Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Pole Mkuu.

Kama una uhakika kweli huwa wanakuomba kwa Shida. ( Yaani wanakuomba kile ambacho hawana) .

Usijisikie vibaya kumsaidia asiejiweza.

Wasaidie tu kadri ya Uwezo wako utakavyokuruhusu.

Na Mungu atakubariki indirectly.
 
Wewe ni KE au ME?
Inaonekana na wewe ni shida, unashinda shinda sana ndani.
 
Bro wata omba vipi akati kila siku una onekana na kisu miksa panga mpya😂🤣.
 
Pole aisee solution ni kuhama tu hapo
 
Vp ni watu kutoka makao makuu ya nchi!? Siku ya sita pia sema SINA, Over!
 
Kama huwezi kuhama, basi vumilia tu!
 
Wape kama unacho kama hauna basi.
Jinsi unavyotoa ndivyo unavyovuta baraka hasa kwa watoto na watu wenye uhitaji.
Naunga mkono hoja...wasaidie kwa ulichonacho, kama huna waambie huna, Baraka zitakujia tu ukiwa mtoaji
 
Achaaa roho mbayaa,kama unauwezo wasaidie....hakuna raha na baraka kama kusaidia wenye uhitaji?fanya hivi kama unakiuwezo wanunulie kisado cha nyanya,vitunguu...na tumafuta....afu wambie mtumie hivyo kila mwezi
Umenena vyema, hii njia bora
 
Sehemu mpya nimehamia.

Wapangaji wanne.

Narudi mke ananiambia wameniuliza kabila nilivyowajibu wakasema kabila lenu hua siyo wachoyo bora tumepata mtu siyo mchoyo.

***** ilikua ni mwendo wa hili balaa kutoka kwa wapangaji watatu. Mwanzo mke aliona ujirani kumbe ile ikafanya waamini kwamba hawa wana pesa. Walivyoanza kuchinjiwa baharini huwezi amini mtu ananuna kabisa.

Na mwingine akauliza kwani mmefilisika siku hizi?

Funny times
 
Usipende kuwapa watoto wa watu vyakula vilivyopikwa kama hamna mazoea ya kupeana zingatia kupeana
Maisha yamebadilika siku mtoto wa watu kaumwa hata kama sababu sio kutokana na chakula chako utaona dunia chungu
Wema usizidi uwezo
 
Kuzaliwa kwenye familia kama ya huyo baba, ni bahati mbaya sana.

Nachukia sana kuona mijitu maskini inazaa na kuwa na watoto halafu haiwezi kuwahudumia.

Watu maskini hawapaswi kuzaa watoto.

Mtu maskini akizaa mtoto anaongeza maskini mwingine duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…