Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Pole Jirani AmKATRINA , Mimi mwenyewe siendeshi gari la mafuta wala nini sema nakwepa kuombwa ombwa hovyo
 
Hapa bwana we tafuta chumba kingine maeneo ayoayo, kama mtu hukuzaliwa na roho ngumu kutekeleza ushauri wa baadhi ya wachangiaji ni ngumu kutekelezeka, kwa kua hakuna ajuae kesho yetu, na hao watoto kesho yao hatujui nini ,mungu ameweka ndani yao we tafuta chumba kwingine ,ili uachane nao kwa amani basi ,cha msingi wanajua umewasaidia na ulikua unawasaidia.
 
Afadhali huyo, kuna mwingine hapa ukifika usiku wa manane anadai chumbani kwake hakulaliki, usiku kucha anasumbua wapangaji, mara alale sofani, mara akae tu kitini kwenye vyumba vya wapangaji kwa atakayemgongea siku hiyo. Anadai anaona mashetani chumbani kwake ikifika usiku wa manane
 
Baraka hizo usipende sana kumind vitu vinavyohusiana ma chakula .jiepusha kumind mambo ya chakula....... vitu vya kumind mi michongo ya kuingiza pesa.... we wape tu si vimichuzi tu hivyo bob wakiomba hela sema sina ....ila vimichuzi sijui vinyama uwapa hata kijiko kimoja kimoja .... narudia tena epuka sana kumind vitu vinahusiana na chakula hasa ukiwa mtoto wa kiume
 
Ulimzoesha vibaya... Kwenye nyumba za kupanga usitake mazoea ya kupitiliza ... Suluhisho ni kuhama tu
 
Ji-distance na kuwa busy na mambo yako,wasikuzoee........ kuna sehemu nilihamia miaka kadhaa iliyopita,nilihama miezi miwili tu,Picha linaanza Mama mwenye nyumba ni mgonjwa mgonjwa ana ishi mita kama tano ya apartment zake.......Saa kumi alfajiri nikasikia mtu anagonga,nikaangalia saa nilidhani nimepitiliza mpaka kumekucha,kumbe mama mwenye nyumba,nikashtuka....akasema mwanangu samahani naomba sukari kidogo natakiwa kunywa dawa.....sikumpa maana nilihisi atakuwa mwanga πŸ˜€πŸ˜€..... kwasababu nilikuwa nina siku mbili tu, asubuhi nikatoka, jioni nikamuuliza mshikaji niliyemkuta akadai yeye amechoka hawasemeshani kwasababu hiyo na kodi yake ikiisha anasepa........hapo hapo namm wazo la kuanza kutafuta nyumba likaja πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…