Nigeria: Aliyemtukana Mungu ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani

Nigeria: Aliyemtukana Mungu ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani

Inategemea huyo Mungu alipomtukana alimtukana akiwa ktk content zilizotokana na dini gani,kama alitumia content za ile dini ya wenyewe kumtukana ajue na atambue yeye ni maiti inayotembea muda wowote kichwa wanabeba

Ila kama ni wale wengine wa shavu hili geuza na hili hata akienda kumtukana tena leo hakuna wa kumgusa.
Kwa mantiki hiyo wamemtoa huko ili wajekumhukumu kwa ule Utaratibu wa "Sisi tunayo Sheria, na kwa Sheria hiyo Imempasa kufa"
Kweli ni maiti inayotembea.
 
Huyu jamaa alikuwa muislamu, akaacha imani akawa atheists

2014 wazazi wake walimpeleka hospitali ya akili, wakiamini alichanganyikiwa

Alifanikiwa kuwa raisi wa Humanist Association ya Nigeria

Shida ni kwamba alikuwa anakosoa dini kwenye account yake ya fb

Huko kwenye jimbo alilokuwa anaishi, kuna sharia law

Siku moja sijui alipost nini wakamkamata wakidai alimtusi prophet mohammed

Alitrend hadi BBC walitengeneza documentary
 
Kwa mantiki hiyo wamemtoa huko ili wajekumhukumu kwa ule Utaratibu wa "Sisi tunayo Sheria, na kwa Sheria hiyo Imempasa kufa"
Kweli ni maiti inayotembea.
Naam; kwa maana amemkufuru mungu. Mkate kichwa, mkate kichwa, mkate kichwa!
 
Ndio maana wenzetu wanakuwa comfortable kumtukana au kumkejeli Yesu kwa sababu uhakika baada ya kuishi upo. Huwa tunaamini ni yeye mwenyewe hatamalizana na wewe.

Sisi ni nani hata tutoe hukumu kwa niaba yake.

Kwa hawa wenzetu mambo ni tofauti kabisa na huyo jamaa na hakika hao watu amekuwa nao, amesali nao, anajua vizuri mihemko yako sijui kwanini alijichanganya.
 
Mwanaume asiyeamini kuwa Mungu yupo kutoka nchini Nigeria, Mubarak Bala (40) ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani kwa tuhuma za kumtukana Mungu kupitia Facebook mwaka 2020.

Mubarak alikamatwa Aprili 28, 2020, kwa tuhuma za kukufuru dini na uchochezi kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii.

Aprili 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 gerezani baada ya kukiri makosa 18, ikiwa ni pamoja na kukufuru na uchochezi.

Hata hivyo jana Januari 7, 2025, aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani. Baada ya kuachiliwa amesema usalama wake bado uko hatarini kutokana na vitisho.

"Wasiwasi kuhusu usalama wangu upo kila wakati," aliambia BBC katika mahojiano yake.

Mwanaume huyo kwa sasa anaishi katika nyumba ya hifadhi, huku mawakili wake wakidai maisha yake yako hatarini ikiwa atarejea kuishi katika jamii.

View attachment 3195842
Aendelee kukaa jela
 
Naona watu povu linawatoka humu wakati mtukanaji mwenyewe ALISHAKIRI MAKOSA YOTE NA NDIPO AKAPEWA STAHILI YAKKE
Kama ndo hivyo; mbona tena wamamwachia huru baada ya kutumikia miaka 4 badala ya hiyo stahiki yake miaka 24? Hapo kuna harufu ya "jambo linasukwa" ili fursa ipatikane na Itumike ile Sharia ya kwenye kile kitabu inayotaka apigwe mawe hadi kufa.
 
Inategemea huyo Mungu alipomtukana alimtukana akiwa ktk content zilizotokana na dini gani,kama alitumia content za ile dini ya wenyewe kumtukana ajue na atambue yeye ni maiti inayotembea muda wowote kichwa wanabeba

Ila kama ni wale wengine wa shavu hili geuza na hili hata akienda kumtukana tena leo hakuna wa kumgusa.
Mke wake anasema kabisa waislamu walikuwa wanajadili namna ya kumuua kwenye magroup ya facebook

Sasa wakati anamshtua atoroke huo mji jamaa akawa ameshakamatwa

Sema nigeria kuwa atheist ni ngumu, hadi kuuliwa wanauliwa

Na kule kuna hukumu ya kifo kwa ajili ya kukufuru
 
Kama ndo hivyo; mbona tena wamamwachia huru baada ya kutumikia miaka 4 badala ya hiyo stahiki yake miaka 24? Hapo kuna harufu ya "jambo linasukwa" ili fursa ipatikane na Itumike ile Sharia ya kwenye kile kitabu inayotaka apigwe mawe hadi kufa.
kuna mashirika mengi ya wazungu yalipaza sauti nasikia

UK Humanists na US Commission of International Religious Freedom waliingilia
 
Kilichomsibu huyo mwanaume ni DINI na wala sio eti alimtukana Mungu.
Mungu hajawahi kuhitaji watu wa kumtetea au kumsemea. Mbona hatujamsikia Mungu akilalamika katukanwa? Watu wanajipa Uwakili kwa Mungu i.e. Mungu ni mteja wao.
Kwani hapo mahakamani mawakili wake hawakuomba upande wa mashitaka wamlete mungu athibitishe uwepo wake? Hao ni waislamu tu na si vingine
 
Kama ndo hivyo; mbona tena wamamwachia huru baada ya kutumikia miaka 4 badala ya hiyo stahiki yake miaka 24? Hapo kuna harufu ya "jambo linasukwa" ili fursa ipatikane na Itumike ile Sharia ya kwenye kile kitabu inayotaka apigwe mawe hadi kufa.
Hapana ndugu,
Kuna rufaa na mambo mengine mimi na wewe hatujui kwahiyo tusidhani wala kubuni
 
Alitukana dini wala sio Mungu.
Mungu akitukanwa adhabu anatoa yeye wala haitaji kusaidiwa na viumbe ambavyo kaviumba mwenyewe.
Ukitukana dini wanadamu watakushughulikia maana ndio walioleta hiyo dini.
 
Back
Top Bottom