Nikirudi nyumbani nisipokuta chakula tayari inanikera sana

Aisee pole sana..katika eneo sifanyi masihara ni maakuli kwa mume wangu..lazima akute chakula anaporudi home ata kama namalizia kupika lazima atapata chakula cha kuzugia zugia akisubiri mlo kamili.ila ongea nae bado hajakufahamu uhitaji wako vizur..
 
Ukiangalia cha maana alichokuwa anafanya ni kuangalia tamthilia kwenye TV tu!
 
Kazi nyingi kama zipi? Hivi mwanamke anayejituma kazi nyingi zinatokaga wapi? Usafi wa nyumba kufua na kupika ndio kazi nyingi ukute hata watoto bado hamna😅 hapo! Kuoa slayqueen ni kujitaftia mabalaa sana
 
Sisi tunapenda wanawake warembo haswaa. Na sasa hao ndio wako namna hiyo. Na kama si mrembo, binafsi hata sina hamu ya penzi.. na sitaki kuoa mke ambaye sina hamu na penzi lake.
Hahahahahah warembo sindio hao waliobandika makucha kama majini?
 
Acha gubu mbona hilo swali halina ubaya kabisa
Maana vyakula ni kubadilisha basi uwe unamuwahi unasema leo nataka kula chakula flan
Acha gubu nyau wee
Ina maana na wewe huwa unamsubiria kidume aje ndio uanze kumuuliza swali la kipuuzi kama hilo mtu mwenye njaa? Mbona mnatutaftaga sababu sana nyie?

Raha ya mke awe anajiongeza anajua cha kukupikia daily ili ufurahie. You don’t wanna plan that shyt we unatamani ukirudi ukute mambo mezani ufurahie chakula kitamu kilichoandaliwa special kwa ajili yako.

Kama ambavyo mnapenda Kupewa zawadi kwa suprise ama hela ndivyo ambavyo tunainjoy kukuta tumepikiwa.
 
Ndo maana wanaume tunakufa mapema😂😂
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unatamani ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Ongea naye, kila jambo liwe na wakati wake, la sivyo itakuwa ni vurugu maisha yenu yote.
Ndoa ina mambo mengi, ikiwamo mawasiliano kati ya wanandoa.
 
Mawasiliano ni muhimu, mueleze chochote atakachotayarisha kitatumika, la kama kuna utakachokuwa na hamu nacho utamtaarifu ili kuepuka kutoelewana kati yenu. Kama ambavyo umeona, hajifunzi lolote kutokana na jinsi unavyochukizwa na hilo swali, suluhisho ni kuongea na si kuzila na kukaa kimya, asipoelewa mnachoongea na kukubaliana hapo itakuwa ni tatizo jingine.
 
lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Huyo mtu kwa mfano ni housegirl, mke au girlfriend?? Hapa nimechukulia "mtu" ni jinsia ya kike..
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unatamani ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Ndugu yangu usisahau kua mkeo io mpishi wako, yeye kukupikia anakusaidia kwahiyo usichukulie poa msaada anaokupa. Pili usisahau wanawake wana majukumu mazito sana ya kuratibu na kutekeleza shughuli za nyumbani kuzidi hata hizo zako za ofisini. Wewe kupata mshahara na kuleta pesa nyumbani sio suluhisho la mambo yote. Msaidie mkeo, ukirudi msosi bado angalia kile umachoweza kumsaidi ili mule mapema. Acha kumlalamikia kisa tu unaleta matumizi nyumbani.
 
Hapana si mtu unamuuliza kwa simu kabla hajaja home nikupikie nini akij anakuta chakula tayari
Kuna vyakula vya kupika fasta mfano yupo njian ndio unatenga maji ya ugali akifika anakula ugali fresh
Haya nawaachia mlooana
 
Hapana si mtu unamuuliza kwa simu kabla hajaja home nikupikie nini akij anakuta chakula tayari
Kuna vyakula vya kupika fasta mfano yupo njian ndio unatenga maji ya ugali akifika anakula ugali fresh
Haya nawaachia mlooana
Nipikie pizza baragumu😅

Kumbe hujaolewa bado😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…