Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Robo tatu ya akili watoto wanariti ujombani, robo ndiyo ya kwako. Pia lishe kuanzia mama akiwa mjamzito hadi ukuaji wa mtoto inaboresha akili ya mtoto. Hapo walipofikia waache wasome hivyo hivyo, usiwalazimishe kwani itakuwa ni kama mashine ya horse power 5, unataka iperform kama mashine ya horse power 10.
 
Wewe unataka mwanao awe na akili darasani au awe anashindana darasani?.

Akiwa na akili zinatosha kabisa ilimradi tu afahamu mambo muhimu ya shule.

Anza kumfundisha mambo ya maisha, elimu nje ya hilo darasa ili imfae naishani achana na kutaka awe anashindania kufaulu mitihani ya darasani.

Angalia pia anaweza nini na ana kipaji gani alafu uanze mtengenezea mifumo.

Kwani mpaka leo hujajifunza kuwa elimu ya darasani ina mchango mdogo sana kwenye kufanikiwa kimaisha? Au na wewe ndio slow learner Mkuu?
 
Ukitaka kuwa na watoto vipanga darasani hakikisha unaoa mke kipanga haswa.Yaani mkeo awe mwerevu Kweli Kweli.

Then hakikisha watoto wako hawali ugali kbsa coz Ni chakula kinachodumaza akili.
Sentensi ya kwanza umesema ukweli kabisa, ila hiyo ya pili umetudanganya, Cha msingi ni lishe bora tangu mama akiwa mjamzito hadi makuzi ya mtoto, ugali hauna shida yoyote kama utapata mboga sahihi
 
Wanarithi kwa baba na mama
Kama nyie ni vilaza msahau watoto wenu kua na akili nyingi
Ndo najiuliza hapa kama mzazi anakuja kudesa JF kwa jambo kama hili, anatarajia mtoto wake awe ana akili kweli?

Relax, kila mtu ana njia yake akifeli shule, msapoti kwenye kipaji chake, mafanikio ya juu kabisa hayahusishi elimu ya darasani, be a proud father/mother and let yout kid's destiny take its way

Shule ya mzungu siyo mwisho wa dunia
 
Naomba kujua watoto ni wa umri gani ?
 
Akili katika lipi? Maana si kwamba kila binadamu kaumbwa na uwezo wa kukariri kwa haraka tunatofautiana pakubwa sana na ni lazima tutofautiana , ukiwachunguza wanao kuna vitu wanauwezo navyo kuliko hiyo ya kukariri unavyo taka wawe
 
Ni genetics kwa asilimia chache sana. Sababu kama ni kweli genetics zingekuwa ndio zina-determine intelligence ya kiumbe kwa 100%. Then it means kuna familia na vizazi ambavyo ni wajinga milele. Kitu ambacho ni kinyume na sheria kuu ya nature, Development and specific adaptability to certain environments. So usiwasikilize waliosema Genetics kama kichocheo kikuu cha akilia za binadamu.

Bali kwa kiasi kikubwa intelligence ya binadamu inachochewa na Malezi na Mazingira. Hivyo kumlea mtoto kwa kukuza curiosity yake ya utoto na kumjibu kila swali lake na kumsukuma ili aendelee kuwa hivyo ni njia mojawapo. Badala ya kumfokea kwa kumuona msumbufu. Kwani kufanya hivyo kutam-discourage na kudumaza uwezo wake milele. Ukilinganisha watoto huona wazazi wao kama miungu na kuamini kila walisemalo.

Hapo utaupa nafasi ubongo wake kukua kwa haraka, wanaita brain-plasticity na ku-strengthen neurotransmitters. Hivyo kuzidisha ufikiri na kasi yake, ikiwemo kuongezeka kwa curiosity. Hapo lazima apasue masomo ya darasani ambayo kwa wakati huo wa miaka 6-7 yatakuwa chini yake sababu tayari ubongo umekomaa kupitiliza. Ni kama vile wewe upewe maswali ya 5+5. Vilevile kumfunza lugha za kigeni kama English au Kifaransa zinasaidia kukuza uwezo wake wa kufikiri na kusolve vitu.

Kama kweli unataka kukuza an absolute thinking machine basi, kwenye kipengele cha mazingira itabidi uwe strickt kupitiliza. Ikiwemo kuangalia marafiki anaocheza nao kila siku ni watoto wa aina gani kutoka familia gani ya watu wa aina gani ili kutomchanganya wako na wao na kupelekea kudumaa kwa ufikiri, curiosity, utambuzi na brain-plasticity inayochochewa na new informations.

Hapo bado hujachelewa kama bado ni wadogo. Kujibu maswali, kujifunza na udadisi isiwe shule tu. Bali maisha yao ya kila siku.
Vilevile fimbo hazisaidii kitu bali hubomoa tu kwa kumpa mtoto uoga na kumuaminisha yeye hawezi kufanya ulichomwambia kwani njia pekee ni kuelewa. Kitu ambacho sio kweli, sababu mara nyingi mzazi na mwalimu ndio wenye makosa yanayosababisha mtoto kutokuelewa.

Na vilevile mazoea ya mzazi na mtoto. Kama mwanao unamlea kama mbwa kazi yako ni kumpa chakula na kumkaririsha kanuni za hisabati. Basi usitegemee huyo mtoto kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.
Kukaa nae muda mwingi, kucheza nae, kuongea nae kama mtu mzima, na kuwa na mazoea naye kama rafiki ndiyo njia pekee ya kujua akili ya kweli ya mtoto na kujua utaikuza vipi. Matter of fact, watoto wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na ufaulu mkubwa darasani, wengi ndivyo walivyolelewa hivyo. Otherwise ni kazi bure.

Dogo langu anapasua 100% kwenye kila mtihani bila hata kutumia nguvu. Na hata mimi nilikuwa nafaulu mitihani bila hata ya kusoma na kukesha usiku kucha kama wale mabaharia wa mabeseni.

Simply sababu uwezo wa kufikiri na uwezo wa kusolve makubwa ulikuwa mkubwa, hivyo viswali vya mitihani ni kama kumuuliza mtu mzima 1+1.

Kuna thread niliandika a few years back inahusu why Africa haina maendeleo, nenda kaicheck. Nimeelezea baadhi ya haya mambo.
 
Angalia kwanza wanao wana vipaji gani na wanapenda nini,ukiona mtoto anapenda kupiga kinanda kwa mfano muendeleze,using'ang'anie tu kuwapiga ili taaluma zao zipande,anza kuwafundisha stadi za maisha,una Dip ya IT itumie hiyo kuwafundisha wanao stadi za maisha kuendana na Teknolojia. Tatizo unataka wanao wasome sana ili baadae wakaajiriwe wakati wewe umesoma IT ambayo unatakiwa uitumie kuwafundisha wanao teknolojia
 
Ni sahihi lkn je watoto wanaweza fanya meditation? Binafsi huwa nafanya lkn kama mtu mzima nakutana na changamoto smtm vp khs watoto?
 
Ugali ni ugali tu.. hakuna cha sembe wala dona. Ni chakula kisicho na faida yoyote. Ni kama kuweka jiwe tumboni. Hata kwenye biblia walikuwa wanakula mikate na sio ugali.
Dah watu mnauchukia ugali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…