Niishi vipi na uyu baba wa watoto wangu

Mambo ya ndani unayaleta huku jamii forum???
Au unafikiri Mimi siijui hii akaunti yako?
Umesahau Kuna siku ulinitajia hii akaunti yako wakati tupo katikati ya 'game'......
Au miuno yangu ilikuchanganya siku Ile hadi ukawa unaropoka?
 
Mmeo ni mjinga tu. Hapo anza kujitetea kwa Mungu wako akupe wepesi wa maisha mengine
 
Dada imarisha beki, usiruhusu kupigwa bao la tatu, watoto hao wawili pambaneni nao kwanza
Shauriana na mumeo na ndugu na jamaa upate shughuli ya kufanya pamoja mlisongeshe
Pia weka wezi elimu yako kama huna shughuli kwa sasa Jf ndo jamii unaweza saidiwa na wenye nafasi za kazi
Ila ukipata usiwe na kiburi, hudumia wote kwa upendo na staha maisha hayana mwenyewe na usimsaliti atakayekusaidia
 
Nyie wanawanake wa aina hii bado mpo? Jamaa amepata mke ila tatizo kwenye miti mingi hakuna wajenzi.
Kama utaweza, uza simu. Nunua ya batani (kikubwa mawasiliano) Anza kuchoma vitumbua, chapati, uza mkaa au maandazi
 
Pole dada..
 
mumeo anafanya kazi gani hadi uamini ana hela
ukute naye maisha yamempiga, ila wewe unaamini ana hela na ni mbahili
Hizo akili za kuelewa hilo suala kwamba nyakati hazifanani,wanawake wengi hawana.
Kama amezoea kupewa 300k siku ukimpa 200k anawaka kama jibwa.
 
Sali muombee mumeo kaa week moja kwa amani alafu siku moja niambie haya. MUME WANGU HIVI HAYA NDIYO YALE MAISHA TULIYOPANGA KUJA KUYAISHI KAMA UMEAMUA KUNITESA MIMI BASI NAKUOMBA SANA USIWATESE WATOTO WAKO HAWANA KOSA alafu lala muache
 
Nadhani ungeanzia maisha ya uchumba, na baada ya ndoa kabla ya kupata watoto jamaa alikuwa anatoaje matumizi???
 
Huyo mumeo ameishakuona kiazi na huna akili Kwa sababu ulishaonesha sio mvumilivu , mpaka ukamkimbia na kurudi kwenu Ina maana wazazi walikusikiliza wakaona huna sababu za msingi pengine makosa yalikuwa ni Yako na ulivyoamua kurudi Kwa mumeo kumbe alishakutoa moyoni hivyo ameamua akukomoe tu ukitaka ondoka au Baki , ushauri wangu ni kwamba kama Kuna sehemu ulimkosea kaa nae chini ujishushe na umuombe msamaha na umwambie jinsi unavyoumia na hiyo Hela ndogo anayokuachia hakuna mwaname jeuri mbele ya mke mnyenyekevu
 
Babu yangu mzaa mama aliwahi nuambia kaka yake alikuwa anapigwa na mke badala aliye yeye mke ndio anapiga ngolo majirani njooni mnisaidie mume wangu ananiua!!
 
Uliingia kwenye ndoa bila kujua ndoa ni nini?
 
Handwriting katika hii ya kutafuta mchumba ni tofauti na hii ya kukosa msaada wa mumewe. Hapa sijamuelewa.

Napenda watu mnaofanya investigation.

ila nikivaa viatu vya huyu dada mimi ni mwanaume. Nilipata stress kazin baada ya kushushwancheo...

Niliteseka sana. Nilikiwa na uwez wa kununua nguo zangu na za watoto kwa kidg ninachokipata leo nakunywa tu pombe...mavaz hata yangu mwenyewe sinuous...nimebadilika...mke kuna muda analaum na anamatanio makubwa ambapo mimi sina uwezo tena japo napata mshahara bila posho. Na madeni nimengi.

Namuona jamaa analopitia mkewe hampi courage anabaki kumlaumu.

Najisikia vby sana kununua nyama na pombe wkt nyumbn watoto wanakula majani na maharage. Siku moja moja nanunua nyama kama kilo 3 au mayai na vitu bzr kwa watoto..matunda nakadhalika.

Najisikia vby sana hali ninayopitia. Sometimes namuonea huruma mwenzangu akipanga bajeti naming akili ikiwa kama haipo.


Kesi ilikuwa hivi.
Boss alinibadilikia. Gghafla barua kutoka juu ikaja ikinitaka kurudi chini na kukosa posho za maofisa. Hali yangu haijabadilika bado japo nikipata mshahara nahakikisha nalipa ada watoto wasiende shule zetu za kata..wabaki private.

Wanaume kama mimi nimejiona kabisa nikivaa viatu vya muwewe huyu dada. Lkn pia nikimuomea huruma dada huyu kama ambavyo naona namkosea mke na watoto kwa sabab za ofsn.

Nilijaribu kumrudia mungu na kujitafuta kwa.namna nyingi lkn hali hizi zisikieni tu.

Wkt mwingine nagombana na makondakta kakitunkadg hata 50/= konda akisumbua tu napata hasira.

Nimebadilika. Nimekuwa mtu wa ajabu. Nasoma sana vitabu mtandaoni hadithi story kibao. Bado ru.


Nikirejea kwa dada fanya mambo haya. Nunua katanga fungal za 100 na 200 hadi 500 uuanze..pika pika cookies na humo mtapata na vya chai kwa familia. Jamaa yeye mpe heshima yake kama mumeo. Hakuna mume mzur huko nje.

Lima bustani hata kwenye makopo panda mbogamboga.

Cheza vikoba uhifadhi hata 1000 kwenye kikoba. Mwakan mkivunja una hela ya shule na nguo za mtoto. Jamaa atarudi mwenyewe
 
Pole sana kwa unayopitia, kuwa karibu na familia yako, hao ndio faraja yako.
 
Haya mambo Ukianza kusikiliza malalamiko ya mwanamke siku zote utamuona mwanaume ni katili sana ila ukipata na nafasi ya kumsikiliza mwaume huenda ukagundua mwanamke ndo shetani
 
Anapaswa kupitia hii comment yako boss,heshima kwako kwa kuona tatizo la wanawake wengi,utafutaji waridhiki umegubikwa na changamoto nyingi sana,hata kama ni kidogo kiasi gani atoe shukurani taratibu mwanaume hubadirika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…