisha yako na kubakia na uhuru wako.
 
Huko kwenu hakuna wazee?
Huyo anapigwa kitu atakukimbia mwenyewe mbona!
 
Kusanya ushahid wa anayokutendea ikibid aliowahi kuwadunda au kuwapiga mikwa waje watestfy mahakama itamuamuru akae maelfu ya kilometa za mraba mbali na maisha yako
Hii sheria ya kukaa mbali kwa mita kadhaa huku kwetu inatendeka kweli? Walai naitaka maana nimechoka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…