Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Hata ikiwa kila ki2 humo sawa na zitatosha kwa kianzio ila profit utayopata ni kubwa sana kaa uwekezaji wa hiyo mil8 kikubwa UZA jumla na rejareja utamaliza mzigo haraka na utawahi kuchukua mzigo mwingine na ukienda kwa mara ya pili dubai unaweza pata mzigo kwa discount kubwa mno yaniii kiufupiii spare parts used haimuangushiii mtuuu tuishiii humu
 
Kuna mengi ya kuzingatia pamoja na imani yako na ujuzi ulio nao. Ingia ufugaji weka ngombe. Kama imani inaruhusu fuga nguruwe.
 
Dah Wabongo KWA kukatisha watu tamaa hamjambo Mimi nilianza na nusu yake baada ya kudunduliza na nikawa naingiza mil 2.5 KWA mwezi kwenye biashala nafaka one kuwa yeye ambaye ana 12 Yani hapo akitulia anatoboa mapema sana
Mkuu umesema kwa kifupi sana tuelezee kwa undani kidogo tupate mwanga.
 
Salaam Alleykhum,

Wadau kwa kutumia uzoefu wenu, nishaurini nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa million 12 nilionao ili kila mwisho wa mwezi at least nipate Net profit ya milioni mbili.

Nipo tayari kufanya biashara ktk mkoa wowote Tanzania au hata kama ni importation business kama mtaji unatosha nipo tayari.

Nipeni ushauri ili nami nitoboe.
Wekeza kwa mkataba na kampuni ya vegrab.co.tz utafunga mashine za kukaushia pilipili na utalipwa na kampuni mpaka 2M Kwa mwezi

Na mradi ni mpaka 20years
 
Wekeza kwa mkataba na kampuni ya vegrab.co.tz utafunga mashine za kukaushia pilipili na utalipwa na kampuni mpaka 2M Kwa mwezi

Na mradi ni mpaka 20years
mkuu na amini una kitu kizuri kutujulisha lkn maelezo yako kama hayajitoshelezi. Chambua kidogo watu wapate mwanga zaidi
 
Biashara mpya kwa mtaji huo mkubwa is too much risk kama hautasimamia mwenyewe mkuu

Ila kuna option ya kununua mazao ya chakula hasa Mpunga gunia zako za kutosha na kuziweka store na inapofika kipindi cha Masika unafanya kuzikoboa gunia zako na kupata mchele wako swafi tayari kwa kuingiza sokoni kwani kipindi hicho uhitaji wa mchele unakuwa mkubwa sana hapa Dar es Salaam na Zanzibar

Minimum profit calculation

Katika centre nyingi ninazo zifahamu kwa muda huu gunia moja la Mpunga lina range kwenye TSH. 50,000/=
Hivyo basi kwa Pesa uliyonayo yaani TSH. 12,000,000, utaweza kupata gunia zenye debe sita sita 240 za mpunga na kuzihifadhi.

Kipindi ambacho Masika imechanganya hasa mwezi wa kwanza au wa pili, wewe ndo unafanya kukoboa mpunga wako ili upate mchele na gunia 1 la mpunga la debe sita linatoa debe tatu za mchele na debe moja la chenga za mchele

Hivyo basi katika zile gunia 240 unazidisha mara 3 na utapata debe 720 za mchele clear na debe 240 za chenga za mchele

Ukija sokoni debe moja la mchele lina range kwenye 35,000/= kwahyo unazidisha mara debe zako 720 za mchele na utapata kiasi cha TSH. 25,200,000/=, pia debe moja la chenga za mchele ina range kwenye TSH 10,000/= ukizidisha na debe 240 utapata kiasi cha 2,400,000/=

Total itakuwa ni Tsh. 27,600,000/= na ukitoa mtaji wako wa 12,000,000/= utapata net profit ya TSH. 15,600,000/= katika kipindi cha miezi mitano cha kuhifadhi mpunga wako

Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu.

Centre zenye mpunga mzuri ni kama zifuatazo Kyela, Kamsamba na kilyatundu, Usangu, Kahama ila kwa Morogoro sizifahamu vizuri

Naomba kuwasilisha na ninakaribisha maswali
Tupe na gharama za usafirishaji toka shamba mpk Dar pamoja na ushuru na mengineyo ili tupge hesabu ya net profit
 
Kuna mengi ya kuzingatia pamoja na imani yako na ujuzi ulio nao. Ingia ufugaji weka ngombe. Kama imani inaruhusu fuga nguruwe.
Mkuu, mrejesho wa faida hapa huonekana baada ya muda gani??
 
Back
Top Bottom