Nikimkumbuka Ronaldinho Gaucho machozi yananitoka

Umewalist wote alafu ukamsahau Messi bahati mbaya au makusudi? kwani Messi amecheza na wote hao karibia 80% ya maisha yao soka.
 
Umewalist wote alafu ukamsahau Messi bahati mbaya au makusudi? kwani Messi amecheza na wote hao karibia 80% ya maisha yao soka.
Ahahahahah
Hapana aisee, nadhani nina mapenzi na wengine ILA unapotaja mchezo wa mpira wa miguu, hakuna namna ukatenganisha mchezo huo na jina Messi hata kama hakutajwa.

Ingawa Messi hakucheza na kina Claudio T, hata hivyo sijawataja kwa kufuata mtirirko wowote, angetokea tu boss, kuna kina
Gudjonsen
D. Dafu
Cafu
Dunga
Davor Suker
Seerdoff
Keane
Viera
N.k
 
Uko sahihi mkuu.

Ukiangalia hata balon D'or walikuwa wanapokezana kwa sababu wengi walikuwa bora. Kaka kapata 1, Zizou 1, Figo 1, hata Gaucho mwenyewe alipata 1. Hapo ni miaka ya 1998 onwards..
Nakumbuka kama Gaucho alipata mbili
 
Huyu mwamba kwenye kizazi cha video, hana mpinzani wala mshindani.
Sio Okocha Jay Jay, Zizzou wala yeyote anaweza kufikia kipaji chake
 
Kumbukumbu zipo sahihi,zinanieleza ndo mchezaji wa kwanza kupewa heshima Santiago bernabeu ktk mechi ya el classico.....baada ya kuwachachafya sana,Rijkard anamtoa ili akapumzike Madridians walisimama na kumpigia makofi kiroho Safi kwa burudani aliyowaonyesha japo alikuwa mpinzani
 
Jamaa alikuwa mwamba kwa hakika....ktk era yake kulikuwa na viungo wa ushambuliaji zaidi ya kumi kwa kuwataja ambao walikuwa mabingwa haswaa tofauti na kipindi cha akina cr7 na reo10 ambapo hao viungo ni wa kuwatafuta na tochi hata kumi hawafiki
Na kipindi hicho kulikuwa na mabeki wa kazi kazi haswa na wenye roho mbaya na Wala hii sheria ya kuwalinda wachezaji nyota dhidi ya mabeki wakorofi haikuwepo,ndo yy aling'aa,sio mchezo mdogo kumfanya Sargado na Hiero kulala na viatu baada ya mechi....Hawa akina reo10 na cr7 wamewakuta akina Marcelo na alves mabeki laini kabisa mabeki wa kushambulia toka lini wakawa na roho Kama zile za akina Nesta au Materazi ambao kwenda mbele ni mwiko kazi yao ni kuosha na kupiga daruga mwanzo mwisho
Mwamba alituburudisha na sisi washabiki na wasio mashabiki wake kila tulipomuona ndani ya pitch tulipenda ikiwezekana pasi zoote apelekewe yeye kwanza
 
Umemaliza Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…