Nikirudi nyumbani nisipokuta chakula tayari inanikera sana

Nikirudi nyumbani nisipokuta chakula tayari inanikera sana

Aisee pole sana..katika eneo sifanyi masihara ni maakuli kwa mume wangu..lazima akute chakula anaporudi home ata kama namalizia kupika lazima atapata chakula cha kuzugia zugia akisubiri mlo kamili.ila ongea nae bado hajakufahamu uhitaji wako vizur..
 
Hata siku moja sijawah kurud nkakuta msosi bado

Bia tamu sana unarudi mapema home ili ugundue nin?
Kama hiyo mkuu?

IMG_20211123_194228.jpg
 
watafutieni wake zenu changamoto [emoji23][emoji23]...
watu wengi hawajui kupangilia kazi zao aisee, sisi kwetu tulilelewaga chai iwe tayari saa 1-2 lunch saa7 dinner saa1 usiku wa kuchelewa kula ni wewe mwenyewe... na mimi nmejilea hivyo hivyo nashangaaga kuona namaliza kupika mtu anapeta mchele saa1 au 2

Sent from
Ukiangalia cha maana alichokuwa anafanya ni kuangalia tamthilia kwenye TV tu!
 
Mimi nakushauri kama mwanamke niliyeolewa ongea nae umwambie hupendi na kiafya kuchelewa kula sio vizuri halafu chunguza kinachosababisha achelewe kupika ukute kazi nyingi,kama ni hivyo tafuta namna ya kumpunguzia kazi lakini kama ni makusudi na inakukera sana akichelewa wewe uwe umelala ili kesho ajitahidi.
Kazi nyingi kama zipi? Hivi mwanamke anayejituma kazi nyingi zinatokaga wapi? Usafi wa nyumba kufua na kupika ndio kazi nyingi ukute hata watoto bado hamna😅 hapo! Kuoa slayqueen ni kujitaftia mabalaa sana
 
Sisi tunapenda wanawake warembo haswaa. Na sasa hao ndio wako namna hiyo. Na kama si mrembo, binafsi hata sina hamu ya penzi.. na sitaki kuoa mke ambaye sina hamu na penzi lake.
Hahahahahah warembo sindio hao waliobandika makucha kama majini?
 
Acha gubu mbona hilo swali halina ubaya kabisa
Maana vyakula ni kubadilisha basi uwe unamuwahi unasema leo nataka kula chakula flan
Acha gubu nyau wee
Ina maana na wewe huwa unamsubiria kidume aje ndio uanze kumuuliza swali la kipuuzi kama hilo mtu mwenye njaa? Mbona mnatutaftaga sababu sana nyie?

Raha ya mke awe anajiongeza anajua cha kukupikia daily ili ufurahie. You don’t wanna plan that shyt we unatamani ukirudi ukute mambo mezani ufurahie chakula kitamu kilichoandaliwa special kwa ajili yako.

Kama ambavyo mnapenda Kupewa zawadi kwa suprise ama hela ndivyo ambavyo tunainjoy kukuta tumepikiwa.
 
Enzi za shule uteseke kama hivyo unarudi zako shule unanjaa unapita jikoni unakuta hakuna dalili ya kuni kupasuliwa na majivu yamepoa kabisa, ukiuliza una ambiwa hapa ni kwako! 😀😀😀

Halafu kwenye ndoa unakutana na same experience!
Ndo maana wanaume tunakufa mapema😂😂
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unatamani ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Ongea naye, kila jambo liwe na wakati wake, la sivyo itakuwa ni vurugu maisha yenu yote.
Ndoa ina mambo mengi, ikiwamo mawasiliano kati ya wanandoa.
 
bora hivyo anaanza kupika
Wangu ndo kwanza anakuuliza tupike nini MUMEWANGU

Amna swali linaloniudhi kama hilo Tupike nini mumewangu

huwa sijibu natoka zangu nje tu kupunga upepo na anifati tena 7bu anajua kashanivuruga
lakini cha kushangaza baada siku 2 anarudia tena hvyohvyo
Nishasema weee nimechoka
[emoji114][emoji2969]
Mawasiliano ni muhimu, mueleze chochote atakachotayarisha kitatumika, la kama kuna utakachokuwa na hamu nacho utamtaarifu ili kuepuka kutoelewana kati yenu. Kama ambavyo umeona, hajifunzi lolote kutokana na jinsi unavyochukizwa na hilo swali, suluhisho ni kuongea na si kuzila na kukaa kimya, asipoelewa mnachoongea na kukubaliana hapo itakuwa ni tatizo jingine.
 
lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Huyo mtu kwa mfano ni housegirl, mke au girlfriend?? Hapa nimechukulia "mtu" ni jinsia ya kike..
 
Unatoka kazini jioni umechoka, unatamani ukifika home ukaoge ukute chakula mezani, lakini ile unafika mtu ndio anaanza kupika chakula, mpaka kuiva masaa mawili mbele dah!
Ndugu yangu usisahau kua mkeo io mpishi wako, yeye kukupikia anakusaidia kwahiyo usichukulie poa msaada anaokupa. Pili usisahau wanawake wana majukumu mazito sana ya kuratibu na kutekeleza shughuli za nyumbani kuzidi hata hizo zako za ofisini. Wewe kupata mshahara na kuleta pesa nyumbani sio suluhisho la mambo yote. Msaidie mkeo, ukirudi msosi bado angalia kile umachoweza kumsaidi ili mule mapema. Acha kumlalamikia kisa tu unaleta matumizi nyumbani.
 
Ina maana na wewe huwa unamsubiria kidume aje ndio uanze kumuuliza swali la kipuuzi kama hilo mtu mwenye njaa? Mbona mnatutaftaga sababu sana nyie?

Raha ya mke awe anajiongeza anajua cha kukupikia daily ili ufurahie. You don’t wanna plan that shyt we unatamani ukirudi ukute mambo mezani ufurahie chakula kitamu kilichoandaliwa special kwa ajili yako.

Kama ambavyo mnapenda Kupewa zawadi kwa suprise ama hela ndivyo ambavyo tunainjoy kukuta tumepikiwa.
Hapana si mtu unamuuliza kwa simu kabla hajaja home nikupikie nini akij anakuta chakula tayari
Kuna vyakula vya kupika fasta mfano yupo njian ndio unatenga maji ya ugali akifika anakula ugali fresh
Haya nawaachia mlooana
 
Nipikie pizza baragumu😅

Kumbe hujaolewa bado😎
 
Back
Top Bottom